Kampuni ya Google Yafikisha Miaka 20 Toka Kuanzishwa

Kutoka kampuni isiyo na dhamani kabisa hadi Tsh Trilioni 252
Google Kufikisha Miaka 20 Google Kufikisha Miaka 20

Kampuni ya Google ni moja kati ya kampuni kubwa sana kwa sasa, kampuni hii imetoka mbali sana na hapo jana kampuni ya Google imetimiza miaka 20. Kwenye miaka hiyo 20 kampuni ya Google imebadilika sana kutoka kampuni iliyoanzishwa na watu wawili kwaajili ya majaribio, hadi kufikia kampuni yenye thamani ya dollar za marekani bilioni $110.8 ambayo ni sawa na Tsh Trilioni 252.

Kwenye miaka hii ishirini 20 ya Google hebu twende tukaangalie historia ya kampuni hii ilipotoka. Kwa kuanza labda turudi nyuma kidogo hadi mwaka 1996, Mwaka huo wagunduzi kutoka chuo cha Stanford cha nchini marekani Sergey Brin na Larry Page walianza kufanyia kazi project yao ya kwanza ambayo ilikuwa inahusu mambo ya tovuti na jina la project hiyo lilikuwa Backrub.

Advertisement

Backrub ilikuwa ni project ya mtandaoni ambayo ilibuniwa maalum kwaajili ya kutathmini umuhimu wa tovuti au (Domain) kwa kuangalia kiasi cha link (backlink) kwenye domain au tovuti kwa ujumla. Baada ya ubunifu huu Sergey Brin na Larry Page walibadilisha jina la project hiyo na kuwa Google.

Jina Google lilitokana na neno la hisabati ambayo maana yake ni moja (1) na sufuri miamoja (100), kutoka kipindi hicho Google ilipata kujulikana na watu wengi hadi hapo mwaka 1998 ambapo Google ilipata mwekezaji wa kwanza anayeitwa Andy Bechtolsheim ambaye ni mgunduzi wa kampuni ya Sun Microsystems, ambaye yeye aliwekeza dollar za marekani $100,000 ambayo kwa sasa ni sawa na takribani Tsh milioni 230 kwa kipindi hicho lazima ilikuwa ni pungufu ya hapo.

Baada ya kupata pesa hizo waanzilishi hao wa Google, Sergey Brin na Larry Page walianzisha ofisi yao ya kwanza ambayo ilikuwa ni sehemu ya kuhifadhi vitu (Garage) ambayo ilikuwa ikimilikiwa na Susan Wojcicki ambaye sasa ni mfanyakazi wa Google na mkurugenzi mtendaji wa YouTube.

Kuanzia hapo Google imekuwa kutoka kampuni changa hadi kufikia sasa na ukweli ” ukiona nyani mzee ujue amekwepa mishale mingi ” historia ya Google haijagubikwa na mambo mazuri tu na uhakika yapo mambo mengi sana ambayo yalikuwa yawakatishe tamaa wabunifu wa kampuni hiyo mengine yameandikwa na mengine hayaja andikwa. Kwa mfano kampuni moja inayoitwa Excite ilikataa kununua kampuni ya Google kipindi hicho bado changa lakini sasa loh.. na hakika wanajuta.

Historia ya Google ni fundisho kuwa inawezekana kwa sasa jambo unalo lifanya linaonekana halina dhamani ila na hakika ukiendelea kufanya jambo hilo bila kujali maneno ya watu na bila kukatishwa tamaa na uhakika lazima siku moja utakuja kufanikiwa.

Kama unataka kujua mambo mengine ambayo yanahusu kampuni ya Google ambayo pengine ulikuwa huyajui unaweza kusoma makala yetu ya je wajua kupitia hapa hapa Tanzania Tech, Kwa habari zaidi za teknolojia hakikisha unatembelea Tanzania Tech kila siku.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use