Mtandao wa TikTok ni moja kati ya mitandao ambayo hadi sasa imekuwa na umaarufu mkubwa sana kutokana na kutumiwa na watu mbalimbali duniani kote. Hivi karibuni inasemekana mtandao huo umekuwa kwa kasi na kuwa na watumiaji zaidi ya bilioni 1 kwa kipindi cha muda mfupi sana.
Kutokana na kuwa mtandao huo umekuwa ni maarufu na kutumiwa na watu wengi sana, leo nimeona nikuandalie makala fupi na rahisi ambayo itakusaidia kujua jinsi ya kutumia mtandao wa TikTok pamoja na kufahamu kazi ya vitu mbalimbali ndani ya app hiyo. Basi bila kuendelea kupoteza muda wako zaidi twende moja kwa moja kwenye makala hii.
TABLE OF CONTENTS
Muonekano wa Mtandao wa TikTok
Mara baada ya kupakua app ya TikTok, utaweza kupata muonekano ambao ni mrahisi kwa watumiaji wa muda mrefu, lakini kama wewe ni mgeni na hii ndio mara yako ya kwanza kutumia mtandao wa TikTok basi hivi ndivyo mtandao huo unavyo onekana kwenye ukurasa wa mwanzo.
Kama unavyoweza kuona hapo juu utakapo ingia kwanza kwenye mtandao wa TikTok sehemu za muhimu kwa sasa ni sehemu hizo tatu ambazo nime kuonyesha. Sehemu hizo hutumiwa na watu wengi hasa wale ambao ni wageni kwenye app hiyo. Kwa ufupi kabisa hizi ndio kazi za sehemu hizo tatu ambazo nime kuonyesha hapo juu.
- Sehemu hii hutumika zaidi kufuata watu au kuangalia video ambazo zinaendana na wewe, naposema zina endana na wewe hapa nina maana kuwa, mtandao wa TikTok unatumia mfumo wa AI ambapo kadri unapo angalia video ndivyo inapojua zaidi video unazo zipenda na ndivyo unavyo endelea kuziona zaidi kwenye ukurasa huo.
- Kupitia sehemu ya pili hapo juu utaweza kutumia sehemu hiyo kuangalia profile ya mwenye video, chini yake ni sehemu ya kulike video hiyo, na chini yake ni sehemu ya kutoa maoni, na kama simu yako inayo kioo kifupi utaweza kuona vidoti vitatu ambavyo ukigusa hapo utaona alama ya mshale ambayo itakuruhusu kushare video hiyo kwenye mitandao mingine au kudownload, pamoja na mambo mengine.
- Sehemu ya mwisho hii itakusaidia kuona video nyingine ambazo zimetumia sauti ambayo video hiyo imetumia. Hapa utaweza kuona video nyingi tofauti zenye sauti hiyo hiyo iambayo inafanana na kwenye video unayo angalia kwa wakati huo. Sehemu hii ni muhimu na ndio yenye kuleta utofauti wa mtandao wa TikTok na mitandao mingine.
Jinsi ya Kupost Video Kwenye Mtandao wa TikTok
Baada ya kujua kuhusu sehemu hizo za muhimu sasa endelea kwenye hatua ya pili ambapo ni jinsi ya kupost video kwenye mtandao wa TikTok. Kupitia hapa utaweza kupost video za kuweka au ku-upload, au unaweza kutengeneza video zako kwa kurekodi kupitia app ya TikTok, utaweza kurekodi video zenye urefu wa sekunde 15 hadi sekunde 60.
Ili kurekodi fungua sehemu hiyo kisha bofya kwa kushikilia kitufe chekundu kilichopo chini mwisho wa kioo cha simu yako, angalia kwa juu utaweza kuona mstari wenye kuonyesha muda wa video, hii itakusaidia sana ili kujua pale sekunde 15 au 60 zinapofikia mwisho.
Effect za TikTok
Wakati unarekodi upande wa kulia utaweza kuona sehemu mbalimbali ambazo zinaweza kukusaidia kufanya mambo mbalimbali, sehemu ya kwanza juu itakusaidia kubadilisha kamera ya mbele na nyuma. sehemu inayofuata itakupa uwezo wa kuongeza speed ya video, sehemu inayofuata utaweza kuweka filter mbaimbali na sehemu inayofuata itakupa effect ya Beautify na sehemu ya mwisho ni sehemu ya kuweka Timer ambayo najua kila mtu anafahamu.
Kuweka Sauti au Sound kwenye Video zako za TikTok
Kabla ya kurekodi video yako kama unataka kurekodi video ambayo wewe unaimba nyimbo za wanamuziki maarufu basi unaweza kutumia sehemu ya Sound kuweza kuweka sehemu ya nyimbo ya msanii unaemtaka. Unaweza kubofya sehemu ya Sound iliyopo juu mwanzo kwenye app ya TikTok.
Baada ya kubofya hapo utaweza kuletewa ukurasa ambao unaweza kutumia kutafuta nyimbo unayotaka, au unaweza kutumia nyimbo yoyote ambayo ina trendy kwa muda huo au kwa maneno mengine kama nyimbo imetumika sana ndani ya app hiyo na watu wa Tanzania basi utaweza kuiona hapo juu pale unapo fungua ukurasa huo.
Baada ya hapo unaweza kuchagua nyimbo unayopenda kisha anza kurekodi na utaweza kuona nyimbo inaimba kila utakapokuwa unabofya na kushilia kitufe cha kurekodi. Baada ya hapo sasa unaweza kuendelea kwa kuchagua sehemu ya maneno yaani description kisha chagua hashtag kwani hizi ni muhimu sana kwenye mtandao wa TikTok, baada ya hapo sasa post video yako.
Kurekodi video zenye Sauti za Watu Wengine
Kama unataka kurekodi video ambazo zinakuja na sauti za watu wengi, unaweza kufuata hatua hizi fupi. Hatua ya muhimu unapokua una angalia video yenye maneno ambayo umeyapenda moja kwa moja bofya kufe kilishopo chini upande wa kulia kwenye kona, kitufe hicho kinaonekana na kinazunguka na kutoa alama za muziki.
Bofya hapo kisha bofya use this sound, na moja kwa moja anza kurekodi kwa kushikilia kitufe cha katikati chekundu na utaweza kuona sauti hiyo inaongea nyuma ya video yako wakati ukiwa unarekodi. Baada ya hapo unaweza kupost video yako moja kwa moja.
Hadi hapo natumaini utakuwa umeweza kutumia mtandao wa TikTok kwa urahisi kabisa, kama kunayo sehemu yoyote ambayo utakuwa umekwama basi unaweza kutuandikia kupitia sehemu ya maoni hapo chini. Kwa maujanja zaidi, unaweza kujifunza hapa jinsi ya kudownload video za TikTok bila kuwa na logo ya TikTok kwenye video hiyo. Kujifunza mambo mbalimbali kwa haraka nakushauri ujiunge na channel yetu kupitia mtandao wa YouTube hapa.