in

Waya za Muhimu Kuwa Nazo Kama Unamiliki Eletroniki

Hizi hapa cable za muhimu kuwa nazo kama unamiliki kifaa cha kieletroniki

Waya za Muhimu Kuwa Nazo Kama Unamiliki Eletroniki

Habari karibu kwenye makala nyingine, leo nimekuletea makala ya tofauti kidogo ambapo nimekuandalia baadhi ya cable (viunganishi) ambavyo ni muhimu sana kwenye maisha ya kila siku. Viunganishi hivi ni muhimu sana kwani vinaweza kukusaidia sana hasa kwa wewe unaemiliki kifaa chochote cha kielektroniki kama TV, simu au computer.

Basi bila kuendelea kupoteza muda, twende moja kwa moja kwenye makala hii. Kumbuka unaweza kununua bidhaa hizi moja kwa moja kwenye soko la kikuu kupitia link maalum chini ya bidhaa usika.

Install Android App
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot

OTG Cable Adapter – TZS 4,240

Waya za Muhimu Kuwa Nazo Kama Unamiliki Eletroniki

Hii ni OTG Cable, cable hii inaweza kukusaidia sana kama unataka kuunganisha simu yako na kifaa chochote kinacho tumia USB. Kupitia cable hii unaweza kuunganisha Flash Drive kwenye simu yako, pia unaweza kuunganisha Controller ya game na kutumia controller hiyo kucheza game kwenye simu yako, mbali na hayo pia unaweza kuchomeka Mouse ya kompyuta na kuendesha simu yako kwa kutumia Mouse, pamoja na mambo mengine mengi.

Nunua OTG Cable (Kikuu)

Micro HDMI Male Cable – TZS 6,466

Waya za Muhimu Kuwa Nazo Kama Unamiliki Eletroniki

Kama kwa namna yoyote unataka kuunganisha TV yako yenye HDMI pamoja na smartphone yako basi cable hii ni ya muhimu sana. Kupitia cable hii utaweza kuunganisha simu yako na TV hivyo utaweza kufanya kila kitu kilichopo kwenye simu yako kuonekana kupitia TV yako kwa mfumo wa HD,unaweza kutumia waya huu kuangalia movie zilizopo kwenye simu yako pamoja na mambo mengine yote kutoka kwenye simu yako kwenda kwenye TV yako.

Nunua Micro HDMI Male Cable (Kikuu)

HDMI Splitter Cable – TZS 11,925

Waya za Muhimu Kuwa Nazo Kama Unamiliki Eletroniki

Kama kwa namna yoyote unataka kuunganisha vifaa viwili au zaidi vyenye kutumia HDMI badi cable hii ni muhimu sana kwako. Cable hii itakusaidia kama kwa mfano unataka kutengeneza work station (Sehemu ya Computer ya Kufanya Kazi) ambapo unataka kuunganisha vioo viwili vya computer kwenye computer moja basi cable hii itakusaidia sana.

Nunua HDMI Splitter Cable (Kikuu)

iOS Hdmi Lightning Cable – TZS 51,675

Waya za Muhimu Kuwa Nazo Kama Unamiliki Eletroniki

Kama wewe ni mtumiaji wa iPhone au iPad na ungependa kuangalia movie au video zilizopo kwenye simu yako kwenye TV yako basi cable hii ni muhimu sana kwako. Kupitia Cable hii utaweza kuunganisha TV yako yenye HDMI na simu yoyote au kifaa chochote kinacho tumia mfumo wa iOS.

Nunua iOS HDMI Lightning Cable (Kikuu)

VGA Male to HDMI Cable – TZS 15,768

Waya za Muhimu Kuwa Nazo Kama Unamiliki Eletroniki

Kama unayo kompyuta au kifaa chochote cha zamani chenye kutumia VGA basi cable hii inaweza kusaidia sana. Kupitia cable hii unaweza kubadilisha kifaa chochote chenye VGA na kutumia HDMI. Kama unavyojua HDMI hutumika kuonyesha picha angavu zaidi hivyo unaweza kutumia cable hii kupata muonekano bora wa movie kutoka kwenye kifaa chenye VGA.

Nunua VGA Male to HDMI Cable (Kikuu)

List inaendelea..

Na hizo ndio baadhi ya cable ambazo ni muhimu sana kuwa nazo, unaweza kununua cabel hizi na kuwa nazo kwani zinaweza kukusaidia kwenye hali mbalimbali. Kumbuka list hii inendelea kuongezwa kadri tutakapo kutana na cable ambazo ni muhimu kwa namna moja ama nyingine.

Pia kumbuka kuwa unapo nunua cable hizi hakikisha una agiza cable ambayo inafanana na simu yako kwa namna zote, pia unaweza kuwasiliana na seller kabla ya kununua cable husika.

Waya za Muhimu Kuwa Nazo Kama Unamiliki Eletroniki
Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Tengeneza Video Bora za YouTube, TikTok na Instagram Kupitia Simu

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.

One Comment