Kama wewe ni mmoja wa watu ambao ni wapenzi wa kucheza game kwenye simu basi makala hii ni kwa ajili yako. Kupitia makala hii nitakuonyesha hatua kwa hatua jinsi ya kucheza game za Android kupitia kompyuta yako ya Windows.
Kabla ya kuanza ni vyema uhakikishe kuwa unayo kompyuta yenye mfumo wa Windows, napendekeza zaidi toleo la Windows 10. Pia hakikisha unayo Internet kwenye kompyuta yako au simu yako. Kama unayo mahitaji yote hayo basi moja kwa moja twende kwenye makala hii.
Kwa kuanza bofya link hapo chini kisha pakua programu ya Nox kwenye kompyuta yako. Kama ulikuwa hujui kuhusu Nox, hii ni programu ambayo inakusaidia kutumia Android kwenye kompyuta yako.
Mbali ya kuweza kucheza game za Android kwenye kompyuta, pia utaweza kupakua Android apps moja kwa moja kwenye kompyuta yako kupitia soko la Play Store.
Kifupi ni kwamba kwa kutumia programu hii utaweza kuwa na Android kwenye kompyuta yako, na moja kwa moja utaweza kutumia programu kama Instagram, WhatsApp, Facebook na programu nyingine kama hizo za mfumo wa Android.
Moja kwa moja unachotakiwa kufanya ni kuingia kwenye tovuti hapo chini kwa kutumia kompyuta yako bofya kitufe cha Download kisha pakua Noxplayer kwenye kompyuta yako.
Baada ya hapo, install programu hiyo kwa kufuata maelezo ya programu hiyo na moja kwa moja utaweza kuanza kucheza game za Android moja kwa moja kwa kupitia kompyuta yako yenye mfumo wa Windows.
Kwa kufuata hatua hizo utaweza kuche game yoyote ya mfumo wa Android kwenye kompyuta yako kwa kutumia Nox Player, kama unataka kujifunza zaidi unaweza kusoma hapa jinsi ya kuinstall mfumo wa Windows kwenye simu yako ya Android.