Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Hizi Hapa Hatua kwa Hatua Jinsi ya Kufanya Manunuzi Amazon

Njia hizi zinaweza kusaidia kuanzisha biashara ya kununulia watu bidhaa
Hizi Hapa Hatua kwa Hatua Jinsi ya Kufanya Manunuzi Amazon Hizi Hapa Hatua kwa Hatua Jinsi ya Kufanya Manunuzi Amazon

Amazon ni moja ya kampuni kubwa sana inayofanya biashara mbalimbali ikiwa pamoja na biashara ya kuuza vitu mbalimbali mtandaoni. Kwa kawaida kupitia tovuti ya Amazon unaweza kununua bidhaa mbalimbali unapokuwa kwenye nchi yoyote, lakini ukweli ni kwamba changamoto huja kwenye njia ya kuweza kupata mzigo wako moja kwa moja.

Kuliona hili leo hapa Tanzania Tech tumewaletea njia ambayo sisi tumekuwa tukitumia kuweza kununua baadhi ya bidhaa kupitia mtandao wa Amazon na kuweza kuzipata hapa nchini Tanzania. Kupitia njia hii pia unaweza kuanzisha biashara ya mtandaoni ambayo inaweza kukusaidia kupata kipato kizuri kwa kusaidia watu kununua bidhaa kupitia tovuti ya Amazoni.

Advertisement

Kitu cha msingi unacho takiwa kujua ni kuwa, angalau unahitaji kuwa na sanduku la posta ambao unaweza kutumia kupata mizigo ambayo sio mikubwa, ingawa pia unaweza kutumia huduma za kuletewa mzigo wako mpaka ulipo kama sisi tunavyofanya. Basi bila kuendelea kupoteza muda twende kwenye hatua hizi.

Kingine ambacho ni muhimu kujua ni kuwa, kuna baadhi ya bidhaa ambazo unaweza kununua direct kutoka Amazon na ukaletewa moja kwa moja. Lakini pia zipo bidhaa ambazo huwezi kununua na kuletewa moja kwa moja hivyo ni lazima kutumia kampuni ya kuweza kukuletea mzigo wako moja kwa moja kutoka marekani au mahali mzigo ulipo. Hivyo basi kwa kuliona hilo napenda nikuelekeze njia mbili ambazo ndio unaweza kuzitumia kununua bidhaa kupitia Amazon.

Kununua Moja kwa Moja Kutoka Amazon

Kuna baadhi ya bidhaa anaweza kuzipata moja kwa moja kutoka Amazon hadi hapa nchini Tanzania, kitu cha msingi ambacho unatakiwa kufanya ni kutembelea sehemu ya tovuti ya amazon ambayo inazo bidhaa ambazo zinaweza kutumwa kwenye nchi mbalimbali ikiwemo Tanzania.

Unaweza kutembelea sehemu ya tovuti hiyo HAPA, lakini pia kumbuka ni muhimu kuangalia sehemu ya “shipping fee” kwenye bidhaa ili kujua kiwango cha fedha unachotakiwa kulipa kwa ajili ya gharama usafirishaji wa mzigo wako.

Hizi Hapa Hatua kwa Hatua Jinsi ya Kufanya Manunuzi Amazon

Kama unavyoweza kuona kwenye picha hapo juu, kama utatumia link hiyo basi huu ndio ujumbe utakao letewa wenye kuonyesha kuwa unaangalia bidhaa ambazo zina uwezo wa kutumwa kuja kwako kama upo nchini Tanzania.

Hizi Hapa Hatua kwa Hatua Jinsi ya Kufanya Manunuzi Amazon

Kwa urahisi zaidi unaweza kutumia app ya Amazon kufungua link hiyo na utapelekwa moja kwa moja kwenye ukurasa huo ndani ya App hiyo, kama bado huna app ya Amazon unaweza kupakua apps za amazon hapo chini.

