Kama wewe ni mmoja wa watu ambao wanafanya kazi kama ya ubunifu wa michoro kupitia kompyuta, au unahitaji laptop yenye uwezo maalum kwa ajili ya kazi maalum basi unahitaji laptop ya MacBook.
Kuliona hili leo nimeamua kukuletea list hii fupi ya laptop za macbook ambazo unaweza kuzipata hapa Tanzania kwa bei nafuu, kumbuka laptop hizi zina tofautiana bei kwa kila moja kulingana na sehemu ambayo una nunua laptop hiyo. Pia bei inaweza kutofautiana kutokana na hali ya kompyuta yaani mpya au iliyotumika. Basi baada ya kusema hayo twende tukaangalie laptop hizi.
MacBook Pro Retina Display (2015)
Kama wewe ni mtu unayetaka laptop ya macbook yenye uwezo mzuri kwa bei nafuu basi laptop hii ya MacBook Pro (2015) yenye Retina Display ni laptop nzuri sana kwako. Uzuri wa laptop hii hauishii kwenye uwezo wake na sifa zake bali laptop hii ni bora sana kwa wale wanaofanya kazi za ubunifu wa michoro kupitia kompyuta (Graphics Design), pia laptop hii inafaa kwa watengenezaji wa programu mbalimbali kutokana na sifa zake.
Sifa za MacBook Pro (2015) with Retina Display
- Ukubwa wa Kioo – Inch 13.3
- Uwezo wa CPU – Intel Core i5
- Uwezo wa Processor – 2.7 GHz
- Uwezo wa RAM – 8 GB 1600 MHz LPDDR3
- Uwezo wa Graphics – Intel HD Graphics 6100 (GB 1.5 = 1536MB)
- Uwezo wa HDD/SDD – Inatumia SSD yenye uwezo wa hadi TB 1 (Bei inaweza kubalilika kulingana na ukubwa wa HDD/SSD).
Bei ya MacBook Pro (2015) with Retina Display
Kwa upande wa bei, bei yake inategemeana na ukubwa wa uhifadhi wa hard disk, unaweza kupata laptop hii kwa hapa Tanzania kuanzia TZS 2,400,000 hadi TZS 2,100,000. Laptop hii inapatikana kwa uhifadhi kuanzia SSD ya GB 128 na kuendelea hadi Terabyte TB 1.
MacBook Air (Mid – 2017)
Kama wewe ni mwanafunzi au ni mtu ambaye unafanya kazi ambazo unakuwa uko kwenye mwendo kila wakati basi unahitaji laptop hii ya MacBook Air (Midi-2017). Laptop hii ni bora kwa sababu ni nyepesi na ina muonekano mzuri sana hasa kwa watu ambao hutegemea kufanya kazi mahali popote bila kujali kuwa ni ofisini au ni sehemu nyingine. Kingine kizuri kuhusu laptop hii ni uwezo wake kwani laptop hii inakuja na sifa zifuatazo.
Sifa za MacBook Air (Midi-2017)
- Ukubwa wa Kioo – Inch 13.3
- Uwezo wa CPU – Intel Core i5 Dual-Core
- Uwezo wa Processor – 1.8 GHz
- Uwezo wa RAM – 8 GB 1600 MHz LPDDR3
- Uwezo wa Graphics – Intel HD Graphics 6000 (GB 1.5 = 1536MB)
- Uwezo wa HDD/SDD – Inatumia SSD yenye uwezo wa hadi TB 1 (Bei inaweza kubalilika kulingana na ukubwa wa HDD/SSD).
Bei ya MacBook Air (Midi-2017)
Kwa upande wa bei inategemeana na ukubwa wa uhifadhi wa hard disk, ila unaweza kupata laptop hii kwa hapa Tanzania kuanzia TZS 2,100,000 hadi TZS 1,800,000. Laptop hii inapatikana kwa uhifadhi kuanzia SSD ya GB 128 na kuendelea hadi Terabyte TB 1.
MacBook Pro (2012)
Kwa upande mwingine kama wewe ni mtu ambaye unataka kompyuta bora ya kufanya kazi za kawaida kama kazi za ofisini na kazi nyingine kama hizo basi MacBook Pro (2012) ni laptop bora sana kwako. Laptop hii inakuja na uwezo wa kawaida lakini pia ni moja kati ya laptop zenye uwezo mkubwa wa kudumu sana, sifa nyingine za MacBook Pro (2012) ni kama zifuatazo.
Sifa za MacBook Pro (2012)
- Ukubwa wa Kioo – Inch 13.3
- Uwezo wa CPU – Intel Core i5 Dual-Core
- Uwezo wa Processor – 2.9 GHz
- Uwezo wa RAM – 4 GB 1600 MHz LPDDR3
- Uwezo wa Graphics – Intel HD Graphics 4000 (GB 1.5 = 1536MB)
- Uwezo wa HDD/SDD – Inatumia HDD yenye uwezo wa hadi TB 1 (Bei inaweza kubalilika kulingana na ukubwa wa HDD/SSD).
Bei ya MacBook Pro (2012)
Kwa upande wa bei, MacBook Pro (2012) unaweza kuipata kwa hapa Tanzania kuanzia TZS 1,400,000 hadi TZS 1,000,000. Kumbuka toleo la laptop hii linatumia hard disk ya HDD na sio SSD. Pia bei ya laptop inaweza kubadilika kulingana na uwezo wa uhifadhi wa ndani wa laptop.
Na hizo ndio laptop ambazo nadhani unaweza kuzipata kwa bei rahisi kwa hapa Tanzania, kumbuka bei inaweza kuwa tofauti kulingana na mambo mbalimbali kwa mfano kama laptop hiyo sio mpya basi unaweza kuipata kwa bei nafuu zaidi, pia kama laptop inatumia HDD na sio SSD basi pia unaweza kupata kwa bei urahisi zaidi.
Kumbuka, kama wewe ni mmoja wa watu wanaoweza kununua vitu kupitia tovuti kama amazon, basi unaweza kupata laptop za macbook kwa bei rahisi zaidi na zikiwa ni matoleo mapya zaidi. Hakikisha unasoma makala jinsi ya kununua kitu kupitia Amazon hapa na uhakika baada ya kuweza kununua bidhaa kupitia tovuti hiyo basi utaweza kupata laptop bora ya macbook kwa bei rahisi zaidi.