Habari mpya hivi karibuni zinasema, huwenda kampuni ya Samsung ikasitisha kutoa simu mpya za Samsung Galaxy Note mwaka 2021 kutokana na janga la corona.
Kwa mujibu wa tovuti ya reuters, inasemekana kuwa kampuni hiyo itawekeza rasilimali zake kwenye simu za Galaxy S21 na simu zinazo jikunja za Galaxy fold. Tetesi kutoka tovuti ya reuters zinasema kuwa, hatua hiyo imefikiwa na Samsung baada ya kushuka kwa mahitaji ya simu hizo hasa kipindi hiki cha janga la corona.
Mbali na hayo, tetesi hizo pia zinasema kampuni ya Samsung inatarajia kuweka kalamu maalum ambayo hupatikana kwenye simu za Galaxy Note (S-pen) kwenye simu mpya ya Galaxy S21 Ultra ambayo inatarajiwa kuzinduliwa mapema mwezi January mwaka 2021.
Mpaka sasa bado hakuna taarifa kamili kutoka kwa kampuni ya Samsung yenyewe, hivyo pengine tuendelee kusubiri na tutakuletea taarifa kamili pale habari hii itakapo thibitishwa na Samsung.