in

Sehemu ya Group Chat Kupitia App ya Tanzania Tech

Sasa utaweza kuchat na watalamu wa teknolojia kupitia Tanzania Tech

App mpya ya tanzania tech

Kama wewe ni mtumiaji wa app ya Tanzania Tech basi makala hii ni kwa ajili yako, na kama bado huja pakua app ya Tanzania Tech basi jaribu sasa app hii ili uweze kupata taarifa na mafunzo mbalimbali ya teknolojia kwa ukaribu zaidi na kwa haraka.

Kwa wale ambao tayari wanayo app ya Tanzania Tech na wanatumia toleo la zamani basi unaweza kupakua sasa toleo jipya ili kupata maboresho mapya pamoja na sehemu mpya ya “Group Chat”.

Kupitia sehemu hii utaweza kuchat kwenye magroup ya wazi na utaweza kupata msaada mbalimbali kwa watu wenye ujuzi wa teknolojia ikiwa pamoja na msaada kutoka kwetu moja kwa moja.

Pia sehemu hii ya group chat siku za mbeleni itakuwa na mambo mengi sana ikiwa pamoja na kipengele cha sunday movie ambacho sasa kitakuwa kwenye group pekee, pia siri nyingi pamoja na njia za kutengeneza pesa mtandaoni zitakuwepo moja kwa moja kwenye group.

Na mambo mengine mengi yanayo tarajiwa kuja baada ya muda mfupi.

Fahamu Anaepiga Simu na Kutuma SMS (Truecaller Pro)

Kitu cha muhimu jisajili kwa kuchagua sehemu ya Group chat iliyopo juu upande wa kulia mara baada ya ku-update app.

Sehemu ya Group Chat Kupitia App ya Tanzania Tech

Baada ya kubofya hapo moja kwa moja utapelekwa kwenye ukurasa wa kulogin, kwa kuwa hii itakuwa mara yako ya kwanza kutumia sehemu hii basi bofya sehemu ya create kutengeneza akaunti kwenye sehemu ya kuchat.

Sehemu ya Group Chat Kupitia App ya Tanzania Tech

Baada ya hapo andika data zako ambazo umetumia kwenye akaunti ya Tanzania tech au kama unatumia akaunti nyingine unaweza kuweka data zako kwenye sehemu hii. Hii itafanya akaunti yako ya Tanzania tech na akaunti ya kuchat kuweza kuunganishwa kwa pamoja.

Sehemu ya Group Chat Kupitia App ya Tanzania Tech

Baada ya hapo, bofya Register na moja kwa moja data zako zitaunganishwa na hutakuwa na haja ya kufanya tena jambo lolote. Moja kwa moja utaingia kwenye group chat ya Tanzania tech.

Sehemu ya Group Chat Kupitia App ya Tanzania Tech

Baada ya hapo sasa unaweza kujiungana group la majaribio, sehemu hii ipo kwaajili ya kuangalia matatizo ya sehemu hii mpya hivyo unaweza kujiunga ili wote kwa pamoja tuweze kufanya majaribio. Magroup mengine yatakuja siku za karibuni.

Apps za Kuangalia TV kwenye Simu ya Android (Hazipo Play Store)

Baadhi ya sehemu ambazo ni muhimu kufahamu ni sehemu ya Menu ya upande wa kushoto juu, hapo utaweza kupata sehemu ya kuedit profile yako, Kuangalia watu waliopo kwenye blocklist, pamoja na sehemu ya dark mode, bila kusahau sehemu ya standby ambayo hii husaidia kuonekana kama up offline kwa muda.

Sehemu ya Group Chat Kupitia App ya Tanzania Tech

Sehemu nyingine tutaendelea kuzifahamu kadri muda unavyozidi kwenye hivyo hakikisha unajiunga nasi leo na moja kwa moja tuweze kufanya majaribio ya sehemu hii kwa pamoja. Kama unayo app ya Tanzania tech hakiksha una bofya sehemu ya update kwenye soko la Play Store, kama huna app ya Tanzania tech basi unaweza kudownload sasa ili kujaribu sehemu hiyo na nyingine nyingi.

Download App Hapa

Kama umependa app ya Tanzania Tech unaweza kutupa nyota tano kupitia soko la Play Store, pia kama unataka kujua app zetu nyingine unaweza kuangalia app zetu nyingine hapa, au soma zaidi kuhusu app zetu hapa.

Amani Joseph

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Maoni 4

Toa Maoni Hapa

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.