Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Twitter Kuja na ‘Fleets’ Sehemu Kama Stories ya Instagram

Sasa jiandae kutumia Stories kupitia mtandao wa Twitter
Twitter Kuja na ‘Fleets’ Sehemu Kama Stories ya Instagram Twitter Kuja na ‘Fleets’ Sehemu Kama Stories ya Instagram

Mtandao wa Twitter hivi karibuni umeanza kufanya majaribio ya sehemu mpya ya Fleets sehemu ambayo itakuwa inafanana na sehemu ya Instagram Stories.

Sehemu hiyo mpya itakuwa inaonekana juu kabisa ya programu au tovuti ya Twitter kama inavyokuwa stories kwenye mtandao wa Instagram.

Advertisement

Kama ilivyo Stories za mitandao mingine, kupitia Fleets pia utaweza kuweka fleets au stories ambazo zinapotea ndani ya masaa 24 huku ukiwa na uwezo wa kuweka Fleets za maandishi zenye idadi ya maneno 280, pia unaweza kuweka picha, GIF pamoja na video zenye urefu wa hadi dakika 2 na sekunde 20.

Pia utaweza kushare link na mambo mengine kama ambavyo unafanya pale unapokuwa unapost tweet ya kawaida.

Twitter Kuja na ‘Fleets’ Sehemu Kama Stories ya Instagram

Kwa sasa tayari sehemu hiyo mpya inapatikana kwa watumiaji wa Twitter nchini Brazili huku siku ya leo Twitter ikiwa imetangaza kuzindua sehemu hiyo kwa watumiaji wake wa nchini India. Kwenye mitandao yote mikubwa ya kijamii, Twitter pekee ndio ulikuwa mtandao ambao hauna sehemu hiyo ya Stories, mara baada ya YouTube kuwezesha sehemu yake ya Stories mwaka 2017.

Kupata taarifa pindi sehemu hii itakapo kuja hapa nchini Tanzania, hakikisha unaendelea kutembelea Tanzania Tech kila siku.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use