Kampuni ya Samsung Yazindua Simu Mpya ya Galaxy F41

Simu hii inakuja ikiwa na battery kubwa ya 6000 mAh
Kampuni ya Samsung Yazindua Simu Mpya ya Galaxy F41 Kampuni ya Samsung Yazindua Simu Mpya ya Galaxy F41

Kampuni ya Samsung hivi leo imetangaza ujio wa Series mpya ya simu za Galaxy F, simu ambazo zinasemekana kuwa bora zaidi upande wa battery na kamera. Kupitia series hiyo, leo Samsung imetambulisha Galaxy F41 simu ambayo inakuja na sifa zinazo fanana na simu nyingi kutoka samsung.

Tukianza na kioo, Galaxy F41 inakuja na kioo cha inch 6.4 kilicho tengenezwa kwa teknolojia ya Super AMOLED, mbali na hayo kioo hicho kinakuja na uwezo wa kuonyesha video zenye resolution ya hadi pixel 1080 kwa 2340.

Advertisement

Kwa mbele, Galaxy F41 inakuja na kamera ya Megapixel 32 huku ikiwa na uwezo wa kuchukua video za 1080p@30fps. Mbali na hayo, simu hii inakuja na teknolojia ya HDR kwenye kamera yake hiyo ya mbele.

Kwa nyuma, Galaxy F41 inakuja na kamera tatu kamera kuu ikiwa na Megapixel 64 na kamera nyingine mbili zikiwa na Megapixel 8 na nyingine ikiwa na Megapixel 5. Kamera zote kwa pamoja zinakuja na uwezo wa kuchukua video zenye resolution ya hadi 4K@30fps.

Kampuni ya Samsung Yazindua Simu Mpya ya Galaxy F41

Kwa upande wa sifa za ndani, Galaxy F41 inaendeshwa na processor ya Exynos 9611 (10nm), yenye speed ya CPU ya Octa-core (4×2.3 GHz Cortex-A73 & 4×1.7 GHz Cortex-A53). Processor hiyo inasaidiwa na RAM ya GB 6 pamoja na uhifadhi wa ndani au ROM ya hadi GB 64 au GB 128. Unaweza kuongeza uhifadhi huo kwa kutumia memory card ya hadi GB 256.

Kwa upande mwingine, Galaxy F41 inakuja na uwezo wa Radio FM yenye uwezo wa kurekodi, pamoja na sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama headphone jack. Mbali na hayo simu hii pia inakuja na ulinzi wa fingerprint ambayo inapatikana nyuma ya simu hii. Simu hii inaparikana kwa rangi tatu tofauti ambazo ni Fusion Black, Fusion Blue, na Fusion Green.

Kampuni ya Samsung Yazindua Simu Mpya ya Galaxy F41

Kwa upande wa Battery, Galaxy F41 inakuja na battery kubwa yenye uwezo wa hadi 6000 mAh, battery ambayo inaweza kudumu na chaji kwa siku nzima kulingana na matumizi yako. Simu hii pia inakuja na teknolojia ya Fast Charging yenye uwezo wa hadi 15W.

Samsung Galaxy F41 imetengenezwa nchini India na inategemewa kupatikana kwanza nchini humo kuanzia octoba 16 kupitia soko la mtandaoni la Flipkart.

Bei ya Samsung Galaxy F41 Tanzania

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use