Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

ZTE Axon 20 5G : Simu ya Kwanza Yenye Kamera Chini ya Kioo

ZTE Axon 20 5G ni ya kwanza kabisa yenye teknolojia hii kufanikiwa kuingia sokoni
ZTE Axon 20 5G : Simu ya Kwanza Yenye Kamera Chini ya Kioo ZTE Axon 20 5G : Simu ya Kwanza Yenye Kamera Chini ya Kioo

Mara nyingi hapa Tanzania Tech huwa hatuongelei sana kuhusu simu za ZTE, hii ni kutokana na kuwa uwezekano wa simu hizo kufika hapa Tanzania ni mdogo sana hivyo hakuna sababu ya kuelezea kuhusu bidhaa ambayo wengi wetu hatuta fanikiwa kuiona kwa namna moja ama nyingine.

Lakini leo pengine hii imekuwa tofauti kutokana na kuwa, hivi karibuni kampuni ya ZTE imeweza kuja na teknolojia mpya ambayo pengine unaweza kuiona kwenye simu mbalimbali ndani ya miaka ijayo.

Advertisement

ZTE Axon 20 5G ni simu ya kwanza kabisa kutoka ZTE yenye kamera ya mbele au selfie ambayo inapatikana chini ya kioo. Tofauti na simu nyingine, kamera ya mbele ya ZTE Axon 20 5G inakuja ikiwa haionekani kabisa na hivyo kufanya simu hiyo kuwa na kioo kikubwa kisicho na kamera ya mbele.

Japokuwa ZTE Axon 20 5G sio simu ya kwanza kujaribu teknolojia hii, lakini simu hii ndio simu ya kwanza ambayo imetangazwa kuingia sokoni hivi karibuni hivyo inafanya simu hii kuwa ndio ya kwanza kabisa ambayo itakuwa inapatikana kwa wateja mbalimbali.

ZTE Axon 20 5G : Simu ya Kwanza Yenye Kamera Chini ya Kioo

Japokuwa swala hili linaonekana ni rahisi lakini ukweli ni kwamba ni gumu sana tena ukizingatia ni lazima lensi ya kamera ipate mwanga ndipo picha ziweze kutokea zikiwa angavu na zenye muonekano mzuri.

Kampuni ya ZTE imeonekana kutatua tatizo hilo kwa kutumia teknolojia mpya ya ambayo inafanya kioo hicho kuwa na uwezo wa kuwa na uwazi bila kuonekana kwa macho ya kawaida. Hii imefanya kioo hicho kuweza kupitisha mwanga hasa sehemu ambayo kamera hiyo inapatikana.

ZTE Axon 20 5G : Simu ya Kwanza Yenye Kamera Chini ya Kioo

Mbali na teknolojia hiyo, kampuni ya ZTE imetengeneza kamera hiyo ikiwa na uwezo wa kurekebisha yenyewe kiasi cha mwanga inacho hitaji ili kuweza kuchukua picha zenye muonekano mzuri. Kamera hiyo pia imerekebishwa pixel na kufanya pixel hizo kwendana na kioo bila kufanya kioo hicho kuingilia muonekano wa picha zinazopigwa na kamera hiyo.

Sifa za ZTE Axon 20 5G

Kwa upande wa sifa za simu hii, simu hii inakuja na kioo cha inch 6.92 kilicho tengenezwa kwa teknolojia ya OLED. Chini ya kioo hicho kunayo kamera ya mbele ya Megapixel 32 yenye uwezo wa kuchukua video za hadi 1080p@30fps.

ZTE Axon 20 5G : Simu ya Kwanza Yenye Kamera Chini ya Kioo

Kwa nyuma simu hii inakuja na kamera nne, kamera kuu ikiwa na Megapixel 64, na nyingine zikiwa na Megapixel 8 na nyingine mbili za mwisho zikiwa na Megapixel 2 kila moja. Kamera hizo zote kwa pamoja zinakuja na uwezo wa kuchukua video za hadi 4K@30/60fps.

Kwa upande wa sifa za ndani, ZTE Axon 20 5G inakuja na ikiwa inaendeshwa na processor ya Snapdragon 765G ambayo inasaidiwa na CPU yenye uwezo wa hadi Octa-core (1×2.4 GHz Kryo 475 Prime & 1×2.2 GHz Kryo 475 Gold & 6×1.8 GHz Kryo 475 Silver). Mbali na hayo uwezo wa simu hii unawezeshwa na RAM ya GB 6 au GB 8 pamoja na uhifadhi wa ROM ya hadi GB 128 au GB 256.

Kwa upande wa battery simu hii inapewa nguvu na battery ya Li-Ion yenye uwezo wa 4220 mAh. Simu hii pia inakuja na teknolojia ya Fast charging yenye uwezo wa 30W, ambayo inaweza kujaza chaji kwenye battery ya simu hiyo hadi asilimia 60% ndani ya dakika 30.

Simu hii inatumia mfumo wa Android 10, mfumo ambao juu yake kuna mfumo wa ZTE ambao unajulikana kama ZTE’s Mifavor 10.5.

Bei ya ZTE Axon 20 5G

Kuhusu upatikanaji simu hii inategemewa kupatikana nchini China kuanzia mwezi huu September tarehe 10. Bei ya simu hizi inategemewa kuanzia TZS 750,000 kwa toleo lenye GB 6 za RAM na ROM GB 128. Toleo lenye GB 8 za RAM na GB 128 za ROM linategemewa kuuzwa kwa TZS 850,000. Toleo la mwisho lenye GB 8 za RAM na GB 256 za ROM linategemewa kuuzwa kwa TZS 952,000, Kumbuka bei zote hizi ni bila kodi hivyo bei inaweza kuongezeka kwa hapa Tanzania.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use