Ni wazi kuwa teknolojia inakuwa kwa kasi sana, pamoja na kuwa tayari teknolojia inarahisha mambo lakini bado yapo mambo ambayo ni muhimu kufahamu ili kuweza kurahisha matumizi ya simu yako hasa kama wewe ni mpenzi wa teknolojia hasa kipengele hichi cha maujanja.
Kuliona hilo leo nuletea njia mpya kabisa ya kuweza kuwasha baadhi ya programu ikiwa pamoja na kufanya mambo mbalimbali ndani ya simu yako kwa kutumia app inayoitwa TapTap. App hii kama ilivyo jina lake inawezesha kufanya vitu hivyo kwa kupiga piga kwa kidole simu yako kwenye upande wa nyuma ya simu yako.
Yaani kwa kupiga piga mara mbili nyuma ya simu yako unaweza kufanya mambo mbalimbali kama vile kuwasha kioo cha simu yako, kuwasha tochi kwenye simu yako, kuchuka screenshot na mambo mengine mengi. Kifupi ni kuwa app hii inakupa njia rahisi ya kutumia simu yako kwa urahis na haraka. Unaweza kuangalia inavyofanya kazi hapo chini.
Kwa kuanza unaweza kupakua programu ya TapTap kupitia link inapatikana hapo chini, app hii haipo kwenye soko la Play Store hivyo ni vizuri kuinstall app hii kupitia link hapo chini. Hakikisha unapakua toleo jipya la app hii kwenye simu yako, toleo la TapTap-0.8.1-Beta.apk ndio toleo jipya zaidi kwa sasa, kama kwa namna yoyote app hiyo haitofanya kazi kwenye simu yako basi unaweza kupakua matoleo mengine.
Unaweza kupata matoleo mengine ya nyuma kupitia link hapa, baada ya kumaliza kuinstall app hii kwenye simu yako sasa moja kwa moja unaweza kufuata video hapo juu. Video hiyo ipo kwa lugha ya kihindi lakini unaweza kufuatisha anachokifanya moja kwa moja na utaweza kuwasha app hii kwenye simu yako.
Kwa sababu app hii ina uwezo wa kufanya vitu vingi nimeshindwa kuelekeza vyote kupitia hapa, kama wewe utakuwa unataka kujua jinsi ya kufanya jambo fulani basi unaweza kuuliza kupitia sehemu ya maoni na moja kwa moja nitakuelekeza kupitia hapo au nitaongeza maelezo kupitia makala hii.
Kama unataka kujifunza zaidi hakikisha unaendelea kutembelea Tanzania Tech kila siku kwani hivi karibuni tunakuletea maujanja mengi zaidi kupitia channel yetu ya YouTube hapa. Kama unataka kujifunza maujanja zaidi, unaweza kusoma hapa kujua jinsi ya kubadilisha video yoyote kuwa video ya katuni.
jee naweza tumia namba ya usa