Kama wewe ni mmoja wa watu ambao hupakua kwa sana video na audio basi makala hii itakusaidia sana. Kupitia makala hii nitaenda kushare na wewe app tatu ambazo unaweza kutumia kuweza kudownload video yoyote na audio kutoka kwenye mtandao wowote kwa haraka.
Kwa kutumia app hizi hutoshindwa kudownload video yoyote kutoka kwenye mtandao wowote ule, iwe ni mtandao wa YouTube, TikTok, Instagram, Facebook au mtandao mwingine wowote. Pia utaweza kudownload audio kutoka kwenye mitandao mingine mbalimbali kama vile youtube na mitandao mingine. Basi bila kuendelea kupoteza muda twenda moja kwa moja kwenye makala hii.
TABLE OF CONTENTS
Download Video na Audio Kupitia InsTube
Kama wewe ni unapenda kudownload video kutoka kwenye mitandao mbalimbali kama vile TikTok, YouTube na mitandao mingine ya kijamii basi unaweza kujaribu app hii ya InsTube, app hii haipatikana kupitia soko la Play Store lakini ni moja kati ya app bora sana ya kudownload video pamoja na audio kutoka mitandao mbalimbali. Unaweza kujaribu app hiyo kwa kudownload hapo chini.
Download Video na Audio Kupitia Videoder
Videoder ni app nyingine ambayo inaweza kukusaidia kudownload video na audio kwa urahisi na haraka. App hii inapatikana kwenye mfumo wa Android na mfumo wa Windows. App hii ni app bora ya kudownload video na audio kutoka kwenye mtandao wa YouTube na mitandao mingine ya kijamii. Binafsi natumia app hii kupakua video kutoka kwenye mtandao wa Instagram hadi leo.
Download Video na Audio Kupitia SnapTube
Snaptube ni app nyingine bora sana ya kudownload video kwa urahisi na haraka, app hii ni nzuri sana na inaweza kukusaidia kupakua nyimbo mpya au video kutoka kwenye mitandao kama YouTube na mitandao mingine kama hiyo. Unaweza kupakua video zote kwa urahisi sana na utaweza kuhifadhi video hizo kwenye simu yako moja kwa moja.
Na hizo ndio app 3 ambazo unaweza kuzitumia kupakua video yoyote kwa urahisi na haraka. Kama unataka kujua njia bora ya kupakua nyimbo mpya za hapa Tanzania kwa urahisi na haraka basi unaweza kusoma makala yetu iliyopita hapa. Kama unataka kujifunza zaidi njia bora za kufanya mambo mbalimbali kwa haraka unaweza kutembelea channel yetu ya Tanzania Tech hapa.