Jinsi ya Ku-Backup na Ku-Restore SMS Zilizofutika

Hatua kwa hatua jinsi ya kubackup SMS kupitia simu yako ya Android
Jinsi ya Ku-Backup na Ku-Restore SMS Zilizofutika Jinsi ya Ku-Backup na Ku-Restore SMS Zilizofutika

Kama wewe ni mmoja wa watu ambao wanasoma makala hii ni wazi kuwa umeshawahi kukutana na tatizo la kupoteza SMS ya muhimu ambayo pengine unataka kujua jinsi ya kuirudisha.

Kama unalo tatizo hilo basi endelea kusoma makala hii hadi mwisho nitakufundisha njia rahisi ya kuweza kurudisha meseji iliyopotea au kufutika. Lakini kabla ya yote ni vizuri ufahamu kidogo kuhusu jinsi ya kufanya backup ya SMS zako ili usipoteze tena SMS zako.

Kwa kuanza Download app hiyo kwa kubofya hapo link hapo chini, kisha kupakua app hiyo moja kwa moja kwenye simu yako ya Android.

Advertisement

Download App Hapa

Jinsi ya Ku-Backup na Ku-Restore SMS Zilizofutika

Baada ya kupakua app hiyo kwenye simu yako, basi endelea kuwa kufungua app hiyo kisha fuata hatua hizi. Bofya Get Started kisha ruhusu app hiyo kwenye permission mbalimbali.

Jinsi ya Ku-Backup na Ku-Restore SMS Zilizofutika

Jinsi ya Ku-Backup na Ku-Restore SMS Zilizofutika

Kama unataka kufanya Backup kwa sasa bofya Set up a Backup, baada ya hapo chagua data ambazo unataka kuhifadhi.

Jinsi ya Ku-Backup na Ku-Restore SMS Zilizofutika

App hii inaweza kufanya backup ya SMS na pia inaweza kufanya backup ya Call Log. Call log hii itakusaidia kuhifadhi namba ambazo ulipigiwa na ulisahau kusave. Kama unataka kufanya backup ya SMS na Call logs hakikisha sehemu hizo zote zimewashwa kwenye hatua hii. Baada ya hapo bofya Next iliyopo chini kulia.

Jinsi ya Ku-Backup na Ku-Restore SMS Zilizofutika

Baada ya hapo, kwenye ukurasa unafuata chagua sehemu unayotaka kuhifadhi backup yako. Unaweza kuchagua kati ya Google Drive, Dropbox au kwenye Simu yako. Kwenye hatua hii ni muhimu kuchagua Google Drive kwani itakusaidia kurudisha SMS hizo hata kama ukipoteza simu yako au simu yako ikiharibika. Baada ya hapo bofya Next

Jinsi ya Ku-Backup na Ku-Restore SMS Zilizofutika

Kama ilivyo WhatsApp pia utaweza kuchagua muda wa kufanya backup, kwenye hatua hii chagua muda ambao unataka SMS zako au Call logs zihifadhiwe. Unaweza kuchagua Kila siku, Kila wiki au Kila baada ya lisaa.

Jinsi ya Ku-Backup na Ku-Restore SMS Zilizofutika

Baada ya kuchagua muda, moja kwa moja bofya kibonyezo cha Backup Now kilichopo chini upande wa kulia.

Jinsi ya Ku-Backup na Ku-Restore SMS Zilizofutika

Jinsi ya Restore (Kurudisha) SMS Meseji Zlizofutika

Kama kwa namna yoyote sasa unataka kurudisha meseji zilizo futika kwa bahati mbaya kwenye simu yako, unaweza kufuata hatua hizi rahisi. Fungua app hiyo ya SMS Backup & Restore kisha bofya sehemu ya menu iliyopo kushoto juu.

Jinsi ya Ku-Backup na Ku-Restore SMS Zilizofutika

Baada ya hapo kwenye menu hiyo tafuta sehemu iliyoandikwa Restore, sehemu hiyo ni ya tatu kwenye menu hiyo kutoka juu.

Jinsi ya Ku-Backup na Ku-Restore SMS Zilizofutika

Chagua backup unayotaka kurestore, kama unazo backup tofauti hakikisha unachagua backup ambayo unataka, bila shaka unataka backup mpya, hivyo chagua backup yenye tarehe ya karibuni.

Jinsi ya Ku-Backup na Ku-Restore SMS Zilizofutika

Baada ya hapo, sasa endelea kwa kubofya kitufe cha Restore kilichopo chini upande wa kulia.

Jinsi ya Ku-Backup na Ku-Restore SMS Zilizofutika

Kabla ya kuanza kurudisha meseji zako unatakiwa kuruhusu app hii kuweza kurudisha meseji zako kwa kubofya sehemu ya OK ambayo itatokea kwenye maelezo yatakayo kuja ya kioo cha simu yako mara baada ya hatua iliyopita.

Jinsi ya Ku-Backup na Ku-Restore SMS Zilizofutika

Baada ya hapo sasa bofya kuruhusu app hii kuwa default kwa muda kwa kubofya Yes kwenye hatua hiyo ili kuanza kurudisha meseji zako moja kwa moja.

Jinsi ya Ku-Backup na Ku-Restore SMS Zilizofutika

Baada ya hapo subiri kidogo wakati meseji zako zikiwa zinarudishwa kwenye simu yako na baada ya kukamilika hatua hii utaweza kupata meseji zako zote pamoja na Call Log kama ulichagua.

Jinsi ya Ku-Backup na Ku-Restore SMS Zilizofutika

Jinsi ya Ku-Backup na Ku-Restore SMS Zilizofutika

Rudisha SMS Kwa Kompyuta iOS na Android

Kama umepoteza meseji na ulikuwa huna programu hiyo, basi unaweza kujaribu njia nyingine ambazo ni lazima kuwa na kompyuta. Kama unayo kompyuta unaweza kutumia programu zifuatazo kurudisha SMS zilizofutika au kupote kwenye simu yako kwa bahati mbaya.

Fonepaw

Hii ni programu ya bure ambayo itakusaidia sana kuweza kurudisha data zilizopote kwenye simu yako ya Android au iOS, uzuri wa programu unaweza kutumia kwa muda bure na unaweza kupakua na kuanza kutumia moja kwa moja kwenye kifaa cha mfumo wa Windows au MacOS.

Jinsi ya Ku-Backup na Ku-Restore SMS Zilizofutika

Download FonePaw Hapa

Kudownload Programu hii ingia kwenye link hapo juu kisha bofya Products baada ya hapo chagua kati ya FonePaw for Android Includes au FonePaw for iOS Includes kisha bofya Free Download.

Jinsi ya Ku-Backup na Ku-Restore SMS Zilizofutika

Mpaka hapo natumaini utakuwa umeweza kurudisha SMS au meseji zilizo futika kwenye simu yako kwa urahisi na haraka. Kama kwa namna yoyote utakuwa umekwama unaweza kuandika maoni hapo chini nasi tutakusaidia moja kwa moja. Kama unataka kujifunza kwa vitendo unaweza kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech kupitia mtandao wa YouTube Hapa.

Kwa muajanja zaidi hakikisha unasoma makala iliyopita ya jinsi ya kufungua application yoyote kwa kutumia SMS au ujumbe mfupi wa maneno.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use