Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Jinsi ya Kutumia Sehemu Mpya ya IGTV kwenye Instagram

Fahamu yote ye muhimu Kuhusu sehemu mpya ya IGTV
igtv instagram igtv instagram

Baada ya tetesi za muda mrefu hapo jana mida ya saa tatu instagram ilitangaza kwa haraka kuhusu ujio wa sehemu mpya ya IGTV. Kama ulikuwa unajiuliza IGTV nini basi kupitia makala hii utaweza kufahamu kuhusu yote ya muhimu kuhusu sehemu hiyo ikiwa pamoja na jinsi ya kuitumia.

  • IGTV ni nini.?

Tukianza kuhusu nini maana ya IGTV hii ni sehemu mpya ndani ya mtandao wa instagram sehemu hii itakusaidia wewe mtumiaji wa Instagram kuweza kutuma video za muda mrefu kuanzia sekunde 15 hadi lisaa limoja.

Advertisement

  • IGTV inapatikana wapi..?

Sehemu hii mpya ya IGTV inapatikana kupitia sehemu mbili tofauti, unaweza kuipata kupitia App ya Instagram karibia na sehemu ya Stories juu ambapo utaona kitufe kipya cha TV. pia unaweza kuipata kwa kupakua app za IGTV za Android na iOS kupitia masoko ya App Store na Play Store. Unaweza kupakua App hizo link ziko hapo chini.

IGTV – Android

IGTV – iOS

  • Je Unaruhusiwa kuweka Video za Muda Gani..?

Kwa mujibu wa tovuti ya maswali na majibu ya mtandao wa Instagram, Mtumiaji wa kawaida ataweza kutuma video yenye muda kuanzia sekunde 15 hadi dakika 10. Kwa wale ambao wanazo akaunti ambazo ziko Verified au Akaunti zenye watu wengi kwa mujibu wa instagram wataweza kutuma video za hadi dakika 60 ambayo ni sawa na lisaa limoja. Kama unataka kuweka video za lisaa limoja unalazimika kuweka video zako kwa kutumia kompyuta.

  • Je Unaruhusiwa kutuma Video za Aina Gani..?

Kuhusu aina ya video instagram wamesisitiza kuwa unatakiwa kutuma video za wima Horizontal na zenye mfumo wa MP4 pamoja na Aspect ratio ya kiwango cha chini cha 4:5 hadi 9:16. Pia watumiaji wote wataweza kuweka video zenye Quality hadi ya 4K. Pia video ambazo hazita fuata vigezo na masharti ya Instagram zitaondolewa haraka.

  • Je Vipi Kuhusu Ukubwa wa Video..?

Instagram imesema kuwa watumiaji wa Sehemu ya IGTV ambao wataruhusiwa kuweka video za sekunde 15 hadi dakika 10 wanatakiwa kuhakikisha video zao zisizidi kiwango cha MB 650, wakati wale wanaoruhusiwa kuweka video za hadi lisaa limoja video zao zisizidi GB 5.4.

  • Je Unawezaje kutengeneza Channel ya IGTV..?

Kwa sasa sehemu hii bado sijaweza kuiona ndani ya app ya Instagram, lakini tayari iko kwenye app zake maalum za Android na iOS. Hapa nitakuelekeza jinsi gani ya kutengeneza Channel ya IGTV kwenye Kompyuta, Android pamoja na iOS. Ni muhimu kujua kuwa unahitaji kutengeneza Channel ili uweze kuanza kuweka video zako kupitia sehemu hiyo ya IGTV.

Android na iOS

  1. Kwanza pakua App ya IGTV kupitia link hapo juu kisha install
  2. Fungua App hiyo kisha bofya sehemu ya settings liyochorwa pembeni ya picha ya profile yako
  3. Kisha bofya Create Channel
  4. Baada ya hapo utaweza kuanza kuweka video zako moja kwa moja.

Kwa Kompyuta

  1. Ingia kwenye kivinjari cha kompyuta yako kisha tembele instagram.com
  2. Ingia kwenye akaunti yako kisha bofya Profile kisha bofya sehemu ya IGTV
  3. Kisha bofya sehemu iliyo andikwa Create Channel fuata maelekezo na utaweza kutengeneza channel yako tayari kuanza kuweka video.
  • Je Unatumiaje Sehemu Hii ya IGTV..?

Baada ya kumaliza hatua zote za kutengeneza channel ya IGTV, Sasa unaweza kuendelea kuweka video zako kwa kufuata hatua hizi.

Ndani ya Instagram App au App ya IGTV

  1. Ndani ya App ya Instagram bofya kifufe cha IGTV au kwa kutumia App ya IGTV washa app hiyo.
  2. Baada ya hapo bofya picha ya profile yako iliyoko upande wa kulia.
  3. Kisha bofya kitufe cha jumlisha na chagua video kisha bofya next.
  4. Weke kichwa cha Habari cha video yako weke maelezo ambayo unaweza kuweka na link kwenda kwenye tovuti yako au mahali popote kisha pia unaweza kuruhusu kutuma video hiyo kwenye akaunti yako ya Facebook ambayo ume link nayo.
  5. Baada ya hapo maliza kwa kubofya Post.

Kwa kutumia Kompyuta

  1. Fungua kivinjari cha kompyuta yako kisha tembelea Instagram.com
  2. Ingia kwenye akaunti yako kisha bofya profile kisha chagua IGTV.
  3. Baada ya hapo bofya Upload Video
  4. Bofya kitufe cha jumlisha kisha chagua video kwenye kompyuta yako.
  5. Weka kichwa cha habari cha video, kisha weka maelezo ya video ambayo pia unaweza kuweka link na pia kushare kwenye mtandao wa Facebook.
  6. Baada ya hapo maliza kwa kubofya Post.

  • Vipi Kuhusu Kupata Pesa Kutokana na Video

Instagram imesema kwa sasa bado hakuna matangazo yoyote yatakayo kuwa yanapita kwenye sehemu ya Video ya IGTV, hivyo kwa sasa hakuna mtu yoyote atakaye kuwa analipwa pesa yoyote kutokana na video zake. Lakini kupitia kwenye mkutano wa uzinduzi wa sehemu hii, msemaji wa Instagram alisema hiyo ni sehemu nzuri sana ya kufanya matangazo hivyo pengine watumiaji wategemee kuona matangazo siku za karibuni.

  • Kuna Tofauti Gani Kutumia IGTV kwenye Instagram na App ya IGTV

Bado instagram haijaweka wazi kuhusu tofauti iliyopo, ila kwa muonekano tu App ya IGTV ni rahisi kutumia na haraka zaidi kuliko sehemu ya IGTV kwenye App ya Instagram.

Kwa sasa hayo ndio ya muhimu ya kujua kuhusu sehemu ya IGTV iliyo zinduliwa rasmi hapo jana, kwa hapa Tanzania na Afrika mashariki kwa ujumla, tayari app za IGTV zipo kwenye masoko yote ya App Store na Play Store, unaweza kupakua sasa na kuanza kutumia sehemu hiyo mpya kutoka mtandao wa Instagram. Kama kuna mahali umekwama au kuna chochote unataka kujua kuhusu IGTV unaweza kuuliza kupitia sehemu ya maoni hapo chini au tembele ukurasa wa instagram hapa kuweza kujua zaidi kuhusu sehemu hiyo.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use