Amazon – Android

Amazon Shopping
Price: Free

Amazon – iOS

‎Amazon Shopping
Price: Free

Kwa mfano, Kama unavyoweza kuona kwenye bidhaa hapo chini, kwa mimi ambaye nipo hapa Dar es salaam naweza kupokea mzigo wangu ndani ya siku saba mpaka siku 10 pale nitakapo nunua bidhaa kwenye ukurasa huo.

Hizi Hapa Hatua kwa Hatua Jinsi ya Kufanya Manunuzi Amazon

Na hiyo ndio njia ya kwanza unayoweza kutumia kuweza kununua bidhaa kupitia tovuti ya Amazon, sasa ipo njia ya pili ambayo hii itakusaidia kuweza kununua bidhaa yoyote kutoka kwenye tovuti ya Amazon, isipokuwa bidhaa kama madawa, mimea, kemikali na vitu vingine kama hivyo.

Kununua kwa Kupitia Kampuni za Kutuma Mizigo

Kifupi ni kwamba njia hii ya kununua bidhaa kutoka Amazon sio njia ya bei rahisi kwani huduma hizi hutolewa na makampuni mbalimbali ambayo mwisho wa siku nayo ni lazima kutengeneza faida hivyo ni muhimu kujua kuwa njia hii sio ya bei rahisi moja kwa moja.

Sasa kama upo hapa Tanzania, unaweza kutumia kampuni ya EasybuyAfrica kwa urahisi zaidi kwani kampuni hiyo imekuwa na uwezo mkubwa wa kutuma mizigo kwa bei nafuu na unaweza kupata mzigo wako kwa urahisi na kwa haraka hasa kama uko Dar es salaam. Unaweza kuangalia video hapo chini jinsi huduma hiyo inavyofanya kazi.

Sasa ili kununua kitu kwa kutumia nji ya tovuti ya easybuyafrica, kwanza unatakiwa kutengeneza akaunti yako kupitia tovuti hiyo hapa, kisha baada ya hapo ingia kwenye tovuti ya amazon na tafuta bidhaa unayo hitaji kisha chukua link ya bidhaa hiyo, jina la bidhaa, bei yake pamoja na kipengele (Category) ambacho bidhaa hiyo inapatikana. Baada ya hapo weka link ya bidhaa hiyo kwenye chumba maalum kwenye tovuti ya easybuyafrica kisha bofya Buy4Me.

Hizi Hapa Hatua kwa Hatua Jinsi ya Kufanya Manunuzi Amazon

Baada ya hapo jaza sehemu zote za muhimu kama ambavyo inaonyesha kwenye picha hapo chini, hakikisha kuwa kila sehemu iliyo na alama ya nyota nyekundu imejazwa kwa usahihi, kisha baada ya hapo bofya sehemu ya Calculate na moja kwa moja utapata bei ya usafirishaji wa bidhaa unayotaka kununua.

Hizi Hapa Hatua kwa Hatua Jinsi ya Kufanya Manunuzi Amazon

Hizi Hapa Hatua kwa Hatua Jinsi ya Kufanya Manunuzi Amazon

Unaweza kufanya malipo kwa kutumia njia mbalimbali za malipo ikiwa pamoja na njia za malipo kwa kutumia huduma za simu pamoja na njia za kulipia cash kupitia ofisi zao. Kwa Tanzania nadhani hii ndio njia rahisi zaidi kwani inakupa uhakika wa kupata mzigo wako kwa haraka na urahisi.

Na hizo ndo njia ambazo unaweza kuzitumia kuweza kununua bidhaa mbalimbali kupitia tovuti ya Amazon, kama unataka kujua zaidi kuhusu njia bora za kununua bidhaa mtandaoni basi hakikisha unaendelea kutembelea Tanzania Tech kwani sasa tutakuwa tunakuletea makala hizi ambazo natumaini zinaweza kukusaidia sana kununua bidhaa kwa haraka mtandaoni.

9 comments
  1. Kaka asante kwa somo zuri
    Naomba siku mmoja uzungumzie jinsi ya kulipia kwa MasterCard au visa
    Maana elimu Bado inaitajika pia jinsi ya kulipa kwa PayPal
    Asante

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use