Habari mpya siku ya leo Jumatatu ya tarehe 7 mwezi wa tisa zinasema, Kampuni ya simu ya Infinix ipo mbioni kuzindua simu mpya ya Infinix ZERO 8 hapa Tanzania, simu hii inasadikika kwa mwaka huu wa 2020 ndio itakuwa kinara wa simu kutoka kampuni ya Infinix.
Kampuni ya simu ya Infinix imeonekana kujizolea sifa nyingi kutokana na uzalishaji wa simu zenye sifa tofauti tofauti. Mionekano ya simu za Infinix na uwezo mkubwa wa processors, RAM, battery na camera vimeifanya Kampuni ya simu ya Infinix kujizolea sifa katika soko la simu la kimataifa, na kuwa miongoni mwa kampuni yenye ushindani mkubwa.
Je unahisi Infinix ZERO 8 imebeba sifa gani zenye kupelekea simu hiyo kuwa kinara wa kampuni hiyo?
Kwa habari nyepesi nyepesi kupitia mtandao wa kijamii wa @infinixmobiletz, Infinix ZERO 8 ina megapixel 64 za kamera ya nyuma na megapixel 48 ya kamera ya selfie yenye resolution kubwa zaidi kuwepo kwenye simu hizo, kamera hiyo ni aina ya Sony IMX686 image sensor.
Kimuonekano inaonyesha dhahiri Infinix ZERO 8 ni kinara kweli wa kampuni hiyo kwa mwaka huu wa 2020, design ya muonekano wa mbele na nyuma ni tofauti kabisa na matoleo ya awali ya Infinix. Infinix ZERO 8 imetawaliwa na wigo mpana wa kioo na kamera zenye kujificha ndani yake, madhubuti kwaajili ya muonekano mzuri na kupata picha halisi katika ukubwa ule ule.
Hakuna taarifa zenye usahihi wa sifa za simu kutoka katika kampuni ya Infinix lakini kutokana na vionjo kupitia mtandao wao wa kijamii @infinixmobiletz ni dhahiri Infinix ZERO 8 ina CPU na GPU zenye speed ya kukimbizana na mobile games za 3D kwa ajili graphics, inawezekana ZERO 8 imefanya mabadiliko pia kwenye RAM, battery na mfumo wa kuingiza chaji.
Je ni zipi sifa nyengine za simu hiyo?