Kampuni za kutoa huduma za simu za Vodacom na Safaricom zimetangaza kuwa zimekamilisha kwa pamoja ununuzi wa chapa ya M-Pesa ikiwa pamoja na bidhaa huduma za msaada za M-Pesa kutoka kampuni ya Vodafone.
Kwa mujibu wa Forbes, ununuaji huu uliripotiwa mwaka jana 2019, ambapo walitaka kununua haki za M-Pesa kwa zaidi ya shilingi za kitanzania Bilioni 20, hii ikiwa imekusudiwa kufanya Safaricom na Vodacom kumiliki asilimia 100 ya M-Pesa ili kuwezesha huduma hiyo kuendelea kusaidia watumiaji zaidi na kupanua huduma hiyo kwenye masoko mengine barani Afrika
“Kwa Safaricom, tunafurahi kwamba usimamizi, msaada na maendeleo ya jukwaa la M-Pesa sasa limehamishiwa Kenya, ambapo safari ya kubadilisha ulimwengu wa malipo ya simu yaliyo safari iliyoanza miaka 13 iliyopita. Ushirikiano huu mpya na Vodacom utaturuhusu kujumuisha maendeleo ya jukwaa hili, kusawazisha njia za huduma, na kuboresha uwezo wetu wa kufanya kazi zaidi na kuwa Kituo kizuri cha kuunganisha wateja wetu, “Mkurugenzi Mtendaji wa Safaricom, Michael Joseph alisema.
Safaricom ilikuwa ikilipa asilimia 2% ya mapato yake ya kila mwaka ya M-Pesa kwa Vodafone kama mrahaba. Safaricom ilipata mapato ya Kshs bilioni 75 katika mwaka wao kamili wa fedha, ambayo inamaanisha kuwa walilipa Vodafone Bilioni 1.5 kama mrabaha. Vodacom pia inalipa 5% kama ada ya mali ya akili kwa Vodafone kwa biashara yake ya M-Pesa ambayo iko hapa nchini Tanzania.
M-Pesa ina zaidi ya watumiaji milioni 40 barani Africa, huku ikiwa inafanya kazi kwenye nchi saba hadi sasa, nchi hizo zikiwa ni pamoja na Tanzania, Kenya, Lesotho, DRC, Ghana, Msumbiji pamoja na Misri.