Jinsi ya Kutuma Meseji Zinazojifuta Zenyewe WhatsApp

Meseji zote unazochat na mtu zitaweza kujifuta zenyewe ndani ya muda wa siku saba
Jinsi ya Kutuma Meseji Zinazojifuta Zenyewe WhatsApp Jinsi ya Kutuma Meseji Zinazojifuta Zenyewe WhatsApp

Hivi karibuni app ya WhatsApp imeongezewa sehemu mpya mbalimbali na moja kati ya sehemu hizo ni pamoja na sehemu ambayo inakuwezesha kutuma meseji ambazo zinaweza kujifuta zenyewe baada ya muda maalum.

Tofauti na sehemu ya kufuta meseji ya “delete for everyone” ambayo mtumiaji anaweza kufuta meseji mwenyewe, sehemu hii mpya yenyewe ufuta meseji yenyewe bila wewe kufanya kitu chochote kile.

Kumbuka, kitu cha muhimu ni kuwa, meseji ambazo utakuwa umetuma kabla ya kuwasha sehemu hii hazitaweza kujifuta. Pia sehemu hii inafanya kazi kwa chat zote za mtu binafsi na pia chat za group. Basi baada ya kusema hayo moja kwa moja twende kwenye hatua hizi.

Advertisement

Hatua ya kwanza hakikisha unaingia kwenye soko la Play Store au App Store kisha moja kwa moja hakikisha app yako ipo updated.

Jinsi ya Kutuma Meseji Zinazojifuta Zenyewe WhatsApp

Baada ya hapo fungua app yako ya WhatsApp na moja kwa moja bofya profile ya mtu ambae unataka kuchat nae na meseji utakazo mtumia zijifute. Bofya profile picha yake kwenye chat zako.

Jinsi ya Kutuma Meseji Zinazojifuta Zenyewe WhatsApp

Baada ya hapo kwenye uwanja wake wa profile, moja kwa moja shuka chini kidogo mpaka utakapo ona sehemu ya ‘Disappearing Messages’.

Jinsi ya Kutuma Meseji Zinazojifuta Zenyewe WhatsApp

Baada ya hapo bofya sehemu hiyo na kisha chagua sehemu ya On ambayo itatokea kwenye ukurasa unafuata mara baada ya kubofya sehemu hiyo.

Jinsi ya Kutuma Meseji Zinazojifuta Zenyewe WhatsApp

Baada ya hapo basi meseji zote ambazo utakuwa unatumiana na mtu huyo zitajifuta zenyewe ndani ya muda wa siku saba. Kama unataka kuendelea kubaki na meseji unazo tumiana na mtu huyo basi moja kwa moja fuata hatua hizi kisha chagua sehemu ya Off kwenye hatua hii ya mwisho.

Jinsi ya Kutuma Meseji Zinazojifuta Zenyewe WhatsApp

Hadi hapo utakuwa umeweza kutuma meseji zinazo jifuta zenyewe kwa muda wa siku saba, kama unataka kujifunza maujanja zaidi unaweza kusoma hapa jinsi ya kubadilisha voice meseji kutoka kwenye sauti kuwa kwenye maandishi. Kwa muajanja zaidi hakikisha unaendelea kutembelea Tanzania tech kila siku.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use