Habari Kubwa za Teknolojia Kwa Wiki Iliyopita 22/8/2020

Apple sasa ina thamani ya $ Trillion 2, Telegram yaja na Video Call na Mengine..
Habari Kubwa za Teknolojia Kwa Wiki Iliyopita 22/8/2020 Habari Kubwa za Teknolojia Kwa Wiki Iliyopita 22/8/2020

Habari na karibu kwenye makala ya Tech Wiki, najua ni muda mrefu sana tokea nilipo andika makala hizi za tech wiki lakini leo imebidi kutoka na kutokuwa hewani kwa takribani muda wa siku tatu.

Hii inatokana na jambo jipya zuri ambalo natumaini wote mtalifurahia kwa namna moja ama nyingine pale litakapo kamilika. Anyway hiyo ni mada ya siku nyingine, hebu sasa tuangalie habari kubwa za teknolojia kwa wiki hii.

Advertisement

Telegram Yazindua Sehemu Mpya ya Video Call

Habari Kubwa za Teknolojia Kwa Wiki Iliyopita 22/8/2020

Mtandao wa telegram hivi karibuni umetangaza sehemu mpya ya kwenye app zake za Android na iOS. Sehemu hiyo itaruhusu watumiaji wote wa mtandao wa telegram kuweza kuwasiliana kwa video kwa urahisi kupitia sehemu hiyo.Mbali ya hayo, mtandao huo pia umetangaza kufikisha miaka 7 tokea ulipo anzishwa mwaka 2013.

Soma Zaidi Hapa

Sehemu Mpya ya Reel Kwenye Mtandao wa Instagram

Habari Kubwa za Teknolojia Kwa Wiki Iliyopita 22/8/2020

Wakati mtandao wa TikTok ukipitia matatizo mbalimbali na serikali za nchi mbalimbali, kampuni ya Facebook ambayo inamili mtandao wa Instagram, wiki iliyopita wametangaza ujio wa sehemu mpya ya Reels. Sehemu hii ni kama ilivyo TikTok kwani inakusaidia kurekodi video fupi yenye sauti yoyote unayoitaka. Reels kwa sasa imeanza kupataikana kwa baadhi ya watu na inategemewa kusambaa zaidi siku za karibuni.

Soma Zaidi Hapa

BlackBerry Kuzindua Simu Mpya 2021

Habari Kubwa za Teknolojia Kwa Wiki Iliyopita 22/8/2020

Ikiwa ni moja kati ya kampuni za kutengeneza simu za muda mrefu hatimaye bado kampuni ya Blackberry inataka kuendelea na utengenezaji wa smartphone. Kwa mujibu wa habari wiki hii kampuni ya Blackberry inategemea kumaliza mkataba wake na kampuni ya TLC hivyo inaonekana kuwa kampuni hiyo sasa imepata mshirika mpya.

Kampuni ya OnwardMobility imetangaza kushirikiana na BlackBerry kutengeneza simu mpya za BlackBerry ambazo zitatoka mwaka 2021. Simu hizo zinasemeakana kuwa na muonekano wa Blackberry ambao ndio ulitambulisha kampuni hiyo kwa watumiaji wake.

Soma Zaidi Hapa

Game ya Fortnite yaondolewa Play Store na App Store

Habari Kubwa za Teknolojia Kwa Wiki Iliyopita 22/8/2020

Kwa sasa moja kati ya habari ambayo inatawala tovuti nyingi za habari za teknolojia ni malimbano baina ya kampuni ya Epic game pamoja na kampuni ya Apple ambapo wiki hii kampuni hiyo ilichukua uamuzi wa kuondoa game hiyo kwenye soko lake la Play Store.

Hii imekuja baada ya kampuni ya Epic games kuchukua uamuzi wa kutengeneza mfumo wa malipo ndani ya game hiyo ambapo watumiaji huweza kununua baadhi ya vitu. Hata hivyo kwa mujibu wa Sheria za soko la Apple ni marufuku kwa game yoyote kuuza bidhaa bila ndani ya app bila kuweka mfumo wa malipo wa apple ambao hulazimisha mwenye game kukatwa asilimia 30 ya manunuzi.

