Njia Mpya ya Wajasiriamali Kukutana na Wateja Kwa Urahisi

Fikia wateja mbalimbali kwa urahisi kupitia Loko Find, Tangaza biashara kwa urahisi
Njia Mpya ya Wajasiriamali Kukutana na Wateja Kwa Urahisi Njia Mpya ya Wajasiriamali Kukutana na Wateja Kwa Urahisi

Ni kweli usio pingika kwamba kuna njia nyingi sana za kusaidia wajasiriamali wadogo kutangaza biashara, lakini kadri muda unavyozidi kwenda njia hizi zimekuwa zikipoteza umuhimu (kuisha muda wake) na kushindwa kutumiwa na wajasiriamali na wafanyabiashara wasasa.

Kuliona hili leo tunakuleta Loko Find, hii ni njia mpya kabisa ya kusaidia wajasiriamali kuweka biashara zao mbele ya wateja wengi zaidi kwa kutumia teknolojia. Njia hii haijalishi kama wewe ni mjasiriamali mdogo, mkubwa au hata wa kati, au unayo ofisi au huna kwani wote wanaweza kupata wateja kwa urahisi kupitia Loko Find.

Advertisement

Loko Find Inafanyaje Kazi

Kuweza kuelewa kwa urahisi unaweza kufikiria Loko Find kama sehemu ya kukutana na wanunuzi pamoja na wauzaji, lakini hii sio kama sehemu ya kuuza na kununua bali hii ni sehemu ambayo wateja watapata nafasi ya kufahamu biashara husika kwa undani zaidi kabla ya kufanya biashara.

Loko Find inafanya kazi kwa kuangalia zaidi eneo ulilopo hii inasaidi kusogeza huduma karibu zaidi na kupunguza gharama za usafirishaji wa bidhaa kutoka kwa mfanyabiashara kwenda kwa mteja. Kupitia Loko Find utaweza kujua aina zote za biashara zilizo karibu na wewe bila kujali eneo ambalo unapatikana kwa sasa. Sifa nyingine za Loko Find ni kama zifuatazo.

Njia Mpya ya Wajasiriamali Kukutana na Wateja Kwa Urahisi

Sifa za Loko Find

Kupitia Loko Find utaweza kufanya mambo mbalimbali kwa urahisi ikiwa pamoja na mambo yafuatayo.

  • Kupitia Loko Find utaweza kuona biashara zote zilizoko karibu na wewe na hivyo kupunguza gharama za usafirishaji.
  • Kupitia Loko Find wateja wataweza kutangaza tenda kwa wafanya biashara mbalimbali walipo bila kujali eneo.
  • Wateja wataweza kuona bei ya makadirio ya bidhaa kutoka kwa wajsiriamali mbalimbali.
  • Wateja wateweza kuona ofa mpya kutoka kwa wajasiriamali mbalimbali.
  • Wateja wataweza kuwasiliana na biashara au wajasiriamali wote kupitia namba ya biashara au kupitia mfumo wa ujumbe mfupi ndani ya app.
  • Pamoja na mambo mengine mengi.

Jinsi Unavyoweza Kutumia Loko Find

Kwa mfano kama unatafuta sehemu za huduma ya Sheria au wakili na upo sehemu ambayo huwenda uhifahamu vizuri basi unaweza kufungua Loko Find na kuona huduma zote za mawakili au wanasheria waliopo karibu na eneo unalo patikana kwa muda huo.

Hiyo haishii hapo, utaweza kuwasiliana na mtoa huduma husika kwa urahisi kwa kupiga simu au kwa kutuma ujumbe mfupi ndani ya Loko Find. Mbali ya hapo utaweza kuona ofa mbalimbali za huduma au biashara husika hivyo itakupa urahisi wa kuchagua biashara au huduma bora na bei nafuu zaidi, inayolingana na bajeti yako.

Lengo la Loko Find

Lengo la Loko find ni kusaidia wajasiriamali wadogo kujitangaza mbele ya wateja mbalimbali kwa urahisi na haraka. Pia Loko find inakusaidia kufanya biashara kwa urahisi na wateja kupata bidhaa mbalimbali kwa urahisi mahali popote kwa gharama nafuu.

Loko Find Business Kwa Wafanyabiashara

Loko Find inpatikana kwa wafanyabiashara na wateja na kama unataka kutoa huduma kwa wateja mbalimbali unaweza kujisajili kwa kupakua app ya Loko Find Business, wewe kama mfanyabiashara utaweza kufanya mambo mbalimbali kama vile.

  • Kupokea tenda kutoka kwa wateja mbalimbali
  • Kuwasiliana na wateja moja kwa moja ndani ya app
  • Utaweza kuweka ofa mbalimbali kwaajili ya wateja wako
  • Utaweza kuweka maelezo kuhusu biashara yako
  • Utaweza kuchagua aina ya biashara unayouza au huduma unayotoa
  • Na mambo mengine mengi

Download App ya Loko Find na Loko Find Business

Kwa sasa Loko Find inapatikana kwa watumiaji wa mfumo wa Android huku ikitegemewa kupatikana kwa watumiaji wa iOS siku za karibuni. Unaweza kupakua Loko Find hapa kama wewe ni mteja au kama wewe ni mfanyabiashara unaweza kupakua Loko Find Business Hapa.

Kwa ajili ya Wateja

Kwa ajili ya Wafanyabiashara

Kama unata msaada zaidi au kuna mahali ujaelewa jinsi ya kutumia app hii unaweza kuwasiliana nasi kupitia sehemu ya maoni hapo chini au unaweza kutembelea tovuti ya Loko Find Hapa.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use