Baada ya kusubiriwa kwa muda, na baada ya kusikia tetesi mbalimbali hatimaye hivi leo kampuni ya LG imetangaza ujio wa simu yake mpya ya LG Wing 5G. Simu hii ni mwanzo mpya kutoka kampuni ya LG, huku ikiwa ni sehemu ya LG Explorer Project, mradi mpya ambao unategemea kuleta simu mpya za kisasa zitakazo badilisha muonekano wa kawaida wa simu kutoka LG.
Tukiachana na hayo, sasa tugeukie simu mpya ya LG Wing. Simu hii inakuja na vioo viwili, kioo kimoja cha juu kinakuja na urefu wa inch 6.8 kikiwa ni full screen na kioo cha chini au ndani kinakuja na urefu wa inch 3.9 huku kikiwa kipo nusu.
Kioo cha juu kimetengenezwa kwa teknolojia ya P-OLED huku kioo cha ndani au cha chini kikiwa kimetengezwa kwa teknolojia ya G-OLED.
Sehemu muhimu kwenye simu hii ni kioo, hii ni kutokana na uwezo wake wa kuzunguka na kuruhusu mtumiaji kuweza kutumia programu mbalimbali kwa haraka na urahisi bila kutoka kwenye app moja kwenda nyingine.
LG Wing 5G imelenga zaidi wapenzi wa kuangalia movie au kucheza game kwa urahisi ambapo utaweza kucheza game, au kuangalia movie huku ukiendelea kufanya mambo mbalimbali kwenye kioo cha ndani.
Mbali na hayo, LG pia imesema kuwa imetengeneza kioo hicho kikiwa imara huku pia kikiwa na uwezo wa kufunga na kufunguka mara nyingi zaidi bila kuharibika kwa urahisi. Mbali na hayo, simu hiyo pia inasemekana kuja na uwezo wa kuzuia maji na vumbi IP54 splash proof, Water-repellent coating na MIL-STD-810G.
Mbali na hayo sifa nyingine za LG Wing 5G ni pamoja na uwezo wa kamera ya mbele ambayo inaendeshwa na mota maalum yenye uwezo wa Megapixel 32, huku ikiwa na uwezo wa kuchukua video za hadi 1080p@30fps.
Kwa upande wa kamera za nyuma, LG Wing inakuja na kamera tatu huku kamera kuu ikiwa na Megapixel 64 na kamera nyingine mbili zikiwa na Megapixel 13 na Megapixel 12. Kamera hizo zote kwa ujumla zinakuja na uwezo wa kurekodi video za hadi 4K au 4K@30fps.
Kwa upande wa sifa za ndani LG Wing 5G inaendeshwa na processor ya Qualcomm SDM765 Snapdragon 765G (7 nm) ambayo inakuja na CPU ya hadi Octa-core (1×2.4 GHz Kryo 475 Prime & 1×2.2 GHz Kryo 475 Gold & 6×1.8 GHz Kryo 475 Silver). CPU hiyo inasaidiwa na RAM ya GB 8 pamoja na uhifadhi wa ndani wa hadi GB 128 au GB 256, uhifadhi huo unaweza kuongezwa kwa kutumia memory card ya MicroSD Card ya hadi GB 256.
Kwa upande wa battery LG wing 5G inakuja na battery ya 4000 mAh ambayo inakuja na teknolojia mbalimbali kama vile Wireless charing, pamoja na Fast Charing. Kwa upande wa bei bado hadi sasa haijajulikana bei halisi ya simu hii, lakini inakadiriwa kuwa kati ya TZS 3,500,000 hadi 4,000,000 pamoja na kodi.
Kama unataka kujua zaidi kuhusu sifa kamili za LG Wing 5G unaweza kusoma hapa, kujua bei kamili ya simu hii endelea kutembelea Tanzania Tech tutakujulisha hivi karibuni.