Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Tengeneza Pesa Mtandaoni Kupitia Tovuti Hizi (2022)

Kama umenyimwa matangazo na Adsense basi jaribu mitandao hii
Tengeneza Pesa Mtandaoni Kupitia Tovuti Hizi (2022) Tengeneza Pesa Mtandaoni Kupitia Tovuti Hizi (2022)

Kama wewe ni mmoja wa watu ambao wamewahi kutafuta njia za kutengeneza pesa kupitia mtandao basi lazima unafahamu kuhusu Google Adsense. Kama bado ufahamu kuhusu Adsense usijali kwani unaweza kusoma makala hii hapa nimejitahidi kueleza kidogo kuhusu Google Adsense.

Lakini kama umekuwa ukipata shinda ya tovuti yako kuwa Approved na Adsense kutoka na sheria zao, basi makala hii ni kwa ajili yako kwani kwenye list hii ipo mitandao ambayo inafanana na Adsense ambayo sheria zake ni tofauti kidogo na sheria za Google Adsense.

Advertisement

Sheria za mitandao hii hazijalishi sana aina ya blog au tovuti uliyo nayo huku mitandao mingine ikiruhusu kuonyesha matangazo hata kwenye tovuti za kiswahili au lugha nyingine tofauti na kingereza hivyo kuwa rahisi kwa watu wengi hasa watanzania kujiunga kwa haraka na urahisi.

Basi baada ya kusema hayo twende moja kwa moja kwenye list hii, kumbuka ni muhimu kusoma maelezo ya mtandao ili kujua kama unakubali tovuti ya kiswahili.

Media.net

Tengeneza Pesa Mtandaoni Kupitia Tovuti Hizi (2022)

Media.net ni mbadala bora kwa AdSense kwa suala la aina za matangazo.

Media.net ni mtandao wa matangazo ambao unamilikiwa na Yahoo! na Bing!, Mtandao huu unatoa matangazo yanayolipa zaidi. Mtandao huu unakuja na aina za matangazo zinazo fanana kabisa na Adsense huku ikiwa na viwango vinavyo lipa zaidi pengine kuliko Adsense.

  • Sheria zake – Ngumu
  • Lugha zinazo kubaliwa – English Pekee
  • Kiwango cha Chini cha Malipo – Dollar $100
  • Muda wa kukubaliwa – Siku mbili za kazi au Siku 7

MUHUMU : Mtandao huu unafaa kwa wale ambao tayari wanazo tovuti zinazo onyesha matangazo ya Adsense na wanataka kuongeza kipato zaidi.

Jiunge na Mtandao wa Media.net

PropellerAds

Tengeneza Pesa Mtandaoni Kupitia Tovuti Hizi (2022)

PropellerAds ni moja ya mtandao ambao unalipa zaidi na ni moja ya mtandao ambao ni mbadala bora wa Adsense kwa sasa.

Mtandao huu unakuja na aina mbalimbali za matangazo ambayo yanaruhusu tovuti yoyote kuweza kutengeneza pesa kwa haraka na urahisi. Kama unayo tovuti ambayo imekataliwa kwenye mtandao wa Google Adsense basi hakikisha unajaribu mtandao huu.

  • Sheria zake – Haina Sheria (Rahisi)
  • Lugha zinazo kubaliwa – Lugha yoyote
  • Kiwango cha Chini cha Malipo – Dollar $25
  • Muda wa kukubaliwa – Unakubaliwa Hapo Hapo.

MUHIMU : Mtandao huu ni bora kwa mtu yoyote mwenye tovuti ya kiswahili au tovuti yoyote inayo husisha maswala ya kudownload.

Jiunge na Mtandao wa PropellerAds

Adversal

Tengeneza Pesa Mtandaoni Kupitia Tovuti Hizi (2022)

Adversal ni mtandao mwingine ambao ni mbadala wa Adsense, mtandao huu unakuja na njia tofauti za kutengeneza pesa kwa haraka.

Kama wewe ni mmoja wa watu ambao wanazo tovuti ambazo zinapata views nyingi lakini bado huna matangazo kwenye tovuti yako basi unaweza kujaribu mtandao wa Adversal. Mtandao huu unakuja na aina mbalimbali za matangazo ambayo yanaweza kukusaidia kupata pesa zaidi.

  • Sheria zake – Ngumu Unahitaji View 50,000 kwa Mwezi
  • Lugha zinazo kubaliwa – Lugha yoyote
  • Kiwango cha Chini cha Malipo – Dollar $20
  • Muda wa kukubaliwa – Baada ya siku moja au wiki moja.

