Kama wewe ni mmoja wa watu ambao wana miliki akaunti kwenye mtandao wa youtube basi pengine hii ni sababu ya wewe kusoma makala hii, kama huna akaunti kwenye mtandao wa youtube na ulikuwa unafikiria kuwa na akaunti basi pengine ni vizuri kusoma makala hii kabla ya kuendelea kwenye hatua ya kufungua channel yako.
Kupitia makala hii nitaenda kukwambia ni njia gani za kutumia kupata pesa zaidi kwenye mtandao wa youtube ikiwa pamoja na kujibu baadhi ya maswali ambayo pengine yalikua yanakusumbua sana.
Kwa kuanza labda tukubaliane kwamba, Subscriber ni sehemu muhimu sana kwenye channel yako hasa kama unatarajia kuanza au ndio kwanza umeanza. Pia ukumbuke kuwa subscriber ndio kitu cha muhimu kinacho saidi wewe kuanza kutengeneza pesa kwenye channel yako kutokana na sheria ya youtube ambayo ina ainisha kuwa na subscriber pamoja na views kuanza kutengeneza pesa kupitia mtandao wa YouTube.
Kama unavyoweza kuona, kwa mujibu wa youtube unahitaji kuwa na subscriber wasio pungua 1000 na views 4000 ndani ya kipindi cha mwaka mmoja au miezi 12. Hii tu ni sehemu ambayo inaonyesha kuwa subscribers ni muhimu sana tena zaidi kama unataka kuanza. Hivyo basi, wakati unafikiria kuanzisha channel kwaajili ya kujipatia kipato mtandaoni ni muhimu kuangalia subscriber ili kufikia malengo yako mapema.
TABLE OF CONTENTS
Je Subscribers Wengi Ndio Pesa Nyingi Youtube.?
Jibu la moja kwa moja kwenye swali hilo ni HAPANA, kuwa na subscriber wengi haku maanishi kuwa channel fulani inaingiza kipata kwa wingi au lah. Bali hii ufikiriwa hivyo kwani watu wengi hudhania kuwa na subscriber wengi ndio hufanya watu wengi zaidi kuangalia video hivyo mtu kutengeneza kipato zaidi.
Je Kitu Gani Kinaweza Kusaidia Kutengeneza Pesa Zaidi YouTube.?
Jibu la moja kwa moja la swali hili ni VIEWS, haijalishi una subscribers wangapi kwenye channel yako kitu cha muhimu ni views. Watu wengi wanapo angalia video zako hii ina maanisha kuwa watu wengi wanaona matangazo yanayopita kwenye video zako hivyo kutengeneza pesa zaidi, hii ni muhimu kwani mtu anaweza kuona video zako bila hata kuwa mmoja wa subscribers wako. Hivyo ni muhimu kutengeneza Views nyingi zaidi kama unataka kutengeneza pesa zaidi.
Je Unawezaje Kujua Kama Channel Inatengeneza Pesa Zaidi.?
Kama unataka kujua kama channel inatengeneza pesa nyingi zaidi basi unaweza kuangalia jumla ya views ambayo inapatikana kwenye ukurasa wa about kwenye channel yako au ya mtu yoyote.
Kama unavyoweza kuona hiyo ni idadi ya views kwenye channel yetu ya Tanzania Tech, views hizo ndio zinaweza kuonyesha kiasi cha pesa ambacho channel inaweza kutengeneza, unaweza kurekodi kwa wiki views zilikuwa ngapi alafu baada ya wiki unaweza kuangalia kujua kama views zimebadilika kwa kiasi kikubwa. Kama kuna mabadiliko makubwa basi channel hiyo inatengeneza pesa nyingi zaidi.
Je Unafanyaje Kuongeza Views Zaidi.?
Ukweli ni kwamba hata mpaka sasa binafsi najifunza kuongeza view kwenye video zetu, lakini kifupi ni kuwa hakuna njia moja ya kuongeza view kwenye video, zipo njia nyingi sana za kuongeza view ikiwa pamoja na kushare video kwenye mitandao ya kijamii na mengine mengi ya muhimu. Unaweza kufanya mambo haya machache ili kuongeza views.
- Andika vichwa vya habari vinavyo vutia watu zaidi.
- Weka Thumbnail au picha za video zinazo vutia zaidi.
- Tengeneza video zenye ubora.
- Tengeneza video zenye kutoa elimu ambayo itasaidia video zako kuangaiwa zaidi.
- Tengeneza video zinazodumu YouTube.
- Shiriki video kwenye mitandao yako ya kijamii.
- Tumia sehemu ya Discussion kutangaza video zako.
Mpaka hapo natumaini umejua kuwa views ni muhimu kuliko subscriber kwenye channel yako. Kumbuka ni muhimu kuweka video mpya mara kwa mara kwani hii itasaidia watu kuweza kujua channel yako na channe yako kutazamwa zaidi na hivyo kutengeneza pesa zaidi.
Maoni*kwaiyo views 4000 kwa video 1 au zote utakazotia ndo zinaesabiwa ukaanza kupata hela