Baada ya kusubiri kwa muda mrefu pamoja na tetesi mbalimbali, hatimaye hivi leo kampuni ya Apple imetangaza kuzindua simu zake mpya za iPhone 12 siku ya tarehe 15 ya mwezi huu.
Kwa mujibu wa mialiko inayo tumwa kwa kampuni mbalimbali, mwaka huu Apple inatarajiwa kuzindua iPhone nne mpya. Tunatarajia kuona iPhone 12 yenye inch 5.2, iPhone 12 yenye inch 6.1, iPhone 12 Pro yenye inch 6.1, na iPhone 12 Pro Max yenye inch 6.7.
UPDATE 16-09-2020 : Baada ya Apple kufanya tamasha lake hapo Septemba 15, kampuni hiyo imezindua matoleo mpya ya iPad Air (2020) pamoja na Apple Watch Series 6 na Watch SE. Kwenye tamasha hilo Haku-kua na tangazo lolote la ujio wa iPhone 12, huku mitandao mbalimbali ikiandika kuwa simu hizo mpya zinatarajiwa kuzinduliwa mwezi ujao.
Inasemekana kuwa vifaa hivi vyote vinatarajiwa kuja na mtandao wa 5G. Lakini, ripoti zina onyesha kuwa ni iPhone 12 Pro Max pekee ndio itakayokuja na uwezo wa mmWave 5G. Pia kuna tetesi juu ya kuwepo kwa sensor ya IPD Pro LiDAR inayosemekana kuwepo kwenye toleo la iPhone 12 Pro.
Mbali na hayo, Apple pia inaweza kuzindua Mfululizo mpya wa Apple Watch 6. Isitoshe, kuna uvumi kwamba kampuni hiyo pia itazindua Apple Watch nyingine kuchukua nafasi ya Series 3. Tunaweza pia kuona Apple TV mpya, HomePod, pamoja na iPad Air.
Kama nilivyo sema hapo juu, uzinduzi huo umepangwa kufanyika mnamo Septemba 15 saa 10am PT. Hapa kwetu Tanzania hiyo ni saa mbili usiku mnamo Septemba 15.