Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Mambo Muhimu Kujua Kabla ya Kununua TV Nzuri

Kama unataka kununua TV Bora na Nzuri fuata hatua hizi muhimu sana
Kununua TV Kununua TV

Ukweli ni kwamba kila mtu anahitaji kitu ambacho ni bora na chenye kudumu, katika swala zima la kununua TV pia ni muhimu sana kuwa na TV ambayo ni bora na ya kisasa na yenye kukidhi haja yako na ya familia yako kwa ujumla.

Katika kuhakikisha hilo kuna mambo ambayo ni muhimu kuzingatia kabla huja amua kununua TV ya aina yoyote, yafuatayo ni mambo hayo.

Advertisement

Ukubwa wa Kioo

Mambo Muhimu Kujua Kabla ya Kununua TV Nzuri

Ukubwa wa kioo ni moja kati ya vitu ambavyo watu wengi huzingatia, hiki ni kipengele muhimu lakini kwenye hili watu wengi hudhani kuwa ukubwa wa kioo ndio unao sababisha TV iwe inaonyesha vizuri, lakini hapa ningependa nikwambie kuwa kuna njia tofauti za kukuwezesha kujua ukubwa gani unahitaji kutokana na matumizi au mahitaji yako.

Kwa mujibu wa THX kama unataka kununua TV ni vyema kujua umbali unaotakiwa kukaa ili kuweza kuangalia TV hiyo vizuri, kwa mfano kama unataka kununua TV ya inchi 32 unatakiwa kukaa takribani futi 4 (nne) kutoka Tv ilipo mpaka unapo kaa kuangalia TV hiyo.

TV zingine unaweza kuangalia hapo chini kujua umbali unaotakiwa kukaa kutokana na ukubwa wa kioo.

Pia kama unataka kufanya mwenyewe unaweza kuingia kwenye tovuti hapo chini kisha chagua ukubwa wa TV kwa kusogeza mshale maalumu.

Tumia Kikokotozi cha TV

Kuweka TV Ukutani

Mambo Muhimu Kujua Kabla ya Kununua TV Nzuri

Watu wengi upenda kufunga TV zao ukutani, hii ni kwa wote wale wenyenazo na hata kwa wale ambao wanategemea kununua TV hizo, lakini hata kwenye hili pia kuna jambo la kuongeza kwani ni muhimu sana kukumbuka kuwa TV yako itakuwa ukutani hivyo itakuwa sambamba na ukuta wako hii inamaanisha kuwa ili kuona vizuri lazima TV yako iwe kubwa kidogo na izingatie vipimo maalumu ambavyo huitwa kwa kitaalamu VESA.

Najua unataka kujua zaidi kuhusu VESA kwa ufupi kabisa VESA ni vipimo maalumu vinavyotumika kupima umbali wa matundu ya kufunga TV au Monitor yako ukutani, vipimo hivyo ndio hutumika kupata stendi (bracket) maalum ya kufunga ukutani TV yako, unataka kujua zaidi angalia video hapo juu.

Teknolojia ya TV

Mambo Muhimu Kujua Kabla ya Kununua TV Nzuri

Linapokuja swala zima la kununua TV jambo lingine la muhimu la kuzingatia ni teknolojia ya TV hapa kuna mambo mawili ya kuzingatia, kuna teknolojia za aina mbili kwenye TV yaani LCD na OLED. Katika kufanya uchaguzi mzuri ni vyema kujua kidogo kuhusu teknolojia hizi.

LCD/LED TV

LCD/LED hizi ni TV ambazo zinatengenezwa na teknolojia inayo julikana kwa kitaalamu kama Liquid Crystal Display, Hizi TV hutumia mwanga kutoka nje ili kuweza kuonyesha picha halisi uzuri wa TV zenye teknolojia hii mara nyingi huwa za bei nafuu na hudumu kwa muda mrefu.

Tatizo la teknolojia hii kwenye TV ni kwamba mara nyingi ni ngumu kurekebisha kiasi cha mwanga kwenye picha inayo onekana hii inatokana na TV hiyo kutumia mwanga kutoka nje. (Tutakueleze zaidi kwenye makala nyingine)

OLED TV

OLED TV hizi ni TV ambazo zinakuja na teknolojia ya organic phosphorus, teknolojia hii inawezesha TV hizi kuweza kutengenezea mwanga waka yenyewe hivyo TV hizi mara nyingi huwa na picha nzuri sana kutokana na uwezo wa kuto kutegemea mwanga kutoka nje tofauti na ilivyo LCD.

Hivyo ni muhimu sana kuwa makini unapo tafuta TV kuangalia teknolojia bora kwa matumizi yako, pia TV hizi pia huwa na matatizo mbalimbali matatizo hayo ni kama vile, kuna wakati TV hizi zinakuwa hazina mwanga wa kutosha hivyo kufanya TV hizo kuwa na picha nzuri lakini nyeusi.

