Habari mpya siku za karibuni zinasema kuwa, kampuni ya Facebook kupitia app yake ya WhatsApp hivi karibuni inategemea kulazimisha watumiaji kukubali vigezo na masharti ya utumiaji wa programu hiyo kwenye sheria zake mpya.
Sheria hizo ambazo zinatarajiwa kuanza kutumika rasmi tarehe 8 mwezi wa pili mwaka 2021, zinadai kuwa mtumiaji yoyote ambaye hata kubali vigezo na masharti ya utumiaji wa programu hiyo, basi ataweza kupoteza akaunti yake moja kwa moja.
Sehemu hiyo mpya ya sheria itakuwa inalazimisha watumiaji wote kubofya kitufe cha “I agree” na kupitia njia hiyo ndipo mtumiaji ataweza kuendelea kutumia app hiyo bila tatizo.
Mbali na hayo, kwa mujibu wa tovuti ya Wabetainfo, mabadiliko mengine ambayo yanatarajiwa kuja pamoja na sehemu hiyo ni pamoja na sehemu mpya ambayo itakuwa inatoa taarifa kuhusu programu hiyo ikiwa pamoja na mabadiliko mengine ya sheria mbalimbali yanayoendelea kwenye programu hiyo.
Sehemu hiyo itakuwa inakuja kama sehemu ya maandishi ambayo yatatokea kila mara programu hiyo inapo kuwa na mabadiliko mapya ambayo yanayo hitajika kufahamika kwa watumiaji. Sehemu hiyo itakuwa kama inavyoonekana kwenye screenshot hapo juu, (picha upande wa kushoto).
Kwa sasa mabadiliko yaliyopo kwenye programu ya WhatsApp ni pamoja na njia mpya ya kuweka wallpaper kwenye chat tofauti, ikiwa pamoja na njia mpya ya kutafuta sticker kwa kutumia sehemu ya kusearch kama inavyo kuwa wakati unatafuta emoji.
kwani hapo awali ulikua unauwezo wa kukataa vigezo na masharti? do!
Hapana hii ni sehemu mpya ambapo watumiaji wote wanatakiwa kukubali vigezo vipya hata wale ambao ni watumiaji tayari.