in

Jiandae na Simu Mpya za TECNO CAMON Nchini Tanzania

Tegemea kukata kiu yako ya kuwa na simu yenye kamera bora

Jiandae na Simu Mpya za TECNO CAMON Nchini Tanzania

Kampuni kinara ya simu za mkononi TECNO ndio kampuni inayosemekana na wadadisi wa masuala ya teknolojia ya simu kuwa huenda ndio itakayoleta teknolojia ya kamera ya simu ambayo kwa mara ya kwanza katika tasnia ya masuala ya simu janja Tanzania itakata kiu kwa watumiaji wa simu hizo hasa kwa upande wa kamera, betri na muundo wa simu yenyewe.

Toleo la simu hiyo halijawekwa wazi bado lakini imebainishwa kuwa litatoka kwenye mfululizo wa matoleo ya TECNO CAMON na litaachiwa sokoni ndani ya mwezi huu Aprili.  Simu hiyo imebainishwa itakuwa na kamera tatu nyuma lensi na flash ambapo kamera kuu ina MP 64.

Install Android App
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot

Jiandae na Simu Mpya za TECNO CAMON Nchini Tanzania

Teknolojia ya kamera ya simu hii inaelezwa kuwa na uwezo wa kupiga picha mahali popote hata gizani kutokana na kuwa na flash nne zenye uwezo na nguvu kubwa ya kusawazisha picha ing’are sehemu zenye ukungu na giza huku lensi yake ikimwezesha mtumiaji kupiga picha kitaalam zaidi hata kama hana ujuzi wa kupiga picha.

Kwa taarifa zilizotufikia ni kwamba upande wa kamera ya mbele ina MP 32 huku ikiwa tofauti kabisa na simu nyingine kwa namna ilivyoundwa kwani iko ndani ya simu ambapo mtumiaji akitaka kupiga selfie, kamera hii huchomoza kwa juu wengine huita Pop- Up Camera.

TECNO ambayo simu yake ya mwisho katika mfululizo wa CAMON ni CAMON 12, ndio kampuni inayotarajiwa kuleta madiliko haya makubwa ya teknolojia ya kamera za simu kwa mwako huu 2020.

Kwa upande wa sifa nyingine endelea kufuatilia taarifa zetu tutawapa mrejesho mara tu baada ya kupata taarifa rasmi kutoka TECNO.

Jiandae na Simu Mpya za TECNO CAMON Nchini Tanzania
Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Infinix na JBL Waungana Tena Na Sasa Ni Infinix Note 40

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.