Jinsi ya Kutangaza Biashara (Sponsored) Kupitia Twitter

Hatua kwa hatua jinsi ya kufanya matangazo kupitia mtandao wa Twitter
Jinsi ya Kutangaza Biashara (Sponsored) Kupitia Twitter Jinsi ya Kutangaza Biashara (Sponsored) Kupitia Twitter

Ni ukweli usiopingika kuwa kwa sasa mitandao ya kijamii imekuwa ni sehemu kubwa ya kibiashara kutokana na kusaidia biashara nyingi kuweza kutafuta masoko kwa urahisi sana.

Lakini kuwa na akaunti pekee kwenye mitandao hiyo ya kijamii haitakusaidia kwa asilimia 100 kwani wote tunajua kuwa na akaunti sio kazi bali kazi ni kupost kwenye akaunti hiyo kila siku.

Advertisement

Zoezi hili ni gumu sana hasa kama wewe huja ajiri mtu wa kufanya kazi hiyo na unayo majukumu mengine ya kila siku.

Ndio maana kukawa na sehemu hii ya (Sponsored), sehemu hii itakusaidia kufanya matangazo kwenye akaunti mbalimbali za watumiaji wa mtandao wa Twiiter ambapo post zako zitaweza kutembelewa na watu wengi zaidi na hatimaye kusaidia biashara yako kupata wateja wengi zaidi.

Kuliona hilo leo, nimekuletea makala ambayo nitakuonyesha hatua kwa hatua jinsi ya kufanya matangazo, au (Sponsored) moja kwa moja kupitia akaunti yako ya Twitter.

Basi bila kuendelea kupoteza muda moja kwa moja twende kwenye makala hii.

Tengeneza Akaunti ya Matangazo

Kama hujawahi kutumia twitter ads, basi hatua ya kwanza ni kutengeneza akaunti yako ya matangazo, akaunti hii sio akaunti nyingine bali hii inakuwa ndani ya akaunti yako ya kawaida hivyo ni muhimu kuingia kwenye akaunti yako ya Twitter unayotaka kufanyia matangazo au Sponsored baada ya hapo ndipo anza kutengeneza akaunti yako ya matangazo.

Kutengeneza akaunti tembelea tovuti ya ads.twitter.com.

Jinsi ya Kutangaza Biashara (Sponsored) Kupitia Twitter

Baada ya hapo hakikisha unajaza data zako kama inavyo onekana hapo juu, Chagua nchi kisha chagua muda au Time zone ambayo kwa hapa Tanzania ni +03:00 ambayo unaweza kuchagua Nairobi au kama Dar es salaam ipo basi chagua hiyo. Baada ya hapo bofya Let’s go.

Chagua Campaign objective

Jinsi ya Kutangaza Biashara (Sponsored) Kupitia Twitter

Sehemu hii ni muhimu kwa kuwa ndio inayokupa nafasi ya kutangaza kwa kupata kile unachotaka, kupitia sehemu hii ni muhimu kuchagua kitu gani ambacho unataka kukipata unapofanya matangazo. Vipo vitu vya aina mbalimbali zifuatazo.

  • Reach – Hapa unataka watu wengi zaidi waweze kuona Tweet yako, hapa unatakiwa kulipia kila wakati tweet yako inapo angaliwa na watu 1000.
  • In-stream video views – Hapa unataka tangazo lako lionekane mwanzo kwenye video za live kutoka Twitter Premium Partners.Utalipia kila mara video yako u\napo onekana
  • Video views – Hapa unaaka kupata views kwenye video yako uliyo iweka kupitia mtandoa wa Twiiter kwenye akaunti yako. Utalipia kila view unayopata
  • App installs – Hapa ni pake kama unataka watu wapy waweza kuinstall app yako, hapa utalipia kwa kila install unayopata.
  • Website clicks or conversion – Hapa ni kama unataka watu waweza kutembelea website yako, hii ikiwa na akaunti zako nyingine za  mitandao ya kijamii. Hapa utalipia kila mara mtu atakapo tembelea tovuti yako au mitandao yako ya kijamii.
  • Engagements – Hapa ni kama unataka kuongeza wafuasi zaidi kwenye tweet zako ambazo tayari umesha promote.
  • Followers – Hapa ni kama unataka kuongeza wafuasi zaidi kwenye akaunti yako ya Twiiter. Hapo utalipia kila mara utakapo pata follower mpya kutokana na njia hii.
  • App re-engagements – Hapa ni kama unataka watu ambao wamesha pakua app yako waweza kuendelea kutumia app hiyo.

