Kampuni ya TECNO hivi karibuni inategemea kuzindua simu yake mpya ya Camon 16 hapo mwezi wa Tisa tarehe 3.
Kwa mujibu wa tovuti ya gadgets 360 ya nchini India, TECNO Camon 16 ambayo ni toleo la maboresho kwa Camon 15, inatarajiwa kuja na kamera nne kwa nyuma huku kamera kuu ikiwa na uwezo wa Megapixel 64 tofauti na Camon 15 ambayo inakuja kamera kuu ya Megapixel 48. Hata hivyo inasemekana kamera hizo kwa pamoja zitakuwa na uwezo wa kuchukua video za hadi 4K.
Mbali ya kamera za nyuma, Camon 16 inatarjiwa kuja na kamera mbili za selfie huku kamera hizo zikiwa na uwezo wa Megapixel 48 kila moja huku zote kwa pamoja zikiwa na uwezo wa kuchukua video za hadi 1080p@30fps.
Kwa kuwa TECNO imekua ikitangaza ujio wa simu hii kwa kutumia hashtag ya #MoreThanACameraPhone ni wazi kuwa Camon 16 itakuwa na maboresho zaidi kwenye upande wa kamera.
Pengine Camon 16 inaweza kuwa na sifa zizofanana kabisa na simu mpya ya Infinix Zero 8 ambayo imezinduliwa wiki iliyopita na Infinix huko nchini Indonesia. Infinix Zero 8 nayo inakuja na kamera nne za nyuma huku kamera kuu ikiwa na Megapixel 64, pamoja na kamera mbili za selfie huku kamera kuu ya selfie ikiwa na Megapixel 48.
Kwa sasa bado hakuna taarifa kama simu hizo zitakuja hapa Tanzania kama Camon 16 hivyo endelea kutembelea Tanzania Tech tutakujuza zaidi pindi tutakapo pata taarifa zaidi. Kujua zaidi kuhusu sifa na bei ya TECNO Camon 16 hakikisha unaendelea kutembelea Tanzania Tech tutakupa taarifa pindi simu hii itakapo zinduliwa.