Kama wewe ni kama mimi na unafurahia kuangalia picha na video kwenye mitandao ya kijamii, basi ni wazi kuwa kuna wakati unatamani kupakua video fulani au picha ili kushare na watu wako wa karibu kwenye akaunti zako za mitandao ya kijamii.
Lakini ni wazi kuwa kwa sasa zipo app nyingi sana zinazoweza kukusaidia kupakua video na picha kwa urahisi kutoka kwenye mitandao hiyo lakini pamoja na hayo, kuwa na app ya kupakua video na picha kwa kila mtandao hii hufanya simu yako kujaa bila sababu ya msingi.
TABLE OF CONTENTS
App ya Statas
Kuliona hili sasa unaweza kupakua video pamoja na picha kwenye mitandao yote ya kijamii kwa kutumia app ya Statas. App hii inakupa uwezo wa kupakua picha na video kutoka kwenye mitandao ya Instagram, Facebook, TikTok, Likee, Twitter pamoja na WhatsApp programu zote za WhatsApp.
Mbali ya kuwa na uwezo wa kupakua video na picha kutoka kwenye mitandao hiyo, pia utaweza kupakua video kutoka kwenye mitandao ya TikTok na Likee bila kuwa na alama au watermark ambayo hutokea pale unapo save video kupitia app hizo.
Mbali na hayo, pia utaweza kupakua Stories za akaunti mbalimbali bila kujali kama zina expire ndani ya masaa 24.
Kitu kingine bora kuhusu app hii ni kuwa utaweza kuhifadhi picha zote ulizo pakua kwenye simu yako lakini kupitia ndani ya app hii utaweza kuona vitu vyote ulivyo pakua na vitapangwa kulingana na mtandao. Kwa mfano : kama ulipakua video kutoka mtandao wa TikTok basi moja kwa moja utaikuta kwenye sehemu ya Galler ndani ya app hiyo kwenye ukurasa wa TikTok.
Jinsi ya Kutumia Statas
Kutuia app hii ni rahisi, pakua app hii kupitia link hapa au bofya hapo chini kisha baada ya hapo ingia kwenye mtandao unao upenda kisha copy link ya post unayotaka kupakua na moja kwa moja utaweza kuona app hiyo ikiruhusu wewe kupakua picha au video. Bofya notification na kisha bofya Download.
Kama utakuwa umependa app hii basi unaweza kusoma makala hii, ambapo tumonyesha apps nyingine tatu ambazo zinaweza kukusaidia kupakua audio na video kwa urahisi na haraka.