Tengeneza Campaign

Jinsi ya Kutangaza Biashara (Sponsored) Kupitia Twitter

Kupitia hapa tuaenda kuchagua kuongeza follower kwenye akaunti ya twitter ambapo hapa tutalipia kwa kila mfuasi mmoja utakae kuwa unampata kwa njia hii.

Baada ya kuchagua objective ya follower moja kwa moja utapelekwa kwenye ukurasa unao fuata ambapo unatakiwa kuandika jina la kampeni yako kisha endelea kwa kuchagua kiasi cha malipo unayotaka kulipia, unaweza kuchagua kiasi kidogo sana au kiasi kikubwa kulingana na uwezo wako.

Tengeneza Ad Group

Jinsi ya Kutangaza Biashara (Sponsored) Kupitia Twitter

 

Baada ya hapo sasa endelea kwa kutengeneza Ad Group, kwa kuwa unaanza kwa mara ya kwanza tengeneza ad group moja ambayo utakuwa unaweka matangazo yako yote, ila kadri unavyozidi kutumia mfumo huu wa Twitter ads unaweza kutengenanisha ad Group kulingana na aina ya objective unayotaka. Pia hakikisha sehemu ya Bid type ipo kwenye Automatic bid.

Chagua Mahali Target Audience

Jinsi ya Kutangaza Biashara (Sponsored) Kupitia Twitter

Kupitia hapa utaweza kuchagua watu wa aina gani waweze kuona zaidi tangazo lako, unaweza kuchagua kwa kuangalia jinsia, pia unaweza kuangalia mahali ambapo watu wanaishi na pia unaweza kuchagua kwa kuangalia watu wanatafuta nini zaidi au kutembelea kurasa gani zaidi kwenye mtandao wa Twitter.

Kwa mfano kama unataka watu wa teknolojia waone tweet yako au akaunti yako basi chagua Technology.

Chagua Mfumo wa Tangazo

Jinsi ya Kutangaza Biashara (Sponsored) Kupitia Twitter

Baada ya hapo sasa endelea kwa kuchagua mfumo wa Tangazo, unaweza kuchagua Tangazo lako lionekane kwa mtindo wa aina mbalimbali kama vile kupitia ukurasa za watumiaji mbalimbali wa Twitter au kupitia sehemu ya kutafuta au sehemu nyingine kama kwenye profile za watu mbalimbali. Baada ya hapo sasa unaweza kumalizia kwa kubofya Next.

Thibitisha

Baada ya hapo hakikisha kila kitu kipo sawa na moja kwa moja unaweza kuwasha campaign yako na utakuwa tayari unaweza kutangaza kupitia mtandao wa Twitter.

Hakikisha kila kitu kipo sawa na pia ni vizuri kuhakikisha njia za malipo zinafanya kazi kama kawaida na umeweka pesa kwenye akaunti zako.

Njia ya Haraka (Twitter Quick Promote)

Kama njia hapo juu unaiona ni ngumu kwako ningependa nikushauri kuwa jifunze hatua kwa hatua kwani itakupa matokeo bora zaidi kwenye biashara yako.

Lakini kama huna muda wa kujifunza unaweza kutumia njia mpya ya Twitter ya Twitter Quick Promote.

Jinsi ya Kutangaza Biashara (Sponsored) Kupitia Twitter

Chagua Tweet unayotaka kupromote kisha bofya kitufe cha vimishale vitatu upande wa kulia chini ya Tweet yako kisha moja kwa moja bofya sehemu ya promote na kisha chagua kiasi unachotaka kutumia na moja kwa moja lipia na anza kutangaza tweet yako.

Kumbuka njia hii ni bora zaidi kama unataka kutangaza tweet na sio app, wala website wala mitandao yako mingine ya kijamii.

Hadi hapo utakuwa umeweza kufanya matangazo kupitia Twitter, kama unataka kujua jinsi ya kufanya matangazo kupitia mtandao wa Instagram kwa kutumia M-Pesa Mastercard basi unaweza kuangalia video hapo chini au soma makala hii kupata hatua kwa hatua.

Kama unataka kujua njia nyingine za kufanya matangazo mbalimbali kama vile kupitia YouTube na Google Ads basi endelea kutembelea Tanzania Tech kwani tunakuletea video hizo na makala siku za karibuni. Kwa maujanja zaidi endelea kutembelea channel ya Tanzania Tech kuwa wa kwanza kujifunza teknolojia na kupata hatua hizi kwa njia ya video.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use