Convert Mafaili ya Aina Zote kwa Pamoja (Windows)

Tumia njia hii ku-convert mafaili ya aina yoyote kwa urahisi na haraka
Convert Mafaili ya Aina Zote kwa Pamoja (Windows) Convert Mafaili ya Aina Zote kwa Pamoja (Windows)

Kama wewe ni mmoja wa watu wanaotumia kompyuta kwa muda mrefu basi ni wazi kuwa kuna wakati unahitaji kubadilisha format ya file moja kwenye file lingine bila kuinstall programu mpya.

Kupitia makala hii nitaenda kuonyesha njia rahisi ambayo unaweza kutumia ku-convert mafaili ya aina zote kwa urahisi na haraka bila ku-install programu nyingi. Kupitia njia hii utaweza ku-convert mafaili ya aina zote kama vile mafaili ya sauti ya aina zote, mafaili ya video ya aina zote, mafaili ya document za aina zote, mafaili ya picha na mafaili mengine mengi.

Convert Mafaili ya Aina Zote kwa Pamoja (Windows)

Advertisement

Kifupi ni kuwa utaweza kubadilisha format ya file la aina yoyote kwa urahisi sana kwa kubofya vitu viwili tu kwenye kompyuta yako. Basi bila kuendelea kupoteza muda twende kwenye hatua hizi.

Download Programu Hapa

Kwa kuanza hakikisha una download programu ya hapo chini, baada ya kudownload install vizuri kwenye kompyuta yako kisha baada ya hapo sasa endelea kwa kufuata maelezo mafupi hapo chini.

Baada ya kuinstall programu hiyo, moja kwa moja nenda kwenye file lolote unalotaka ku-convert kisha moja kwa moja right click kwenye file hilo na chagua File converter.

Convert Mafaili ya Aina Zote kwa Pamoja (Windows)

Baada ya hapo moja kwa moja chagua aina ya file unalotaka kisha moja kwa moja programu hii itaweza kuanza ku-convert kwa haraka.Huna haja ya kufanya kitu chochote zaidi ya hatua hizo.

Uzuri wa programu hiyo unaweza ku-convert file za aina zote kwa urahisi na haraka kwa kubofya vitu viwili tu kwenye kompyuta yako.

Convert Mafaili ya Aina Zote kwa Pamoja (Windows)

Programu hii ni bora pengine kuliko programu nyingine zote ambazo umewahi kutumia kuweza kuconvert mafaili kwenye kompyuta yako. Jaribu programu hii kisha niambie maoni yako kupitia sehemu ya maoni hapo chini.

Kama unaona njia hii ni ngumu kwako unaweza kusoma hapa kujua jinsi ya ku-convert video kwa urahisi kwa kutumia programu ya VLC. Kwa maujanja zaidi hakikisha unaendelea kutembelea Tanzania tech kila siku.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use