in

Sasa Download (GTA V) Grand Theft Auto V Bure Bila Kulipia

Utaweza kupata toleo zima la GTA V bure kabisa kwa njia halali na bila kulipia

Sasa Download (GTA V) Grand Theft Auto V Bure Bila Kulipia

Kama wewe ni mpenzi wa game basi najua pale naposema GTA V au Grand Theft Auto V basi unanielewa. Kama bado hujanielewa hebu ngoja nitafute namna rahisi ya kuweza kukelewasha. Unaweza kuanza kwa kuangalia video hapo chini ya Trailer.

Zipo trailer nyingi sana za GTA na unaweza kutafuta mtandaoni na utaweza kuona jinsi game hiyo ilivyo maarufu na inavyo pendwa. Sasa baada ya hayo moja kwa moja ngoja nikwambie njia ya kupata game hii bure kabisa bila kulipia. Njia hii ni halali kwa aslimia 100 na utapata game ambayo unaweza ku-update kila itakapo ongezewa kwenye kifaa chako.

Unchotakiwa kufanya ni kutengeneza akaunti ya Epic Games ambapo kupitia tovuti hiyo wanatoa game za bure kila wiki siku ya jumatano. Utaweza kupakua game hiyo kwenye kifaa chako na utaweza kutumia kadri utakavyo. Kwa sasa Epic Games inatoa Grand Theft Auto V ambayo itakuwa bure hadi tarehe 21 ambapo game hiyo itaisha kuwepo kwenye ofa hiyo ya bure.

Sasa Download (GTA V) Grand Theft Auto V Bure Bila Kulipia

Kwa sasa unacho takiwa kufanya ni kujiunga kwenye tovuti ya Epic Games , tengeneza akaunti kisha baada ya hapo unaweza kurudi kwenye tovuti hii na bofya link hapo chini na moja kwa moja utapelekwa kwenye ukurasa wa kupakua Grand Theft Auto V Premium Edition bure kabisa bila kulipia. Bofya Hapo chini Kujiunga au kama unayo akaunti utapelekwa kwenye ukurasa wa kupakua game moja kwa moja kwenye kifaa chako.

Pia kupitia link hii unaweza kuwa unapata games mbalimbali za bure kabisa kupitia kwenye store ya Epic Games, hivyo kama umekosa game hii ya Grand Theft Auto V Premium Edition unaweza kutumia link hiyo kupata games nyingine za premium edition kwa kutumia link hiyo.

PAKUA GTA V BURE HAPA

Amani Joseph

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.