Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Kampuni ya Apple Yazindua Toleo Jipya la iPad Air (2020)

iPad Mpya zinakuja na muundo ulio boreshwa na processor mpya ya A14 Bionic
Kampuni ya Apple Yazindua Toleo Jipya la iPad Air (2020) Kampuni ya Apple Yazindua Toleo Jipya la iPad Air (2020)

Kampuni ya Apple hapo jana ilifanya tamasha lake ambalo lilikuwa likisubiriwa na watu wengi kwa matarajio ya kuzinduliwa kwa simu mpya za iPhone 12, lakini badala yake kampuni hiyo ilifanya uzinduzi wa tablet yake mpya ya iPad Air (2020), pamoja na saa mpya za Apple Watch Series 6 na Watch SE.

Kwenye makala hii tuta angalia zaidi kuhusu iPad Air (2020) na kwenye makala inayofuata tuta angalia zaidi kuhusu Apple Watch Series 6 na Watch SE. Basi bila kupoteza muda twende moja kwa moja kwenye makala hii.

Advertisement

Muundo wa iPad Air (2020)

Tukianza na muundo wa iPad Air (2020), tablet hii inakuja na kioo cha inch 10.9 kilicho tengenezwa kwa teknolojia ya Liquid Retina IPS LCD. Kioo hichi kina uwezo wa kuonyesha rangi milioni 16 kupitia resolution yake ya pixels 1640 kwa 2360, mbali na hayo kioo hiccho kimetengezwa kikiwa na ulinzi wa Scratch-resistant glass, pamoja na teknolojia nyingine kama True-tone, Wide color gamut pamoja na 500 nits typ. brightness.

Kampuni ya Apple Yazindua Toleo Jipya la iPad Air (2020)

Ukingo kati ya kioo na kava la iPad Air (2020) sasa umepunguzwa na umekuwa mdogo zaidi huku ikiwa imebakizwa nafasi ya kamera ya mbele yenye uwezo wa Megapixel 7, kamera hii inaweza kuchukua video za hadi 1080p@30 na 60fps.

Kwa nyuma iPad Air (2020), inakuja na kamera moja ya Megapixel 12 yenye uwezo wa kuchukua video za hadi 4K@24/30/60fps, 1080p@30/60/120/240fps; gyro-EIS.

Kwa juu iPad Air (2020) inakuja na kitufe cha kuwasha ambacho pia kinatumika kama sehemu ya ulinzi ya fingerprint pale unapogusa sehemu hiyo. Kwa chini iPad hii inakuja na sehemu mpya ya USB Type-C 1.0 sehemu ambayo ni tofauti kabisa na sehemu ya USB kwenye tablet ya mwaka jana ya iPad Air (2019).

Sifa za Ndani za iPad Air (2020)

Kwa upande wa sifa za ndani iPad Air (2020) inakuja na sifa nzuri sana, kwa upande wa processor iPad hii inakuja na chipset mpya ya A14 Bionic (5 nm) yenye uwezo wa mkubwa sana tofauti na iPad zote za Apple ambazo zinatumia chipset ya A13 Bionic.

Kwa upande wa RAM hadi sasa hakuna taarifa kamili kuhusu RAM ya iPad hii, japokuwa inategemewa kuwa na uwezo wa kati ya GB 2 au GB 3 za RAM. Kwa upande wa ROM au uhifadhi wa ndani iPad Air (2020) inakuja kwa matoleo mawili tofauti, toleo lenye GB 64 na toleo lenye GB 256. Kama kawaida huwezi kuongeza uhifadhi huu kwa kutumia Memory card ya aina yoyote.

Kwa upande wa battery, iPad hii inakuja na battery ya Li-Po yenye uwezo wa hadi 28.6 Wh huku ikiwa na uwezo wa kudumu na chaji kwa muda wa masaa 10 kama utakuwa unaitumia kwa multmedia. iPad hii inakuja na sensor mbalimbali ikiwa pamoja na accelerometer, gyro, compass, na barometer.

Kampuni ya Apple Yazindua Toleo Jipya la iPad Air (2020)

Kama unataka kujua zaidi kuhusu sifa kamili pamoja na bei ya iPad Air (2020), unaweza kusoma zaidi hapa. Kama unataka kujua zaidi kuhusu saa za Apple Watch Series 6 na Watch SE, unaweza kusoma makala inayofuata.

1 comments
  1. pia mm nina facebook pages lkn napata shida kwenye payments issues nshawasiliana na facebook lkn naona bdo ni changamoto aina ya kadi ninayotumia ni master card kwa ajili ya payments lkn kila nkfanya muamala naambiwa muamala umediclined sijui shida ni master card au nn naomba mnsiadie na hilo kwenye post zangu ili niweze kubooat my post ni get payments if possible

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use