Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

YouTube Kuja na Shorts Sehemu Mpya Inayofanana na TikTok

Jiande kuweka video zako fupi zenye muziki kwa nyuma kupitia YouTube
YouTube Kuja na Shorts Sehemu Mpya Inayofanana na TikTok YouTube Kuja na Shorts Sehemu Mpya Inayofanana na TikTok

Hapo kipindi cha nyuma, YouTube ilikuwa ni moja kati ya mtandao pekee ambao ilikuwa ukitegemewa zaidi kwenye upande wa video za mtandaoni. Miaka kadhaa baadae, TikTok nayo sasa imeingia na hadi sasa naweza kusema, TikTok ni mmoja ya mtandao mkubwa sana unao tegemewa na watumiaji mbalimbali duniani kote hasa kwenye mtindo mpya wa video fupi.

Kama unavyojua, “ukiwa mkubwa upendi kushindwa na wadogo zako”, hivyo hivi karibuni YouTube imeanza kufanyia kazi sehemu mpya ya Shorts ambayo inasemekana kufanana na mtandao wa TikTok. Kwa mujibu wa tovuti ya The information, sehemu hiyo mpya itakuwa inaishi ndani ya mtandao wa YouTube na itawaruhusu watu kuweka video fupi pamoja na muziki kwa nyuma kama inavyofanya TikTok.

Advertisement

YouTube Kuja na Shorts Sehemu Mpya Inayofanana na TikTok

Mpaka sasa bado hakuna anaejua muonekano wa sehemu hiyo mpya, ila kwa mujibu wa tovuti ya The information, sehemu hiyo inategemea kuzinduliwa rasmi mwishoni mwa mwaka huu 2020.

Kwa sasa TikTok ni moja ya mtandao unao ongoza kwa video fupi ambazo zinakuja na muziki kwa nyuma, video ambazo ndio zimesaidia mtandao huo kukuwa kwa kasi zaidi huku ukiwa na zaidi ya watumiaji walio pakua app hiyo milioni 842 kutoka kwenye masoko ya Apple App Store na Google App Stores kwa muda wa miezi 12 iliyopita, hiyo ikiwa ni sawa na ongezeko la downloads kwa zaidi ya asilimia 15 kwa muda wa mwaka mmoja. App Annie imeripoti.

Hii sio mara ya kwanza YouTube kuleta sehemu mpya zinazo fanana kutoka kwenye mitandao mingine. YouTube ilileta sehemu ya Stories baada ya kuona ongezeko la watumiaji wa sehemu kama hiyo kupitia mtandao wa Instagram. Mbali na YouTube, Facebook nayo inapambana kuja na sehemu yake kama TikTok inayoitwa Lasso, sehemu ambayo tayari imeanza kufanyiwa majaribio ya kimya kimya huko nchini Brazil.

Kwa sasa tuendelea tu kusubiri na huwenda moja ya sehemu hizi inaweza kweli kuja kushindana na mtandao wa TikTok ambao kwa sasa unaendelea kuwa na watumiaji wengi zaidi.

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use