Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Jinsi ya Kuwezesha Dira ya Kisasa (Compass) Kwenye Simu

Njia bora ya kuwezesha dira au compass kupitia simu yako ya Android
Jinsi ya Kuwezesha Dira ya Kisasa (Compass) Kwenye Simu Jinsi ya Kuwezesha Dira ya Kisasa (Compass) Kwenye Simu

Ni wazi kuwa simu za smartphone zimefanya mabadiliko makubwa sana, mabadiliko haya yamechangia sana kwenye maendeleo ya duniani kwa kuwa teknolojia imerahisha sana mambo.

Pamoja na mambo mengi ambayo yamewezeshwa na teknolojia ya smartphone, pia kupitia smartphone yako unaweza kutumia dira au compass ya kisasa yenye uwezo mkubwa sana.

Advertisement

Kama wewe ni mtumiaji wa dira ni wazi kuwa ulishawahi kujaribu app mbalimbali kwenye simu yako, lakini kupitia makala hii nitakuonyesha njia bora kuliko zote za kuwezesha dira kwenye smartphone yako. Baadhi ya sehemu zinazoweza kupatikana kwenye njia hii ni pamoja na –

Utaweza kuwasha dira au compass ambayo inaweza kuonyesha ulipo na wapi uende bila kutumia Internet, pia utaweza kutumia kamera ya simu yako kuweza kuona sehemu halisi unapoenda moja kwa moja kupitia kwenye kamera ya simu yako. Pamoja na mengine mengi sana.

Jinsi ya Kuwezesha Dira ya Kisasa (Compass) Kwenye Simu

Kwa mujibu wa watumiaji wa dira hii kutoka nje ya nchi, dira hii ina lavel za kijeshi yani ni sawa na dira inayotumiwa na wanajeshi mbalimbali. Sina uhakika sana na hili ila unaweza kujaribu ili kujua kama dira hii ina uwezo unaosemwa.

Kwa kuanza download app kupitia link hapo chini, baada ya kudownload install app kwenye simu yako kisha fungua app hii.

Download App Hapa

Ndani ya app utaweza kupata aina tatu za dira, kuna dira yenye kuonyesha muelekeo, dira ya ramani na dira ya kwenye kamera.

Utaweza kuwasha dira zote kwa kutumia vitufe vilivyoko chini ya app hii kama inavyoweza kuonekana kwenye picha hapo chini.

Jinsi ya Kuwezesha Dira ya Kisasa (Compass) Kwenye Simu

Kwa kufanya hivyo utakuwa umewezesha dira hii ya kisasa kwa urahisi kupitia simu yako ya Android. Kwa maoni yangu hii ni dira bora sana kati ya app zote za dira ambazo nimewahi kujaribu.

Kama unataka kujua zaidi unaweza kusoma hapa kujua jinsi ya kutumia ramani (Map) kwenye simu yako ya Android bila kutumia Internet. Kama unataka kuendelea kujifunza zaidi endelea kutembelea Tanzania tech kila siku.

4 comments
  1. inaonekana ni nzuri lakini link unazo weka sema na kweli kwaupande wangu mimi hua hazifunguki kabisa.

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use