Mwaka mmoja uliopita, kampuni ya Samsung ilitangaza kusitisha simu za Galaxy J, huu ukiwa ni mpango wa kuingiza sokoni matoleo mapya ya Galaxy A na Galaxy M ambayo yanatumiwa na watu wengi sana kwa sasa.
Hivi karibuni, kampuni ya Samsung inatarajia kuingiza sokoni toleo jipya kabisa la simu za Galaxy F Series, simu ambazo zinasemekana kuwa bora zaidi kwenye upande wa kamera.
Kwa mujibu wa tovuti mbalimbali, Simu mpya za Galaxy F Series zinategemewa kuwa ni simu za bei nafuu huku zikikadiriwa kuuzwa kwa bei ya makadirio kati ya TZS 1,000,000 hadi TZS 600,000.
Kwa sasa inasemekana simu ya kwanza ya Galaxy F Series, inategemewa kupatikana huko nchini India huku ikiwa na jina la Galaxy F41.
Kama unavyoweza kuona hapo juu, Galaxy F41 inategemewa kuja na processor ya Samsung Exynos 9611, RAM ya GB 6 pamoja na uwezo wa kioo hadi resolution ya pixel 1080 kwa 2340. Mbali na sifa hizo hapo juu sifa nyingine za simu hii bado hazijajulikana.
Simu hizi zinategemewa kuanza kuapatikana hapa Tanzania kuanzia mwezi wa kumi na mbili au mwezi wa 11 mwishoni mara baada ya simu hizo kuzinduliwa huko nchini India. Kwa sasa matoleo ya simu za Galaxy A ndio matoleo ya simu za bei nafuu zaidi kwenye simu za Samsung, huku Galaxy A10 ikiwa ndio inayo ongoza kununuliwa zaidi.
Kujua zaidi kuhusu simu hizi mpya za Samsung Galaxy F Series, hakikisha unaendelea kutembelea Tanzania Tech kila siku.