Sasa Twitter Inaruhusu Kupost Mlolongo wa Tweet kwa Pamoja

Sasa utaweza kupost muendelezo wa tweet kwa pamoja
twitter-app twitter-app

Wakati Twitter inaendelea kuwapa watumiaji wake njia na uwezo zaidi wa kutoa mawazo yao kupitia mtandao wa Twiiter, hivi karibuni kwa mara nyingine Twitter imeleta njia nyingine ya kuongeza uwezo wa kupost tweet yako yenye mlolongo wa Tweet au Thread.

Hapo mwanzo ili kupost tweet yenye mlolongo ilikuwa inakupasa kuweka alama za 1/1 na kuendelea ili tweet zako ziwe kwenye mlolongo. Lakini sasa Twiiter imeleta kitufe kipya mabacho utaweza kupost mlolongo wa Tweet kwa pamoja pale unapoanza kupost.

Advertisement

Kwa kubofya kitufe cha duara chenye jumlisha kilichopo pembeni ya Tweet utaweza kuongeza mlolongo wa tweet na kisha utaweza kupost zote kwa pamoja. Kwa mujibu wa mtandao wa Thenextweb utaweza kuongeza mlolongo wa Tweet hadi mara 25.

Hata hivyo Sehemu hizi tayari zimesha anza kuja kwenye programu za twitter za mifumo yote ya Android pamoja na iOS, kama bado ujapata sehemu hii ingia kwenye soko la programu kwenye simu yako kisha angalia update za programu ya Twitter.

Nini maoni yako kuhusu maboresho haya kutoka twitter.. tuambie kwenye maoni hapo chini, Kwa habari zaidi za teknolojia hakikisha una download App yetu mpya ya Tanzania Tech kupitia Play Store na vilevile tembelea channel yetu ya Tanzania Tech kupitia Youtube ili uweze kujifunza zaidi mambo yote ya teknolojia kwa njia ya Video.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use