Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Jinsi ya Kujua Jina la Nyimbo Yoyote kwa Kutumia Simu Yako

Sasa fahamu jina la nyimbo yoyote kwa urahisi kwa kutumia simu yako
Jinsi ya Kujua Jina la Nyimbo Yoyote kwa Kutumia Simu Yako Jinsi ya Kujua Jina la Nyimbo Yoyote kwa Kutumia Simu Yako

Kama wewe ni mpenzi wa muziki kama mimi basi ni lazima kuna wakati umesikia nyimbo mahali na inawezekana umeipenda sana lakini tatizo linakuja kuwa hujui jina la nyimbo hiyo na hii inaweza kuzuia wewe kushindwa kupata nyimbo hiyo kwa ajili ya kusikiliza tena au kudownload.

Kuliona hilo leo nimekuletea njia mpya na rahisi ambayo inaweza kukusaidia kujua jina la nyimbo yoyote kwa kutumia simu yako ya Android au iOS. Kumbuka njia hii inaweza kusaidia sana kama umesikia nyimbo ikiwa inaimba na unataka kujua jina la wimbo huo kwa ajili ya kudownload au kurudia kusikiliza tena. Basi bila kupoteza muda zaidi twende moja kwa moja nikuonyeshe njia hizi.

Advertisement

Jinsi ya Kujua Jina la Nyimbo Yoyote kwa Kutumia Simu Yako

Musixmatch

Kama wewe ni mpenzi wa muziki basi inawezekana tayari unajua app hii, Musixmatch ni moja kati ya app bora sana za kusaidia kutambua nyimbo yoyote kwa urahisi na haraka. Uzuri wa app hii ni kuwa, ina uwezo wa kutambua nyimbo za aina zote ikiwa pamoja na nyimbo za bongo flava na nyimbo nyingine zote za hapa Tanzania. Mbali na hayo, pia unaweza kupata mashairi ya nyimbo mbalimbali za wasanii pamoja na mambo mengine mengi. Kama wewe ni mpenzi wa muziki na bado huna App hii kwenye simu yako basi nakushauri pakua sasa app hii.

SoundHound

Njia nyingine ambayo unaweza kutumia kujua jina la nyimbo kwa kutumia simu yako ni pamoja na app hii ya SoundHound. App hii ni bora sana kwa sababu inakupa urahisi sana wa kutambua nyimbo na unaweza kuongea na app hiyo kwa kuiuliza jina la nyimbo na app hiyo itakwambia moja kwa moja. Unacho takiwa kufanya ni kusema “Ok Hound, what’s the song?” na app hii itakwambia jina la nyimbo hiyo ikiwa pamoja na msanii aliye imba.

Beatfind

Njia nyingine ni kutumia app ya Beat Find, app hii pia nayo inaweza kukusaidia kupata jina la nyimbo yoyote ikiwa pamoja na kupata mashairi ya nyimbo hizo. App hii kwa sasa inapatikana kwenye simu za mifumo ya Android pekee hivyo kama wewe unatumia iOS basi unaweza kujaribu app nyingine hapo juu.

Music Recognition
Price: Free

Shazam

Kama wewe ni mfuatiliaji wa Tanzania Tech basi najua ni lazima unajua app hii ya Shazam, app hii miaka ya karibuni ili nunuliwa na kampuni ya Apple na hii ni kwa sababu app hii ni moja kati ya app ya muda mrefu ambayo inasaidia kupata jina la nyimbo yoyote. App hii ni rahisi kutumia na kama nilivyo kwambia app hii ni ya siku nyingi sana hivyo inakuja na datakazi kubwa sana hivyo inaweza kutambua nyimbo nyingi kwa haraka na kwa urahisi.

Natumaini hadi hapo utakuwa umefanikiwa kuapata app ambayo itaweza kusaidia kujua jina la nyimbo yoyote ambayo unaipenda. Kama umesha fanikiwa kujua jina la nyimbo unayo ipenda unaweza kupakua nyimbo hiyo kwa urahisi kwa kufuata njia hizi hapa. Kama pia unataka kudownload nyimbo mpya za bongo unaweza kusoma hapa, pia kama unataka kudownload video yoyote kutoka mtandao wa YouTube basi hakikisha unasoma makala hii hapa.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use