Wote tunajua kuna wakati unajikuta huwezi kutumia simu yako labda kutokana na muda mwingi unajikuta unafanya kazi kwenye kompyuta hivyo inakuwia vigumu kushika simu yako kila saa, kukusaidia katika hilo leo Tanzania Tech tunakuletea njia hii rahisi ya kuwezesha kupiga na kupokea simu yako kwa kutumia kompyuta yako.
Basi kwa kuanza hatua hizi unatakiwa kuwa na baadhi ya vitu vifuatavyo, unatakiwa kuwa na kompyuta ambayo ina uwezo wa kutumia wifi pia unatakiwa kuwa na simu ya android yenye uwezo wa kutumia wifi. Baada ya kuhakikisha una vitu vyote hivi basi unaweza kuendelea kwa kufuata hatua hizi rahisi.
Hatua ya kwanza hakikisha una internet ya kutosha kuweza kupakua programu hii kutoka Play Store, programu hii inaitwa Remote Phone Call Trial unaweza kudownload kwa ku-bofya hapo chini.
Kumbuka programu hii unaweza kutumia bure kwa muda wa siku 15 tu, kama utapenda kutumia zaidi programu hii inakubidi ununue programu hii ya kulipia na unaweza kutumia programu hii kwa muda wote utakao hitaji wewe. Baada ya kudownload programu hiyo kwenye simu yako basi ingia kwenye kompyuta yako kisha bofya hapa kudownload programu kwaajili ya kompyuta kisha install kwenye kompyuta yako na endelea kufuata hatua zingine.
Baada ya kudownload programu zote, washa programu zote za kwenye kompyuta pamoja na ile iliyoko kwenye simu yako kisha baada ya kuwasha programu zako utaona device IP na password hizo ziandike pembeni kwani utazingiza kwenye programu ya kwenye simu ambayo uliwasha awali, bofya sehemu ya add WiFi device kwenye programu hiyo ya simu alafu ingiza namba za device IP ambazo ulizi andika pembeni hapo awali, baada ya kuingiza device IP bofya ok kisha weka password kisha malizia kwa kuweka namba unazoziona kwenye kioo cha kompyuta yako baada ya kumaliza hatua zote hizo utakuwa umemaliza na uko tayari kutumia simu yako kwenye kompyuta.
Kwa mafunzo zaidi ya teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech kila siku au unaweza ku-download App ya Tanzania Tech kupitia Play Store, pia usisahau kujiunga nasi kupitia channel ya Tanzania tech kupitia youtube ili kujifunza maujanja ya teknolojia kwa njia ya video.
Nice
Karibu sana Ema
Hata mimi nimeipenda sana blog yenu
Asante sana diza endelea kutembelea Tanzania Tech
Sijawahi kuona tovuti bora kama hii endeleeni kukaza buti.
Nimefurahi sana imefanya kazi duhh kweli thanks.
Asante sana John. Karibu sana
Maujanja hayo hatari m nisha jua yote kuliko darasani mwalimu anavyo tu tichi Maoni*
Karibu sana Victor
Sita choka kamwe kushukuru blog ili kila mdu ninapo jifunza mambo tafauti fauti. Big-up na Mungu awawezeshe tena
Asante Sana Malisawa na Karibu sana
Hongereni sana kwa kazi nzuri ya kuelimisha watumiaji wa Laptop na Sim,kiukweli mmekua msaada mkubwa sana kwa sisi wadau na wapenzi wa vitu hivi.kikubwa msikate tamaa kwani kila kazi inachangamoto zake.kazi njema.
Asante sana Gewa na Karibu sana
Duuuuuh hivi sasa sitapata tabu tena…
Karibu sana Saady
napataje kweny mac
Kwani Tanzania Tech nimewapenda hata mlipoanza hii website yenu nilikuona kama masihara hivi mi kila hatua unayoenda nakufuatilia uko viziri ndugu.Safi sana!
KWanini website yako usiiweke watu watembelee bure kwenye app ya FreeBasics?
Nashukuru sana kaka, Tutafanyia kazi ushauri wako kaka.
Nimeipenda
Je unaweza ku-download vidmate kwenye laptop?