MUHIMU : Mtandao huu ni bora kwa mtu yoyote mwenye tovuti ya ambayo inao watumiaji wengi. Unaweza kutengeneza pesa kwa haraka sana kama tovuti yako ni maarufu.

Jiunge na Mtandao wa Adversal

ylliX

Tengeneza Pesa Mtandaoni Kupitia Tovuti Hizi (2022)

ylliX ni mtandao mwingine ambao ni mbadala wa Adsense, mtandao huu unalipa zaidi huku ukiruhusu aina mbalimbali za matangazo.

Kama wewe upo nchini Tanzania na umekuwa ukitafuta mbadala wa Adsense basi unaweza kujaribu mtandao wa ylliX. Mtandao huu unakuja na aina mbalimbali za matangazo huku ukiwa na njia mpya za kuruhusu watanzania kupokea pesa kupitia bank za hapa Tanzania.

  • Sheria zake – Haina Sheria (Rahisi)
  • Lugha zinazo kubaliwa – Lugha yoyote
  • Kiwango cha Chini cha Malipo – Dollar $2
  • Muda wa kukubaliwa – Unakubaliwa hapo hapo.

MUHIMU : Mtandao huu ni bora kwa mtu yoyote mwenye tovuti ya Kiswahili au tovuti yoyote ambayo imekataliwa kwenye mtandao wa Google Adsense.

Jiunge na Mtandao wa ylliX

Infolinks

Tengeneza Pesa Mtandaoni Kupitia Tovuti Hizi (2022)

infolinks ni mtandao mwingine ambao ni mbadala wa Google Adsense, mtandao huu unakuja na njia za tofauti za kutengeneza pesa kwa urahisi.

Kama wewe ni mmoja wa watu ambao wanatafuta njia za tofauti za kutengeneza pesa basi jaribu mtandao huu wa infolinks. Mtandao huu unakuja na njia maalum ambayo uweka link maalum kwenye makala, link ambazo mtu anapo bofya basi unaweza kutengeneza pesa.

  • Sheria zake – Haina Sheria (Rahisi)
  • Lugha zinazo kubaliwa – Lugha yoyote
  • Kiwango cha Chini cha Malipo – Dollar $20
  • Muda wa kukubaliwa – Siku moja ama mbili.

MUHIMU : Mtandao huu ni bora kwa mtu yoyote mwenye tovuti ya yenye makala mbalimbali hasa makala zenye maneno ya kingereza au maneno ya bidhaa.

Jiunge na Mtandao wa Infolinks

Propush me

Tengeneza Pesa Mtandaoni Kupitia Tovuti Hizi (2022)

Propush me ni mtandao mwingine ambao ni mbadala wa Adsense, mtandao huu unakuja na matangazo ya Notification ambayo yanaweza kukusaidia kupata pesa zaidi.

Kama unataka kuongeza kipato kwa haraka basi unaweza kujaribu mtandao huu wa Propush me, mtandao huu unakupa uwezo wa kupata pesa kutokana na kila subscriber yani baada ya mtu kuscriber basi unapata pesa yako moja kwa moja na kadri unavyozidi kuwa na watu wengi ndivyo unavyopata pesa zaidi kupitia mtandao huu.

  • Sheria zake – Haina Sheria (Rahisi)
  • Lugha zinazo kubaliwa – Lugha yoyote
  • Kiwango cha Chini cha Malipo – Dollar $20
  • Muda wa kukubaliwa – Hapo hapo.

MUHIMU : Mtandao huu ni bora kwa mtu yoyote mwenye tovuti ya kudownload, kama unataka kupata pesa kwa haraka basi jaribu mtandao huu.

Jiunge na Mtandao wa Propush me

Na hiyo ndio baadhi ya mitandao ambayo ni mbadala wa mtandao wa Adsense, kumbuka hii ndio baadhi ya mitandao ambayo tumewahi kujaribu na kuweza kuona mafanikio yake. Kama unataka kujua zaidi unaweza kusoma hapa kuona jinsi tulivyo tumia moja ya mtandao huu kutengeneza zaidi ya milioni 20 za kitanzania.

Kujua zaidi jinsi ya kupata pesa mtandaoni hakikisha una tembelea tovuti yetu kila siku, pia usisahau kusubscribe kwenye channel yetu kupitia mtandao wa YouTube ili kujifunza kwa vitendo.

3 comments
  1. Hello Tanzania tech, nimejiunga kwenye hy mitandao. Mfano propush ,infolinks na yllix lakini nimeshindwa kuunganisha na website yangu. Kama hutojali naomba unielekeze au kama kuna video ya kuangalia naomba unisaidie. Namba yangu 0628469436 (ipo whatssap

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use