Wakati vita dhidi ya virusi vya corona vikiendelea, pia vita vya kampuni za teknolojia kugombea kuwa platform bora ya kuwasiliana kwa njia ya video bado inaendelea. Siku chache zilizopita, kampuni ya Google ilizindua Meet, sehemu mpya ya kuwasiliana kwa njia ya video kupitia huduma mbalimbali za Google.
Kama haitoshi sasa kampuni ya Facebook nayo imezindua rasmi sehemu mpya ya kuwasiliana kwa njia ya video inayoitwa Rooms. Kama ilivyo huduma ya Google, Facebook Rooms nayo inapatikana kwenye huduma mbalimbali za Facebook kama vile Facebook yenyewe pamoja na Facebook Messenger na huduma nyingine za Facebook kama WhatsApp na Instagram.
Kwa sasa Rooms inapatikana kwenye facebook pamoja na kwenye facebook messenger, huku baadae sehemu hiyo ikitarajiwa kuja kwenye programu za WhatsApp na kupitia kwenye sehemu ya DM kwenye programu ya Instagram.
Kwa sasa utaipata Rooms kupitia Messenger kwa kufungua app ya Messenger kisha bofya sehemu ya People na moja kwa moja juu ya ukurasa huo utaweza kuona sehemu ya Create a Room ikiwa kwa juu mwanzo kabisa wa ukurasa huo.
Pale unapo tengeneza Rooms utaweza kuchagua watu waweze kujiunga na moja kwa moja kwa kushare link ya Room na video chat yako itaweza kuonekana moja kwa moja kwenye sehemu ya facebook home feed na mtu yoyote aliye na link yako ataweza kujiunga moja kwa moja.
Tayari sehemu hii ya Rooms inapatikana kwa watumiaji wote wa Messenger na unaweza kupata Rooms kupitia app ya Messenger, na baadae tegemea kuona sehemu hii kupitia app ya WhatsApp pamoja na Instagram kupitia sehemu ya DM au Direct Messenger.