Vodacom na Infinix Wazindua Simu Mpya ya Infinix NOTE 8

“Ofa ya GB 96 katika kila simu ya Infinix NOTE 8 kwa muda wa mwaka mzima”
Vodacom na Infinix Wazindua Simu Mpya ya Infinix NOTE 8 Vodacom na Infinix Wazindua Simu Mpya ya Infinix NOTE 8

Kampuni ya simu za mkononi inayoongoza kidijitali nchini, Vodacom Tanzania PLC, kwa kushirikiana na Infinix leo imetambulisha rasmi simu mpya aina ya Infinix NOTE 8. Simu hii mpya itaambatana na ofa ya GB 96 za internet kutoka Vodacom Tanzania PLC kwa Mwaka mzima.

Simu ya Infinix NOTE 8 ni ya kwanza toka kampuni hiyo, kuundwa ikiwa na processor ya MediaTek Helio G80 Octa Core, ambayo imetengezwa mahususi kuhakikisha inafanya kazi muda mrefu na kwa uwezo madhubuti, na hii ni kuifanya kuwa simu yenye uwezo mkubwa kuliko matoleo mengine ya mwanzo toka Infinix.

Vodacom Tanzania PLC wanashirikiana kuifikisha Infinix NOTE 8 kwa Watanzania ili kuhakikisha kila mtanzania anaingia katika ulimwengu wa kidijitali kwa kumiliki simu bora na kupitia mtandao wenye kasi ili kufurahia maendeleo ya teknolojia duniani.

Advertisement

Vodacom na Infinix Wazindua Simu Mpya ya Infinix NOTE 8

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi, Afisa wa Uhusiano wa Infinix, Aisha Karupa alisema, “MediaTek Helio G80 processor na Teknolojia ya MediaTek HyperEngine Game imeipelekea NOTE 8 kuwa na uwezo wa kuhimili application zenye ujazo mkubwa pasipo simu kupata moto au kuzimika ghafla wakati wa matumizi.”

Karupa alisisitiza, “pamoja kuwa na processor kubwa yenye kukufaidisha wewe mpenzi wa games, kazi nyingi za kiofisi na za shuleni lakini pia Infinix NOTE 8 ina sifa nyingine pendwa kama vile, kamera mbili za mbele zenye MP 16 na kamera 6 nyuma zenye MP 64, chaji yenye kujaza battery ya ujazo wa 5200mAh, kioo cha inch 6.95 na memory ya GB 128 ROM kwa GB 6 RAM”.

Vodacom na Infinix Wazindua Simu Mpya ya Infinix NOTE 8

Kwa upande wake, Mkuu wa Kitengo cha Masoko wa Vodacom Tanzania PLC Nandi Mwiyombella, alisema kwamba nia ya kampuni ya Vodacom ni kuipeleka Tanzania katika ulimwengu wa kidijitali, ili kulitimiza hili hawana budi kuhakikisha wateja wanapata huduma za Intaneti bila kikwazo chochote.

“Umuhimu wa mtandao wenye kasi kwa kila mtumiaji wa smartphone unajulikana, na ili watanzania tusiwe nyuma ya ukuaji wa teknolojia tunahitaji mtandao wenye kasi ili kujifunza mambo mapya kila leo na kwa kulizingatia hilo Vodacom Tanzania PLC inakusogeza karibu na ulimwengu wa kidijital kupitia ofa ya GB 96 katika kila simu ya Infinix NOTE 8 kwa muda wa mwaka mzima,” alisema Nandi.

Vodacom na Infinix Wazindua Simu Mpya ya Infinix NOTE 8

Infinix na Vodacom Tanzania Plc wamekuwa washirika kwa muda mrefu tangu kuzinduliwa rasmi kwa bidhaa za Infinix nchini.   Kampuni hizi mbili zimekuwa zikishirikiana kuleta mapinduzi katika sekta ya mawasiliano nchini, Simu hii ya Infinix Note 8 inapatikana katika maduka yote ya Vodacom nay ale ya Infinix yaliyopo maeneo yote nchini.

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use