Pia swala la bei kwenye TV hizi ni tatizo kwani huwa zinauzwa kwa bei ghali sana ukilinganisha na TV zenye teknolojia ya LCD, vilevile tafiti zinaonyesha kuwa TV hizi za OLED katika ubora huwa haziwezi kuwa na uwezo wa kudumu sana nadhani hii inachangiwa sana na aina ya TV pia.

Viunganishi vya TV

Mambo Muhimu Kujua Kabla ya Kununua TV Nzuri

Katika kipengele hichi ni muhimu kuwa makini kwani kwenye miaka ya sasa viunganishi vya TV vimekuwa ni kitu cha msingi sana kuzingatia kwa mfano, kama unataka kununua TV ni vyema kuangalia kama TV hiyo inatumia Flash au USB na vitu vingine kama VGA, HDMI na viunganishi vingine kama AV Kingamuzi cha ndani na vingine ambavyo hutumika sana kwa sasa.

TV bora ni ile inayofanya kila kitu unachotaka kwa hiyo kama unatumia flash sana hakikisha TV yako inakuwa na sehemu za flash mbili au hata tatu pia kingamuzi au kisimbusi cha ndani ni muhimu kwa kila TV ya sasa kwani utakuwa huna haja ya kununua kisimbusi cha pembeni kwaajili ya kuangalia channel za ndani, hivyo ni muhimu uliza kabla ya kununua.

Resolution ya TV

Mambo Muhimu Kujua Kabla ya Kununua TV Nzuri

Resolution pia ni kitu cha msingi sana cha kuzingati kwenye swala zima la kununua TV, Resolution zipo za aina mbili kwa sasa kuna Ultra HD (ambayo inajulikana kama 4K) pamoja na HD. TV zenye Ultra HD ni TV ambazo huwa na pixel 3840X2160, wakati TV zenye resolution ya HD huwa na 1920×1080 pixel, hivyo hii inaonyesha Ultra HD ni bora kwa sababu inazidi resolution ya HD kwa mara nne zaidi hivyo mara nyingi TV zenye resolution ya Ultra HD huwa na uwezo wa konyesha picha angavu na nzuri zaidi ya TV zenye resolution za HD.

Ubora wa Speaker za TV

Mambo Muhimu Kujua Kabla ya Kununua TV Nzuri

Kuangalia speaker ni kitu cha msingi hasa kama umepanga kutumia TV yako bila kutumia speaker za nje yaani subwoofer, TV nyingi huja na teknolojia mbalimbali za sauti hivyo ni muhimu kuangalia lebo ambazo zinaonyesha aina ya teknolojia za sauti ambazo zipo kwenye TV unayotaka kununua. Kwa mfano kuna TV inakuja na DTS au Dolby Digital Surround zingine pia huja na teknolojia za SRS au Sound Retrieval System ambazo hutoa sauti bora kwenye mazingira tofauti.

Brand ya TV

Mambo Muhimu Kujua Kabla ya Kununua TV Nzuri

Brand ya TV au aina ya TV ni kitu kizuri cha kuzingatia kwa sasa kuna aina nyingi sana za TV hivyo ni vyema sana kuangalia aina ya TV unayotaka kununua kwani kwa kufuata uchaguzi sahihi utaepuka kununua TV feki ambayo pengine isinge weza kudumu kama ambavyo ungenunua brand tofauti, (kumbuka TV feki hazija fungiwa hapa Tanzania hivyo kuwa makini na fanya uchunguzi kabla ya kununua).

Muundo wa TV

Mambo Muhimu Kujua Kabla ya Kununua TV Nzuri

Kitu cha mwisho cha kuzingatia ni muundo wa TV yako, hapa kuna aina nyingi za TV kama vile Curved na Flat TV hizi ni muhimu kuangalia kutokana na aina ya nyumba au chumba chako unachoweka TV hiyo. Mara nyingi TV zenye muundo wa Curved zinapendeza zikikaa kwenye vyumba vikubwa na maranyingi zinafaa zaidi kuwekwa kwenye Meza na sio ukutani. Kwa kuzingatia haya ni vyema kuchagua TV ambayo itaendana na mahali pamoja na ukubwa wa nyumba au chumba chako.

Na hayo ndio baadhi tu ya mambo ambayo ni muhimu sana kuzingatia pale unapotaka kununua TV, Kama unataka kujifunza zaidi endelea kutembelea Tanzania Tech kila siku kwani kwa sasa tuna andaa makala nyingine zinazo endelea kukuelimisha zaidi kuhusihana na teknolojia ya TV na mengine kwa ujumla.

Kwa habari zaidi hakikisha upitwi kwa kudownload App yetu ya Tanzania tech kupitia Play Store na kama unataka kujifunza teknolojia kwa njia ya Video unaweza kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech kwenye mtandao wa Youtube.

12 comments
  1. Nimependa sana Blog yenu kwa kweli ni mfano wa kuigwa kuanzia muundo mpka mambo mnayoweka humu kweli nimeipenda sana.

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use