Kwanza napenda kuchukua nafasi hii kuwatakiwa heri ya Christmas kwenu nyote, hakika Mwenyezi Mungu ametupendelea wote na leo tupo pamoja tukisherekea Christmas nyingine. Ni wazi kuwa tuna wajibu wa kumshukuru Mungu na kuendelea kuomba kila siku.
Kwa kuwa najua siku ya leo wengi wenu mtakuwa nyumbani, basi nimeona niwaletee makala hii fupi ambapo utaweza kujua apps nzuri ambazo unaweza kutumia ku-stream movie bure bila kulipia. Kupitia apps hizi pia utaweza ku-download movie hizi na kuangalia bila Internet ndani ya apps hizo.
Basi bila kuendelea kupoteza muda zaidi moja kwa moja twende tukangalia apps hizi, kumbuka apps hizi nyingi hazipo kwenye soko la Play Store hivyo kama unataka kupakua app yoyote unaweza kufanya hivyo kwa kubofya kitufe chini ya maelezo ya apps husika.
VIU Premium
Kama wewe ni mpenzi wa movie na tamthilia mbalimbali za kutoka india, Nigeria, Kenya, Korea, Ghana, Pakistani na nchi nyingine basi app hii itakufaa sana. App hii inakuja na filamu nyingi pamoja na tamthilia ambazo unaweza kuangalia ndani ya app hii moja kwa moja au kwa kudownload moja kwa moja kupitia kwenye app hiyo, app hii pia inakuja na movie za Kiswahili.
ZiniTevi
ZiniTevi ni app nyingine nzuri ambayo unaweza kutumia ku-stream movie kupitia simu, smartTV kupitia Laptop na hata vifaa vingine vya kidigital. App hii ni moja kati ya app nzuri sana ya kugundua movie mpya na inakuja na njia bora sana ya kutambua movie mpya na ku-stream bure bila kulipia. Pia unaweza kudownload na kuangalia movie hizo ndani ya app hii.
Tubi Pro
Tubi pro ni app nyingine ambayo itakusaidia ku-stream movie kwa urahisi kupitia simu yako, app hii nayo inakuja na mchanganyiko wa filamu pamoja na tamthilia ambazo unaweza kuangalia au ku-stream moja kwa moja kwenye simu yako ya Android. Unaweza kuangalia movie bila kulipia.
HD Movies
App ya mwisho kwenye list hii ni HD Movies app hii itakupa uwezo wa kuangalia movies zote kwa urahisi na kupitia simu yako ya Android. App hii haina tofauti sana na app nyingine kwenye list hii kwani nayo utaweza ku-stream movie ikiwa pamoja na kuhifadhi movie hizo ndani ya app hii na utaweza kuangalia bila kutumia internet.
Na hizo ndio app ambazo unaweza kutumia ku-stream movie moja kwa moja kwenye simu yako siku ya leo, kama utakuwa unataka apps zaidi unaweza kusoma hapa kujua apps nyingine za kudownload movie kwa urahisi kupitia simu yako hapa.
Hadi siku nyingine napenda tena kukutakia heri ya Christmas na uwe na ijumaa njema na mapumziko mema.! Hadi siku nyingine endelea kutembelea Tanzania tech.