Kama wewe ni mwanafunzi Apps zifuatazo zinaweza kutatua matatizo mbalimbali kwa haraka na kwa ubora zaidi kulingana na sababu ambazo nitakuwa nazitaja kwenye kila app, mbali ya hayo app hizi zinaweza kutumiwa na mtu yoyote ambaye anaona app hizi zina manufaa kwake.
Pia kwa kuwa app hizi ni kwa ajili ya wanafunzi nyingi hazina matangazo na unaweza kutumia bila kulipia na kwa ukamilifu wa asilimia 100. Basi baada ya kusema hayo bila kuendelea kupoteza muda wako twende moja kwa moja kwenye app hizi.
TABLE OF CONTENTS
Photo Translator Pro
Kwanza baada ya kufanya tathimini nimegundua kuwa wanafunzi wengi wa hasa wa mwaka wa kwanza kupata changamoto ya lugha na hivyo kushinda kufanya vizuri kwa kushindwa kujua vizuri kilicho andikwa kwenye vitini mbalimbali.
Kuliona hili nimekuletea app ya Photo Translator Pro, app hii inakupa uwezo wa kutafsiri maneno yote kwenye karatasi yako na kuyaweka kwenye lugha rahisi ya Kiswahili.
Unachotakiwa kufanya ni kupakua app hii kisha chagua sehemu ya lugha na chagua swahili na moja kwa moja nyooshea kamera ya simu yako kwenye karatasi yenye maandishi ya lugha ya kiingereza na bofya kitufe cha kupiga na moja kwa moja juu ya kioo chako utaweza kuona tafsiri ya maneno hayo kwa Kiswahili.
Oxford Advanced Learners Dictionary 10th edition
Kama wewe ni mwanafunzi kamili basi lazima unahitaji kuwa na Dictionary, haijalishi wewe ni mwaka wa kwanza, au mwaka wa tatu Dictionary ni muhimu sana.
Kuliona hili pia nimekuletea app ya Oxford Advanced Learners Dictionary 10th edition, app hii inakuja na toleo zima la dictionary Oxford Advanced learners ambayo ni toleo la 10. Toleo hili litakupata tafsiri ya maneno yote magumu kwenye masomo yako ikiwa pamoja na maneno yale ambayo hutumiwa zaidi kwenye masomo mbalimbali ya kisayansi na hata lugha.
CamScanner PDF Creator
CamScanner PDF Creator ni moja ya app ambayo ni muhimu sana kwa wanafunzi wa aina zote, app hii inaweza kupunguzia gharama kubwa za kutoa copy kila ambazo kila mwanafunzi wa chuo lazima amepitia.
App hii ni tofauti na ambayo umezoea kupakua kupitia Play Store kwani hii imeondolewa matangazo na itakuruhusu kutumia bila kuwa na alama ya CamScanner ambayo huwa kwenye document ambazo una scan. Mbali ya hayo utaweza kucopy maandishi yaliyopo kwenye karatasi na kuyaweka kwenye soft copy, pamoja na mambo mengine mengi sana.
Kama wewe ni mwanafunzi na ungependa kupunguza gharama za kutoa copy kila mara basi nakushauri sana kupakua programu hii ya CamScanner PDF Creator.
Symbolab Pro
Kama wewe ni mmoja wa watu ambao hesabu inasumbua kidogo basi app hii itakusaidia sana, app hii ni moja kati ya app maarufu sana ambayo inaweza kusaidia kufundisha hesebu ngumu kwa kukupa kanuni muhimu ikiwa na njia mbalimbali za kufanya hesabu hizo.
App hii inaweza kukusaidia kufanya hesabu mbalimbali ikiwa pamoja na
- Equation Calculator
- Integral Calculator
- Derivative Calculator
- Limit calculator
- Inequality Calculator
- Trigonometry Calculator
- Matrix Calculator
- Functions Calculator
- Series Calculator
- ODE Calculator
- Laplace Transform Calculator
- Na nyingine nyingi..
Toleo hili halina matangazo na unaweza kufanya hesabu mbalimbali kwa urahisi kwa kutumia simu yako ya Android au Tablet.
WPS Office Premium
Kama wewe ni mmoja wa watu ambao unataka kubadilisha maandishi kweye pdf au kwenye word basi hakikisha una pakuwa programu hii. Programu hii inafanya kazi kama microsoft word na zaidi. Programu hii inakusaidia kuedit PDF na file zote zinazotokana na microsoft.
Programu hii ni rahisi kutumia na inakuja bila matangazo na unaweza kutumia kwa muda wowote ule unao hitaji. Unaweza kupakua app hii kupitia link hapo chini.
Na hizo ndio app ambazo unaweza kutumia wewe kama mwanafunzi wa mwaka wa kwanza, najua app hizi ni app za kawaida sana lakini ukizitumia kwa usahihi app hizi zinaweza kusaidia sana kwenye maisha yako ya chuo.
Kama unataka kujua zaidi, unaweza kusoma hapa kujua laptop nzuri ambazo unaweza kutumia wewe mwanafunzi au kama wewe ni mfanyakazi wa ofisini.