in

App Bora Unayohitaji kwa Ajili ya Watoto (Katuni za Watoto)

Kupitia njia hii utaweza kupata katuni nzuri za watoto za kuelimisha na kuburudisha

App Bora Unayohitaji kwa Ajili ya Watoto (Katuni za Watoto)

Kama wewe ni mzazi basi lazima umeshakutana na matatizo ya mtoto kumaliza bando kwenye simu yako kwa kuangalia katuni kupitia mtandao wa YouTube au YouTube Kids

Kuliona hilo leo hapa Tanzania tech nimekuletea app moja tu ambayo na uhakika inaweza kusaidia sana kutunza bando lako ikiwa pamoja na kufurahisha watoto wako hasa kipindi hichi cha likizo ambacho najua lazima utakuwa unasumbuliwa sana na simu yako kwenye mambo ya game au katuni.

Install Android App
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot

Tofauti na mtandao wa YouTube ambao unatumia sana bando na unayo matangazo mengi, au app ya YouTube Kids ambayo nayo pia inatumia bando kwa kiasi kikubwa sana. App hii itakusaidia kuweza kupata katuni maarufu za watoto na utaweza kuzipakua na kuhifadhi ndani ya app hiyo na mwanao ataweza kuangalia bila simu yako kuwa na data au Internet.

Basi bila kupoteza muda twende moja kwa moja niku onyeshe jinsi ya kutumia app hii kwenye simu yako ikiwa pamoja na kupata video bora za katuni kwa ajili ya watoto wako. Bure kabisa bila kulipia.

Kwa kuanza download app hapo chini kisha moja kwa moja endelea kwenye hatua zinazofuata hapo chini.

Download App Hapa

Baada ya kudownload na kuinstall app hii kwenye simu, moja kwa moja fungua app hii kisha bofya kitufe cha Play kilichopo katikati.

App Bora Unayohitaji kwa Ajili ya Watoto (Katuni za Watoto)

Baada ya hapo moja kwa moja utaplekwa kwenye ukurasa maalum ambapo unatakiwa kuweka pattern, hii ni muhimu kwaajili ya kuzuia mtoto kufungua programu hii bila ruhusa yako. Moja kwa moja chora pattern na kisha rudia kwa mara ya pili kuweza kuhakiki.

App Bora Unayohitaji kwa Ajili ya Watoto (Katuni za Watoto)

Baada ya hapo moja kwa moja endelea kwenye screen ambayo utaona video za katuni mbalimbali mchanganyiko, unaweza kuangalia mija kwa moja ambapo utatumia data au unaweza kudownload video hizo na zitabaki kwenye app hiyo na utaweza kuangalia bila data.

App Bora Unayohitaji kwa Ajili ya Watoto (Katuni za Watoto)

Kama unataka ku-download video kwa pamoja, moja kwa moja bofya vitu vitatu kwenye kona ya kulia ya kila video kisha moja kwa moja bofya view offline.

App Bora Unayohitaji kwa Ajili ya Watoto (Katuni za Watoto)

Baada ya hapo moja kwa moja utaweza kuona video hizo zimeanza kupakuliwa kuja kwenye simu yako, subiri mpaka duara linalo tokea kwenye kioo cha simu yako liweze kujaa kwa asilimia 100.

App Bora Unayohitaji kwa Ajili ya Watoto (Katuni za Watoto)

Pia unaweza kudowload video moja kwa moja ukiwa unaangalia ndani ya app hii, unaweza kufanya hivyo kwa kubofya alama ya download iliyopo ndani ya video.

App Bora Unayohitaji kwa Ajili ya Watoto (Katuni za Watoto)

Baada ya hapo sasa unaweza kuangalia video bila kutumia bando na utaweza kuongeza video kila mpya kwa kudownload na kuhifadhi kwenye sehemu ya Offline.

App Bora Unayohitaji kwa Ajili ya Watoto (Katuni za Watoto)

Kwa kufanya hivyo moja kwa moja utaweza kudownload katuni mbalimbali ambazo zina mafunzo kwa watoto. Pia kizuri kuhusu app hii pia inakupa uwezo wa kuset muda gani mtoto aweze kuangalia na mara baada ya muda huo kuisha basi app hii itajizima na kujifunza, unaweza kupata sehemu hiyo kupitia Settings.

Kama mwanao anayo simu yake basi unaweza kutumia njia hii kuweza kujua kila kitu ambacho mwanao anafanya kwenye simu yake. Kujifunza zaidi hakikisha unaendelea kutembelea Tanzania tech kila siku.

App Bora Unayohitaji kwa Ajili ya Watoto (Katuni za Watoto)
Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Hizi Hapa Browser Bora Zenye Mfumo wa Akili Bandia (AI)

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.