Hata hivyo Epic Games ilishindwa kufuata sheria hizo na kuweka mfumo wake wa malipo ambapo ilifanya Game maarufu ya Fortnite kuondolewa kwenye soko la App Store. Hata hivyo kampuni ya Google nayo iliondoa app hiyo pia kutokana na sababu hizo hizo.

Soma Zaidi Hapa

Apple Tafikisha Thamani ya Trilioni 2 za Marekani

Habari Kubwa za Teknolojia Kwa Wiki Iliyopita 22/8/2020

Hivi karibuni kampuni ya Apple ifikisha thamani ya Trilioni 1 kwenye soko la hisa la marekani, lakini kama hiyo haitoshi hivi karibuni kampuni hiyo imekuwa kampuni ya kwanza kwa nchini Marekani kufikisha thamani ya dollar Trilioni 2 za marekani. Thamani ya kampuni hiyo imeongezeka kufikia thamani hiyo ndani ya muda wa miezi 24 tu.

Kampuni ya Apple sio kampuni pekee Duniani kufikisha thamani hiyo, kampuni ya Saudi Aramco, inayo jihusisha na gasi pamoja na mafuta, yenye makao yake makuu huko Saudi Arabia yenyewe ndio ilikuwa kampuni ya kwanza duniani kufikisha thamani hiyo ya dollar trilioni 2 mwaka 2019.

Soma Zaidi Hapa

Facebook Kusitisha Muonekano wa Zamani Mwezi Ujao

Habari Kubwa za Teknolojia Kwa Wiki Iliyopita 22/8/2020

Hivi karibuni kampuni ya facebook itangaza muonekano mpya wa tovuti yake, muonekano huo umekuwa kwenye majaribio kwa muda sasa huku kukiwa na njia ya kuwasha na kuzima muonekano huo. Hivi karibuni Facebook imetangaza kuwa muonekano huo wa zamani utaondolewa mwezi ujao na watumiaji wote wanatakiwa kutumia muonekano huo mpya ambao ni rahisi zaidi kutumia.

Soma Zaidi Hapa

Huawei Yazindua Laptop Mpya ya Matebook X

Habari Kubwa za Teknolojia Kwa Wiki Iliyopita 22/8/2020

Kampuni ya Huawei imetangaza ujio wa laptop yake mpya wiki hii, laptop hiyo inakuja na sifa bora na muonekano wa kisasa. Laptop hiyo inakuja kwa matoleo mawili tofaut pamoja na sifa zifuatazo

Processor: Intel® Core™ i5-10210U / Intel® Core™ i7-10510U
Display: FHD, 13.0 inches (diagonal)
RAM: 8/16 GB
Storage: 512 GB SSD
Web Cam: 720p Hidden camera
OS: Windows 10

Soma Zaidi Hapa

Infinix Yazindua Simu Mpya ya Infinix Smart 5

Habari Kubwa za Teknolojia Kwa Wiki Iliyopita 22/8/2020

Kampuni ya Infinix nayo wiki hii imetangaza ujio wa simu yake mpya ya Infinix Smart 5 huko nchini India, Simu hiyo inakuja na muonekano ulio zoeleka pamoja na mfumo wa Android 10 Go na sifa nyingine kama ifuatavyo.

CPU: Octa-core 1.8 GHz Cortex-A53
RAM: 2/3 GB
Storage: 32/64 GB
Display: IPS LCD, 6.6 inches
Camera: Triple 13 MP, QVGA, QVGA
OS: Android 10 (Go Edition)

Soma Zaidi Hapa

Kwa ufupi kabisa hizo ndio habari kubwa kwa wiki hii ambayo inaisha kesho jumapili tarehe 23 mwezi wa nane mwaka 2020. Kama unataka kujua zaidi kuhusu habari za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech kila siku pia hakikisha unatufuta kwenye kwenye channel yetu kupitia mtandao wa YouTube kwani kuna kitu kikubwa kinakuja.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use