Toleo jipya la WhatsApp limetoka hivi karibuni na moja kati ya sehemu mpya ambayo imeboreshwa ni sehemu ya Wallpaper ambayo sasa utaweza kuweka Wallpaper tofauti kwenye kila chat ndani ya programu hiyo.
Mbali ya kuweka Wallpaper tofauti kwenye kila chat ambayo hii inaweza kusaidia sana kujua ni nani unamtumia meseji kwa urahisi. Pia WhatsApp imeleta aina mpya ya Wallpaper ambazo unaweza kutumia kwenye simu yako.
Wallpaper hizo zime gawanyika kwa vipengele viwili yaani dark pamoja na bright. Wallpaper za bright hizi unaweza kuweka wakati wa mchana au wakati unahitaji mwanga zaidi kwenye simu yako, na wallpaper za dark unaweza kuweka wakati wa usiku wakati macho yako hayaitaji mwanga zaidi.
Mbali na hayo, pia ukiwasha sehemu ya dark mode kwenye simu yako moja kwa moja na sehemu ya chat itaweza kubadilika na kuwa na mwanga mweusi.
Maboresho mengine ambayo yameletwa kwenye toleo hili jipya la WhatsApp ni pamoja na uwezo mpya wa kutafuta sticker, ambapo sasa utaweza kutafuta sticker kupitia sehemu ya kusearch na moja kwa moja sticker inayo husiana na neno ulilo andika itatokea moja kwa moja kama ilivyo GIF.
Kwa sasa kama bado hujapata uwezo wa kubadilisha wallpaper kwenye kila chat, hakikisha unasasisha (update) toleo jipya la WhatsApp kupitia Play Store au App Store. Kama bado hujapata sehemu hiyo basi endelea kusubiri utapata sehemu hii ndani ya siku chache zijazo, hakikisha una update programu yako ya WhatsApp.
Kama unataka kujua jinsi ya kubadilisha wallpaper kwenye sehemu ya kuchat maarufu kama Instagram DM, basi soma hapa kujua hatua zote jinsi ya kufanya hivyo.