Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

TECNO Yazindua Simu Mpya ya Spark 5 Nchini Ghana

Simu hii mpya ya TECNO Spark 5 Inakuja na sifa bora tofauti na Spark 4
TECNO Yazindua Simu Mpya ya Spark 5 Nchini Ghana TECNO Yazindua Simu Mpya ya Spark 5 Nchini Ghana

Kampuni ya TECNO hivi leo imetambulisha kwa mara ya kwanza toleo jipya la simu mpya ya TECNO Spark 5, simu ambayo ni toleo la maboresho kutoka kwenye simu za Spark 4 ambazo zilizinduliwa mwaka jana 2019.

Simu hii mpya ya TECNO Spark 5 inakuja na maboresho mengi sana ikiwa pamoja na uwezo zaidi wa kamera pamoja na battery. Tukianza na upande wa kioo, simu hii mpya ya Spark 5 inakuja na kioo cha inch 6.6, kioo ambacho kime tengenezwa kwa teknolojia ya IPS LCD huku pia kikiwa na uwezo wa kuonyesha picha na video za hadi resolution ya hadi pixel 720 kwa 1600.

Advertisement

TECNO Yazindua Simu Mpya ya Spark 5 Nchini Ghana

Kwa juu simu hii inakuja na kamera ya Megapixel 8, kamera ambayo ipo juu ya kioo ambayo pia ina saidiwa kupiga picha za selfie zenye mwanga kwa kutumia flash ya LED. Simu hii pia inakuja na teknolojia ya AI au Artificial Intelligence, hivyo tegemea kupata picha za selfie zenye mwanga na rangi bora zaidi.

Kwa nyuma, simu hii inakuja na kamera nne ambapo kamera kuu inakuja na Megapixel 13, nyingine mbili zikiwa na Megapixel 2 kila moja, na kamera ya mwisho ikiwa na Megapixel 0.3. Kamera zote kwa pamoja zina saidiwa na teknolojia ya AI pamoja na LED Flash nne, huku kamera hizo kwa pamoja zikiwa na uwezo wa kuchukua video za hadi pixel 1080p@30fps.

TECNO Yazindua Simu Mpya ya Spark 5 Nchini Ghana

Kwa upande wa sifa za ndani, TECNO Spark 5 inakuja na processor yenye speed ya hadi Octa-core (4×2.0 GHz Cortex-A53 & 4×1.8 GHz Cortex-A53). CPU hiyo ina saidiwa na RAM ya GB 2 pamoja na uhifadhi wa ndani wa hadi GB 32. Unaweza kuongeza uhifadhi huo kwa kutumia memory card ya hadi GB 256.

Mbai na hayo simu hii inakuja na mfumo mpya wa Android 10 huku juu yake kukiwa na mfumo wa wa HiOS 6.1, pia simu hii inakuja na sehemu ya fingerprint ambayo ipo kwa nyuma, Radio FM pamoja na sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama headphone jack. TECNO Spark 5 pia inakuja na uwezo wa mtandao wa hadi 4G.

Kwa upande wa battery simu hii inakuja na battery kubwa ya 5000 mAh, ambayo imetengenezwa kwa teknolojia ya Li-Po. Battery ambayo inaweza kudumu na chaji kwa siku nzima kulingana na matumizi yako, pia vilevile Spark 5 ni moja kati ya simu za TECNO zenye teknolojia ya Fast Charging ambayo husaidia simu kujaa chaji kwa haraka.

TECNO Yazindua Simu Mpya ya Spark 5 Nchini Ghana

Kwa upande wa bei, simu hii kwa sasa imezinduliwa nchini Ghana na inatarajiwa kupatikana kwanza nchini humu na baada kuja kwenye nchi nyingine za Afrika kama Tanzania. Simu hii kwa sasa inapatikana kwa Ghanaian Cedi GHS 720 ambayo ni sawa na takribani Shilingi za kitanzania TZS 286,000 bila kodi. Simu hii inapatikana kwa rangi nne za Misty Grey, Vacation Blue, Ice Jadeite, pamoja na Spark Orange.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use