Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Jinsi ya Kuandika CV, Barua ya Kazi na Mifano ya CV (200+)

Andika CV bora na barua ya kuomba kazi kwa urahisi na haraka
Jinsi ya Kuandika CV, Barua ya Kazi na Mifano ya CV (200+) Jinsi ya Kuandika CV, Barua ya Kazi na Mifano ya CV (200+)

Ni wazi kuwa kadri muda unavyozidi kwenda ndivyo wanafunzi kutoka vyuo mbalimbali wanavyo maliza masomo na kuingia mtaani kwaajili ya kutafuta kazi. Lakini ni ukweli kuwa ni sehemu chache sana za kutoa elimu unapofundishwa jinsi ya kuandika CV bora kwa ajili ya kuomba kazi.

Kuliona hili kupitia makala hii nitakuonyesha njia rahisi ambayo unaweza kutumia kuandika CV bora kwa urahisi na haraka bila kuwa na ujuzi wowote. Kitu cha muhimu ni kuhakikisha unakuwa na kompyuta kwani ni wazi kuwa CV bora lazima inakuwa imeandaliwa kwa kutumia kompyuta.

Advertisement

Basi bila kuendelea kupoteza muda wako zaidi moja kwa moja twende kwenye somo hili la jinsi ya kuandika CV na barua ya kuomba kazi bila kuwa na ujuzi.

Jinsi ya Kuandika CV na Mifano ya CV

Kwa kuanza unatakiwa kupakua programu hapo chini kwa ajili ya kompyuta, baada ya kupakua programu hii, Unzip kisha Install programu hiyo kwenye kompyuta yako. Hakikisha unafuata maelekezo ndani ya file yaliyo andikwa soma hapa.

Download Programu Hapa

Baada ya Kumaliza Kuinstall, fungua programu hiyo na sasa upo tayari kuandika CV bora bila kuwa na ujuzi wowote.

Jinsi ya Kuandika CV, Barua ya Kazi na Mifano ya CV (200+)

Baada ya kufungua programu hii moja kwa moja bofya angalia sehemu ya Resumes, kisha bofya View Sample Resumes.

Jinsi ya Kuandika CV, Barua ya Kazi na Mifano ya CV (200+)

Baada ya hapo utaweza kuona mifano ya CV zaidi ya 200, unachotakiwa kufanya sasa ni kuchagua aina ya kazi uliyosomea au unayoomba kwa muda huo.

Jinsi ya Kuandika CV, Barua ya Kazi na Mifano ya CV (200+)

Ili kuchagua aina ya kazi uliyosomea kwaajili ya kupata mfano bora wa CV, moja kwa moja sehemu ya Select an Industry iliyopo juu upande wa kushoto.

mifano ya cv

Kama unavyoweza kuona, utaweza kuchagua aina ya kazi au professional yako, kisha upande wa kulia utaweza kuchagua aina ya kazi kulingana na ulichosomea.

Baada ya kuchagua moja kwa moja soma CV yenyewe kama inaendana na kazi unayomba, mara nyingi CV hizi zinakuwa na mambo yote ya muhimu ila unaweza kuongezea kama unaona haitoshi, kufanya hivyo bofya kitufe cha Personalize This Resume ambacho kipo chini upande wa kulia.

Jinsi Ya Kuandika CV

Baada ya kubofya hapo utapelekwa kwenye ukurasa ambapo sasa utaweza kuedit CV yako na kuongeza kila kitu unachotaka kuongeza, hakikisha unajaza kila kitu unachotaka ikiwa na jina lako kwa juu. (Kama ni mara yako ya kwanza kutumia programu hii basi itakuuliza jina lako kamili, sanduku la posta na mambo mengine ya msingi kabla ya kutumia hivyo ni muhimu kujaza).

Vitu hivyo ndivyo hutumika kwenye kila CV unayo edit na vitajiweka venyewe moja kwa moja pale unapo bofya sehemu ya Personalize This Resume. Pia unaweza kuedit baadae.

Jinsi Ya Kuandika CV, mifano ya cv

Baada ya kumaliza moja kwa moja bofya kitufe cha Word au PDF kilichopo juu upande wa kulia na moja kwa moja utaweza ku-save CV yako kwenye fomati uliyo chagua moja kwa moja.

mifano ya cv, Jinsi Ya Kuandika CV

Baada ya hapo moja kwa moja utaweza kupata CV yako tayari kwa kutuma maombi ya kazi kwa urahisi na haraka bila kupoteza muda mrefu. Kama unataka kuandika CV hii kwa kiswahili basi unaweza kutumia Google Translator kuweza kutafsiri CV hii kwa kiswahili.

Jinsi ya Kuandika Barua ya Kuomba Kazi

Kama unataka kuandika barua ya kuomba kazi, programu hii pia inakuapa nafasi ya kuandika barua kwa urahisi na haraka. Unachotakiwa kufanya ni kurudi mwanzo wa programu hii kisha chagua View Sample letters.

Jinsi Ya Kuandika CV

Kama ilivyokuwa awali moja kwa moja utapelekwa kwenye ukurasa ambao unatakiwa kuchagua aina ya barua unayotaka, kwenye kipengele hichi utachagua kati ya barua mbili, barua kabla ya usaili ya Interview na barua baada ya Interview.

Jinsi Ya Kuandika CV

Baada ya hapo chagua CV unayo itaji kisha copy na paste kuweza kuedit kulingana na mahitaji yako, hakikisha unajaza kila kitu au kila sehemu iliyo achwa wazi.

Kwa kufuata hatua hizo utaweza kutengeneza CV ikiwa pamoja na kuandika barua ya kuomba kazi kwa urahisi kwa kutumia njia hii. Kama kuna mahali umekwama unaweza kuuliza kupitia sehemu ya maoni hapo chini.

Kama unataka kujifunza zaidi unaweza kusoma hapa jinsi ya kutengeneza business card na kadi za mwaliko bure bila kuwa na ujuzi wowote. Kama unataka kuendelea kujifunza zaidi hakikisha una tembelea Tanzania tech kila siku.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use