Ukweli ni kwamba teknolojia imekuwa sana kwa kipindi cha miaka 10 iliyopita hadi sasa, hapa nazungumzia kutokea mwaka 2009 hadi sasa mwaka 2019. Hi, karibu Tanzania Tech na kwa kuanza najua tayari umesha shirikia au pengine umesha fanikiwa kuona picha mbalimbali zikisambaa kwenye mitandao ya kijamii zikiwa na hashtag ya #10Yearschallenge.
Sasa baada ya kuona challenge hii kwa watu wengi, hatimaye Tanzania tech tumeamua kuangalia #10Yearschallenge ya mambo mbalimbali ya kiteknolojia. I Hope utaenda ku-enjoy pamoja na kujifunza jinsi teknolojia inavyozidi kukuwa kila siku.
TABLE OF CONTENTS
Mauzo ya Simu 2009 Vs 2019
Japo kuwa utaona kama ni juzi tu ila 2009 teknolojia ilikuwa bado inajikongoja, kipindi hicho kwenye upande wa mauzo ya Simu Nokia 5230 ndio ilikuwa simu inayoongoza kwa mauzo kwa kuwa na mauzo ya nakala zaidi ya milioni 159 kwa mwaka mzima.
Mwaka 2019 kutokea 2018 mauzo ya simu yamekuwa tofauti kidgo na sasa kwani kwa kipindi hicho kampuni ya Nokia haikuwa hata kwenye Top 3 ya mauzo ya simu kwa mwaka 2018 – 2019. Mwaka jana 2018 simu iliyokuwa inaongoza kwa mauzo ni Samsung Galaxy Note 9 kwa kuuza nakala zaidi ya milioni 30 kwa mwaka mzima tokea simu hiyo ilipo zinduliwa.
Simu ya Bei Ghali 2009 Vs 2019
Kwa kuwa teknolojia inaendelea kukuwa kila siku, hata mwaka 2009 ulikuwa ni mwaka wa kupiga hatua kwa kampuni mbalimbali za kiteknolojia. Mwaka huu ndipo kampuni ya Apple ilizindua simu mpya ya iPhone 3GS, Simu hii ilikuwa ni moja kati ya simu nzuri sana na pia ndio iliyochukua chati ya kuwa simu ya bei ghali kwa mwaka huo. Sasa hapa siongelei iPhone 3GS ya kawaida bali nazungumzia iPhone 3GS SUPREME ambayo ilikuwa imetengenezwa kwa Gold na Almasi.
Simu hii imetengenezwa kwa Pure Gold na kama unavyoweza kuona ilikuwa na mkanda wa almasi mbela, na nyuma logo ya Apple pia ilikuwa imetengenezwa kwa almasi na kwenye kitufe cha home kulikuwa na jiwe la almasi ambalo ni hadimu sana. Kwa ujumla simu hii ilikuwa na samani ya dollar za marekani milioni $3.15 sawa na takribani Tsh bilioni 7.26.
Mwaka 2018 kuja 2019, bado kuna simu nyingi ambazo ni za bei ghali lakini zote haziwezi kushindana na simu hii ya iPhone 4. Simu hii sio iPhone ya kawaida bali hii ni iPhone 4 Diamond Rose ambayo imetengenezwa kwa almasi hadimu sana na kufanya thamani ya simu hii kupanda na kufikia dollar za marekani milioni $8 ambayo ni sawa na takribani shilingi za Tanzania Tsh Bilioni 18.4.
Samsung Galaxy 2009 Vs 2019
Kama nilivyo sema mwaka 2009 ulikuwa ni mwaka wa kihistoria kwa makampuni mengi sana ya kiteknolojia, historia hiyo pia ipo kwa kampuni ya Samsung kwani mwaka 2009 kampuni hiyo ilitoa mfululizo wa kwanza wa simu za Samsung Galaxy. Simu hiyo ya kwanza ya Samsung Galaxy iliyopewa jina la Samsung GT-I7500 au Samsung Galaxy (original) ni moja ya simu ambazo pia zilikuwa na teknolojia ya kisasa na muundo mzuri kwa kipindi hicho.
Kwa mwaka huu 2019 Simu za samsung galaxy zimebadilika sana na karibia kila mwezi simu mpya za Samsung Galaxy zimekuwa zikitoka zikiwa na teknolojia ya kisasa kabisa. Kwa mwaka huu 2019 toleo jipya la Samsung Galaxy F ndio toleo la simu za Samsung Galaxy ambalo linategemewa kuwa toleo la kisasa na lenye muundo mzuri, huku ikifatiwa na Samsung Galaxy S10 ambayo pia inategemewa kuwa simu ya kisasa na yenye muonekano mzuri.
Gari la Mwaka 2009 Vs 2019
Tuzo za gari la mwaka au World Car Awards (WCOTY) zilianzishwa mwaka 2003 na ili kusudi gari liweze kushiriki linatakiwa liwe maarufu angalau kwenye nchi 5 au kwenye mabara mawili na iwe ni kabla ya january 1 kabla ya kuanza kwa tuzo hizo.
Mwaka 2009 gari lililo shilkilia chati ya gari la mwaka huo ilikuwa ni Volkswagen Golf Mk6, Gari hili kwa mwaka huu ni gari la kawaida sana yani ni sawa na kusema Vits wala sio IST.
Kwa mwaka 2018 kuelekea 2019 mambo ni tofauti sana tena ukizingatia kwa sasa kuna magari mengi sana yanayotumia umeme. Mwaka 2018 gari ambalo limeshikilia chati ya kuwa gari bora la mwaka ni Volvo XC60.
Kama unataka kujua zaidi kuhusu vigezo na masharti vilivyo tumika unaweza kusoma zaidi kuhusu tuzo hizi kupitia mtandao wa Wikipedia Hapa.
Apple 2009 Vs 2019
Kama umesoma makala nzima kuanzia mwanzo basi lazima utakuwa umeona mwaka 2009 ulikuwa na umuhimu gani kwa kampuni ya Apple. Ila kama ujasoma basi labda ni kwambie kuwa mwaka 2009 ni mwaka muhimu kwa Apple kwani kampuni hiyo ndipo ilipotoa simu mpya ya iPhone 3GS.
Fast Forward mwaka 2018 kuelekea 2019, Apple ni kampuni ya tofauti sana na mwaka 2018 kampuni hiyo imetangazwa kuwa kampuni yenye thamani ya Trilioni 1 za marekani. Lakini pamoja na hayo bado kampuni hii iko kwenye chati ya simu bora za mwaka 2018 kwa kuwa na simu zinazo tumiwa zaidi na watu wengi.
Nadhani mpaka hapo unaona jinsi gani teknolojia ilivyoweza kubadilika kwa kasi sana, mambo yapo mengi sana ambayo pengine tukiandika hapa tutachukua zaidi ya kurasa mbili na najua wengi wetu hatupendi kusoma maneno mengi.
Anyway kwa leo hii ndo #10Yearschallange ambayo tumeona kushiriki na nyie, mpaka siku nyingine guys endelea kupitia tovuti ya Tanzania Tech kila siku kifunza mambo mengi zaidi kuhusu teknolojia.
Habari ndugu!
Kuna simu moja nimeichukua China, simu aina ya Huawei Nova 3e, sasa nikitaka kujisajiri kwenye Huawei ID, inanionyesha imeshasajiriwa kwa namba za China.
Sasa nitawezaje kuisajiri kwa ID ya Tanzania nahitaji msaada wenu ndugu zangu
Wenu katika habari za Teknolojia
Ndg Erick Gulayi