Jinsi ya Kuondoa Lock ya Android Bila Kuflash au Kureset Simu

Kama simu yako inayo Pattern au Lock ya aina yoyote na umesahau soma hii
kuondoa Lock kuondoa Lock

Kutokana na ulimwengu wa teknolojia kuwa mpana kila siku sio ajabu unaposikia mtu akikwambia nimesahau password au pattern za simu yangu, hii ikiwa ni matokeo ya teknolojia kuwa kubwa sana kiasi kwamba kila kitu unakuta kinatumia password hivyo kutokana wingi wa vifaa ni rahisi sana kusahau pattern au password yako. Kuliona hilo leo Tanzania Tech tunakuleta njia ya kuondoa pattern au password yoyote ile kwenye Android bila kupoteza data zako kabisa!.

Kwa kuanza ni vyema kujua vitu vichache ambavyo vita kusaidia. Njia hii itakusaidia endapo kama utakuwa umewasha USB Debugging kwenye simu yako (hii ni muhimu sana) bila kufanya hivi njia hii haita fanya kazi hivyo ni vyema ujue kuwa simu yako imewashwa USB Debugging sehemu hii inawashwa kwa kufuata njia hizi (bofya hapa kuzijua). Vilevile unatakiwa kuwa na ADB Drivers za simu yako ili kupata driver hizo Bofya hapa kisha download ADB Driver Installer install kwenye kompyuta yako kisha endelea kwa kufuata hatua hizi.

Advertisement

Baada ya kuinstall driver zako moja kwa moja download programu ya Android SDK Tools kwaajili ya Windows Hapa na kwaajili ya Mac Hapa na kama unatumia Ubuntu au chrome OS bofya Hapa, fungua programu hiyo kisha chagua na install programu hiyo kama inavyonekana kwenye picha hapo chini.

Ukisha maliza kuinstall fungua mahali ulipo install programu hiyo kisha fungua Android SDK Tools Users > App Data > Local > Android > Android-SDK > Platform-Tools kisha shikilia control kwenye keyboard ya kompyuta yako kisha right click kwa kurumia mouse yako kisha bofya open command window here.

 

Baada ya hapo sehemu ya command itafunguka chomeka simu yako kisha subiri kidogo kisha bofya hap chini kwenye view raw au bofya hapa kisha copy code hizo na paste kwenye command ya kompyuta yako uliofungua awali kisha bofya Enter kisha subiri kidogo kisha restart simu yako.

Kama code hizo hazitofanya kazi kwenye simu yako basi tumua code hizi hapa chini kujaribu tena kufungua simu yako, kama awali copy na paste kwenye command uliofungua awali kisha bofya Enter.

Baada ya kurestat simu yako utaona pattern au lock ya simu yako imeondoka kabisa na hapo utakuwa umewezesha simu yako kuondoa lock screen au pattern ya aina yoyote kwenye simu yako ya Android. Kama kuna mahali umekwama usisite kutandikia kwenye maoni hapo chini nasi tutakujibu moja kwa moja.

Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia usisahu kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja yote ya teknolojia kwa njia ya video.

21 comments
  1. Maoni*Naomba msaada wenu wataalamu wa simu,
    Simu yangu ina tatizo la kujiwasha data yenyewe ;nikizizima inajiwasha baada ya sekunde chache.Nimejaribu kui-restart bado tatizo liko palepale.Nifanyeje?

    1. Bloza unatumia laini gan na cha kufanya nenda kwny setting-more-access network halafu badilsha APN futaile ya zaman na weka mpya

  2. Maoni*mimi Simu Yangu Nikibonyeza Voice Up Na Power Buttun Kwa Pamoja Inaniletea Menu Tofauti Inaleta Hivi;
    MMI test
    Full Test
    Item Test
    Test Info
    Reset

  3. Mimi naitwa Dativa Majaliwa natumia simu aina ya infinix nilisahau pattern ikafungiwa sasa nitafanyaje kuifungua bila kutumia computer maana niko bukoba vijijini hamna mtu mwenye computer huku mswada wenu please

  4. Mm simu yangu nime flash na mkono ime kuja Google account kila Niki weka ina kataa naomba nifanyaje mpaka ifunge app

  5. habari mkuu, naomba unisaidie kujua, nitawezaje ku-set USB degugging wakati simu ukiwa locked? au kama sijaelewa naomba unieleweshe kuhusu hiyo setting ya USB debugging

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use