in

Sponsored : CRDB Yaendelea Kuibuka Kinara Tuzo za Mabenki

Makala hii imedhaminiwa na CRDB Bank PLC

Sponsored : CRDB Yaendelea Kuibuka Kinara Tuzo za Mabenki

Benki ya CRDB imeibuka na tuzo ya benki ya ndani ya nchi inayopendwa zaidi (Most Preferred Domestic Bank of the Year) katika tuzo za Tanzania Consumer Choice Awards 2020 zilizofanyika mwishoni wa wiki iliyopita.

Tuzo hiyo inakuja ikiwa ni siku chache tangu Benki ya CRDB ilipoibuka kinara katika tuzo zinazotolewa na Bodi ya Taifa ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu (NBAA) kama taasisi ya fedha iliyoongoza kwa kuwasilisha Taarifa ya Fedha bora kwa mwaka 2018/2019 kwa kuzingatia viwango vya kimataifa.

Install Android App
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
Sponsored : CRDB Yaendelea Kuibuka Kinara Tuzo za Mabenki
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela, akikabidhiwa tuzo ya benki ya ndani ya nchi inayopendwa zaidi katika hafla fupi ya tuzo za Tanzania Consumer Choice Awards 2020 zilizofanyika mwishoni wa wiki iliyopita.

Tuzo za Tanzania Consumer Choice Awards ni tuzo zinazotolewa kila mwaka zikilenga kutambua ubora wa biashara mbalimbali kutokana na kura zinazopigwa na wateja wake.

Akipokea tuzo hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abudlmajid Nsekela amewashukuru wateja na Watanzania kwa ujumla kwa kuichagua Benki ya CRDB kama benki yenye asili ya ndani ya nchi inayopendwa zaidi (Most Preferred Domestic Bank of the Year).

“Ushindi huu ni ishara tosha kuwa wateja wetu na Watanzania kwa ujumla wana imani kubwa na  Benki yao ya CRDB na hivyo hii kwetu sisi ni deni ambalo tunapaswa kuwalipa kwa imani hii kubwa waliyotupa. Ahadi yetu ni kuendelea kutoa huduma bora zinazoendana na mahitaji ya wateja ambayo yamekua yakibadilika kila uchao” alisema Nsekela.

Kwa upande wake Mgeni Rasmi katika tuzo hizo, Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Silaoneka Kigahe ameitaka sekta binafsi kuwa mstari wa mbele katika kusukuma mbele gurudumu la uchumi wa nchi kwa kuwa sasa hivi wameshaelewa maono na mtazamo wa Serikali ya Awamu ya Tano katika masuala ya uchumi.

Sponsored : CRDB Yaendelea Kuibuka Kinara Tuzo za Mabenki
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela, akiwa na Mkurugenzi Mkuu wa benki ya Standard Chartered Tanzania, Sanjay Rughani katika hafla fupi ya tuzo za Tanzania Consumer Choice Awards 2020 zilizofanyika mwishoni wa wiki iliyopita.

“Wito wangu kwa wafanya biashara ni kuhakikisha wanazalisha bidhaa na huduma ambazo zitakidhi mahitaji ya soko la ndani lakini pia kuweza kushindana katika masoko ya nje na naamini uwezo huo tuko nao na sisi kama serikali tutaendelea kutengeneza mazingira mazuri kwa ajili ya wafanyabiashara? Alisema Naibu Waziri Kigahe.

Sponsored : CRDB Yaendelea Kuibuka Kinara Tuzo za Mabenki
Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Infinix na Teknolojia Mpya Ya Mobile Gaming Kupitia Dimensity 9300

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.